Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Lakini Rais anafuata Ilani ya chama ambayo imeweka mkazo kwenye value addition kuanzia sekta ya viwanda hadi utalii. Huoni sekta ya Utalii kufanya innovation kama hizi kuongeza thamani ya Utalii wetu sio kazi ya Rais?? Kama katiba ndio Kila kitu je Ilani kazi yake ni nini inayomuelekeza Rais Kila anachopaswa kufanya??

Kingine mbona JPM Ali involve kwenye Extra Curricular activities mfano alienda mechi za Ligi kuu, alikua anapost video akishangilia ushindi wa Taifa Stars, aliwahi kupiga simu live kipindi Cha shilawadu kusema anawafuatilia Kila ijumaa. Hizo zote ni PR tu Wala hatukuona wananchi mkilalamika ila nashangaa kwa Mama imekua nongwa.
Ushamba unawasumbua bado wana zile akili za mwanaume akitembea uchi ni poa tu lakini mwanamke akifanya hivyo hivyo ni mwendo wa kumdhalilisha.

Haya ni matatizo ya mfume dume uliotulea, ni akili fulani za kipuuzi tu zilizopitwa na wakati.
 
Alama ya nchi akiwa ni mama wa miaka 62 sio binti wa miaka 18. Kumbuka hilo, na hizi ni akili za kimfumo dume sio kingine chochote.

Angekuwa amefanya haya mambo Hayati Mkapa au Magufuli usingepoteza muda wa kuandika yote aliyoandika sana sana ungemsifu kwa kumpamba kwamba ni kidume kweli kweli.

Tuachane na haya masuala ni madogo sana, na ukiyafuatilia sana ni kielelezo cha wewe kuwa mpenda habari za udaku. Yale yale ya watanzania wanaopoteza pesa nyingi kununua magazeti ya UWAZI na CHEKA wakiachana na magazeti kama Citizens na Daily News.
Hayo mengine sitakujibu..
Hapo kwenye DailyNews ndo nimekuona na wewe ni mpenda propaganda tu.
Sasa,DailyNews,Habari Leo na Uhuru ni magazeti ya kusomwa na mtu serious?
 
Maneno mazito !!
Hayo yote ndio mapungufu tuliyonayo kama taifa!.Tunaviamini vyama na watu kuliko katiba ya nchi. JPM alikuwa anatenda makosa mengi tu kwa kisingizio cha ilani ya uchaguzi. Vyama hasa CCM vimehodhi mamlaka ya kuamua lolote bila kuzingatia katiba ya nchi. Hii imepelekea vyama kuanza kushindana ili kushika Dola! .... Na vyama karibu vyote vimekuwa na tabia ya kuwasemea wananchi hata kama hawakutumwa.

Nongwa unayoisikia kwa SSH inatoka kwenye kundi lisilofungamana na chama chochote, kundi hili ni kubwa, hawatumii majukwaa kujinadi ila wana manung' uniko kuhusu kile kinachoendelea. Mitaani wapo wanaohoji bila ushabiki na kuonyesha kutoridhishwa na matendo yanayofanywa na vyama. Makosa ya JPM hayawezi kuhalalisha ukiukwaji wa katiba wala kumhalalisha SSH na chama chake waendelee kuvunja katiba na sheria za nchi.
 
Nikama vile Jiwe alivyotaka kuliangamiza Taifa. Ila swala la Jiwe kupata Corona usingelisikia hata kidogo kwani kwenye usukani walikuwepo Sukuma gang. Jiwe kafa kwa corona sababu ya kuamini ushirikina kuliko science
Jiwe alichanja chanjo ya corona.
 
Mbona kama una wivu sana na watu waliofika Us kupitia Mama? Jiwe aliishia kuwapeleka chato
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wivu wa nini boss? kwani unafahamu naishi wapi? Kulikuwa na mazungumzo kuhusu walioajiliwa ikulu, umeiona? Au unasoma kama mistari ya Biblia na Kuruani halafu unajibu?
Kuna sehemu serikali hitakiwi kuajili watu wenye elimu ya hapa na pale; Ikulu, BoT, Usalama wa Taifa. Sasa ikulu yetu hujazwa marafiki wa rais, waziri mkuu. Nzuri wawe marafiki na elimu ya kutosha, sasa hawa wetu.. Dah!
 
Kuwa mstaarab japo kwa kujifanyisha tu. Yule ni sawa na Mama yako au shangazi yako.
Nawe boss sasa una makuu. Akishakuwa sawa na mama yake au shangazi yake ndo asiambiwe kuacha tabia mbaya? Ktk familia yako wazazi hawajawahi au hawakuwahi kukatazwa mambo machafu na ninyi watoto wao?

Rais wa nchi ni heshima ya nchi, siyo heshima ya familia yake. Rais wa nchi anabebewa hata mafaili au karatasi za hotuba kwa heshima ya nchi. Iweje ashikwe kama abiriria wa dala dala?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwani neno primitive ni tusi?
Inategemea na kiwango chako cha elimu. Kama ni darsa la 12 ukiangalia kwenye kamusi utaliona powa tu! Lakini tulio na elimu ya juu tunafahamu mzungu analitumia kumaanisha nini.
 
Primitive siyo tusi;
(Relating to, denoting, or preserving the character of an early stage in the evolutionary or historical development of something)

Kama hujui Kiingereza sema nitaweka kwa Kiswahili
OK! Umeangalia kwenye kamusi? KWa walio na elimu ya sekondari munaona ni powa tu! Lakini sisi wana sociolojia tunafahamu huyo mzungu alimaanisha nini kutumia neno hilo.
Siku nyingine jaribu kujifunza tabia za wengine usijejikuta unachekelea matusi.
 
