Rais Samia akutana na rais wa TLS, Mwabukusi - Ikulu ya Chamwino Dodoma

Rais Samia akutana na rais wa TLS, Mwabukusi - Ikulu ya Chamwino Dodoma

Hivi wewe ndugu yangu mbona uko kimya sana siku hizi tofauti na wakati ule dr. Slaa anagombea? njoo utoe nasaha zako humu walau ,mara moja kwa wiki au share zile linki zako za KLH News - Kijijini leo hii.. humu ndani.
Mzee MM aliingia kwenye mtanzuka wakati wa kubadilisha gia angani" 🤔...ila baada ya mapinduzi ya Januari 21,2025 ni heri arudi tu!
 
UPDATES KUTOKA KWA MWAMBUSI: - Leo Nimefika Ikulu CHAMWINO kuwasilisha Majumuisho ya wadau na tulipata nafasi ya kuzungumza na Kumueleza Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano kuhusu Utawala Bora,Haki zabkushiriki katika chaguzi za kidemokrasia,Masuala ya Utekwaji na enforeced Disappearance , Kuhusu Umuhimu wa kuwa na chaguzi zinazozingatia haki za wananchi kupata,Watu na wagombea kutokuondolewa kwa kukatwa kwa masuala ya kiufubdi na Maeneo yenye kuhitaji maboresho ili kuwa na uchaguzi mzuri ulio Huru na wa Haki ili kupata viongozi wanao wataka kupitia sanduku la kura.

Mh.Rais Ametusikiliza na kuahidi kuangalia namna bora ya Kufanya kwa mambo yatakayowezekana kwa muda uliopo na kuboresha ili kuwa na Uchaguzi huru na Haki.

Aidha kwa kuwa kulikuwa na Mapendekezo ya Muda mfupi,Muda wa kati na Muda mrefu ameahidi kuyapitia yote na kuona namna bora ya kuyatekeleza.

BAK Mwabukusi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 27 Agosti, 2025.

View attachment 3455282 mView attachment 3455283
Huyu mwamba anafaa kuwa waziri mkuu
 
NILIKUPENDA SANA MAMA SAMIA KIPINDI KILE ULIPOINGIA OFISINI, -KWENYE URAIS., BAADAYE UKANIGEUKA.

HUJACHELEWA MAMA, NAFASI BADO UNAYO YA KUREKEBISHA MAMBO! HATUA YA MWANZO KABISA, AHIRISHA MICHAKATO YA UCHAGUZI MKUU, KAA MEZANI NA WADAU WOTE WA UCHAGUZI, TENGENEZENI TAIFA. NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE MAMA.

cc Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kwa sasa ni maagizo tu! Nadhani Mama atayafanyia kazi au kutoyafanyia kazi kabisa kuanzia 2026!
Kampeni zinaanza leo pale TP Kawe kwenye jimbo la Gwajima.
 
Kwa jinsi navyomuona Mwabukusi, hata kama analambishwa asali lakini si yeye anayeanzisha ombi la asali bali analazimishwa kulamba asali.

Namanisha, kuna watu wakienda sehemu ni kujichekesha chekesha na kunawa mikono na kusifia sifia mwisho wa siku wanaomba asali.

Kwa Mwabukusi inaweza kuwa tofauti kidogo, akienda sehemu lazima atoe changamoto bila kuomba asali, labda wao wenyewe ndio waanze kumbembeleza na vitisho juu. Katika hali ya kawaida, anachukua asali huku akipiga mkwara kwa sababu ni ngumu kushindana na chama tawala kinachomiliki dola. Ni mtu mmoja tu Tanzania anayeweza kugomea asali.
huyo mtu ni TAL

#FREE LISSU#
 
Sina imani na hicho kikao bora kingefanyikia youtube live
 
Huyu Mama sasa kaona maji yanazidi unga ndio maana anakubali kukutana na watu tena bila mashariti.

Kwa aliyotamka jana Rais wa TLS, angemuwekea kinyongo na wala asingekubali kukutananae.

Unaomba kikao na Rais Leo, kesho unakutananae!

Si bure hapa.
Nadhani tumpongeze mh Rais kwa kukubali kuanza kukutana na wenye mawazo tofauti na serikali, mwanzo mzuri. Nadhani Kuna siku atakutana na kina heche na timu yake.
 
..TLS wanaponzwa na haiba ya Chadema ktk kutetea HAKI.

..yeyote anayetetea haki sasa hivi anaonekana kama ni mfuasi wa Chadema.

..hata viongozi wa Dini wakitetea haki wanaambiwa wanachanganya dini na siasa, na kuwa ni wana Chadema.

..vivyo hivyo kwa asasi na vyama vya kitaaluma.

..kwa upande wangu naamini TLS walipaswa kufanya zaidi ya wanavyofanya sasa hivi.
Sure
 
Back
Top Bottom