Rais Samia akutana na rais wa TLS, Mwabukusi - Ikulu ya Chamwino Dodoma

Rais Samia akutana na rais wa TLS, Mwabukusi - Ikulu ya Chamwino Dodoma

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,274
Reaction score
9,326
UPDATES KUTOKA KWA MWAMBUSI: - Leo Nimefika Ikulu CHAMWINO kuwasilisha Majumuisho ya wadau na tulipata nafasi ya kuzungumza na Kumueleza Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano kuhusu Utawala Bora,Haki zabkushiriki katika chaguzi za kidemokrasia,Masuala ya Utekwaji na enforeced Disappearance , Kuhusu Umuhimu wa kuwa na chaguzi zinazozingatia haki za wananchi kupata,Watu na wagombea kutokuondolewa kwa kukatwa kwa masuala ya kiufubdi na Maeneo yenye kuhitaji maboresho ili kuwa na uchaguzi mzuri ulio Huru na wa Haki ili kupata viongozi wanao wataka kupitia sanduku la kura.

Mh.Rais Ametusikiliza na kuahidi kuangalia namna bora ya Kufanya kwa mambo yatakayowezekana kwa muda uliopo na kuboresha ili kuwa na Uchaguzi huru na Haki.

Aidha kwa kuwa kulikuwa na Mapendekezo ya Muda mfupi,Muda wa kati na Muda mrefu ameahidi kuyapitia yote na kuona namna bora ya kuyatekeleza.

BAK Mwabukusi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 27 Agosti, 2025.

snapins-ai_3708556221765270491.jpg
snapins-ai_3708556221740145797.jpg
 
Huyu Mama sasa kaona maji yanazidi unga ndio maana anakubali kukutana na watu tena bila mashariti.

Kwa aliyotamka jana Rais wa TLS, angemuwekea kinyongo na wala asingekubali kukutananae.

Unaomba kikao na Rais Leo, kesho unakutananae!

Si bure hapa.
 
Back
Top Bottom