Nawe boss sasa una makuu. Akishakuwa sawa na mama yake au shangazi yake ndo asiambiwe kuacha tabia mbaya? Ktk familia yako wazazi hawajawahi au hawakuwahi kukatazwa mambo machafu na ninyi watoto wao?

Rais wa nchi ni heshima ya nchi, siyo heshima ya familia yake. Rais wa nchi anabebewa hata mafaili au karatasi za hotuba kwa heshima ya nchi. Iweje ashikwe kama abiriria wa dala dala?
Tabia ya ndani kabisa ya wanaoponda Mama kushikana mikono na Greenburg ni uhanga wa mfumo dume. Angekuwa amefanya hivyo Kikwete, RIP Mkapa au RIP Nyerere hakuna ambaye angesimama na kuanza kuandika haya yaliyoandikwa humu ndani.

Ni nongwa za kijinga tu, unyanyasaji wa jinsia yake. Ukishangaa Samia kumshika mkono mzee wa kizungu utashangaa sana aliyekuwa Chancellor wa Ujerumani namna alivyokuwa na ukaribu na viongozi wengine wa dunia hii.
 
OK! Umeangalia kwenye kamusi? KWa walio na elimu ya sekondari munaona ni powa tu! Lakini sisi wana sociolojia tunafahamu huyo mzungu alimaanisha nini kutumia neno hilo.
Siku nyingine jaribu kujifunza tabia za wengine usijejikuta unachekelea matusi.
Unakuja kwenye JF na kutamba kuwa wewe ni mtaalamu wa sociology!! Fani za kimama hizo za kukifunza maneno kwa ajili ya kuchamba.

Kama wewe MchunguZI ni mwanaume basi umesoma fani za kimama
 
Kwani utamaduni wa Tanganyika ni kuuwa watu ? Mbona kuanzia 1964 mumeikalia Zanzibar kwa mabavuu Na mnaendelea kuuwa watu kila uchaguzi/ uchafuzi unapofika, mkilazimisha kuweka vibaraka wenu?
Waambie hao pumbaf zao
 
Inategemea na kiwango chako cha elimu. Kama ni darsa la 12 ukiangalia kwenye kamusi utaliona powa tu! Lakini tulio na elimu ya juu tunafahamu mzungu analitumia kumaanisha nini.
Unataka kukuza vitu unnecessarily. Hakuna tusi hapo. Wamaasai wamebaki na culture na traditions zao hata baada ya wazungu kuleta mambo mageni. Mfano wamebaki na mavazi yao pamoja na kwamba baadhi hasa walioenda shule wanavaa mavazi ya kawaida.
 
Wa-TZ wenzangu!

Wakati wa Wikileak nilitambua walioendelea na hasa US wanatumia maafisa wa ubalozini ili kuzifahamu nchi walimo. Balozi zao zinatumika sana kuwaelewesha tabia za viongozi wetu; uwezo na udhaifu wao.

Ina maana Peter Greenberg alikuja akiwa director wa film lakini naaamini kupitia ubalozi wake alishafahamu tabia za rais wetu hadi mambo ya ndani, na ukiangalia film hii, rais alichotwa akili hadi akamuona ni rafiki kuliko hata sisi wa-TZ.

Ukiangalia Film ya Royal Tour kiutu uzima, (Siyo kama mtoto anayefurahia wanyama) inatia kichefu-chefu jinsi rais wa nchi alivyopunguziwa thamani hadi kufikia kuwa mcheza film akiwa ikulu. Walifikia hatua ya kuitana majina kama wana mahusiano ya ziada. Peter! Mama Samia!

Haya yangeondolewa wakati wa ku-edit! Nadhani yaliachwa makusudi na naamini kwa uhusiano huu Peter sasa atatumika kiurafiki kuwasiliana na rais moja kwa moja.

Kule twitter Maria Sarungi kaibua jingine nami nimethibitisha. Wamasai wanaitwa ni 'PRIMITIVE' na huyo director wa film na ikaachwa kama sehemu ya maelezo ya film ya Tanzania! Yaani tuna raia PRIMITIVE! Rais Samia anaambiwa Magufuli alipatwa na COVID anakubali, Yeah! wakati wa-TZ hatujawahi kuambiwa jambo kama hilo. Kwa nini haya yote yametokea?

Ikulu yetu haina usalama. Namaanisha watu wanaostahili kumulazimisha rais aendane na matakwa ya taifa na siyo uamuzi wake, hawapo na hawana nguvu hizo. Ina maana rais mzembe anaweza angamiza taifa. Tabia zake binafsi zinatambaa na anazungukwa na watu wa aina yake bila kizuizi.

Very, Very Sorry!
This is best for the president, sijui nilisikia wapi??
 
Mimi naogopa kusema sana lakini tangu mwanzo nilipinga rais wa nchi kuigiza kwenye movie nionyesheni royal tour zingine nilizoigizwa na rais wa nchi!!!! labda rais wa bongo movie zao
 
Mimi naogopa kusema sana lakini tangu mwanzo nilipinga rais wa nchi kuigiza kwenye movie nionyesheni royal tour zingine nilizoigizwa na rais wa nchi!!!! labda rais wa bongo movie zao

Ona hii

Back
Top Bottom