Rais Samia aliweka wazi kuhusu ongezeko la mshahara, 23.3% ni kwa kima cha chini tu. Watumishi acheni lawama mara moja

Rais Samia aliweka wazi kuhusu ongezeko la mshahara, 23.3% ni kwa kima cha chini tu. Watumishi acheni lawama mara moja

kuna watu wameongezewa 250k.

kama kuna watu atawaongezea 50k na mishahara yao duni basi ni tapeli.
Hakuna kitu kama icho,hiyo increment si ya salary peke yake Bali na posho ambayo pia calculation yake hufanyika kwa kuangalia mshahara mpya
 
Kwenye maisha ya kawaida ukikutana na mtu awe kijana au mzee akaanza kejeli kwa kundi au watu anaodhani wako chini yake kimaslahi au kielimu, usijaribu kujadili naye , Mkimbie kabisa kwani mnajadiliana kitu ambacho mtakuja kujutia baadae.
Huyu kijana/mzee pasina shaka kabisa, amekosa malezi bora na kuendelea kujadiliana naye hapa ni kuunga mkono hoja yeke dhidi ya Walimu.
Sitaki kuamini kama kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kunyanyua mdomo wake akawadhihaki Walimu, tulifundishwa na Walimu walioshia darasa la 7 tukajua kuandika na kusoma, hata tulipofika vyuoni bado hatukuona Walimu wetu wale ni wajinga. Mada hii ingejikita tu kwenye ongezeko la mshahara ila kwa kuwatukana Walimu hii ni dalili ya kukosa adabu kwa kisingizio cha Uhuru wa kuongea.
Jukwaa kubwa kama hili ifike hatua liweke mipaka ya kujadiliana, unaruhusu vipi dharau hii kwa kisingizio cha Uhuru wa kijadiliana? Mjadala bora ni ule usioruhusu kutweza utu/ hadhi ya mwingine kwa namna yoyote ile.
 
Hakuna kitu kama icho,hiyo increment si ya salary peke yake Bali na posho ambayo pia calculation yake hufanyika kwa kuangalia mshahara mpya
Ni kweli mf vyombo vya ulinzi na taasisi za serrkali posho na allawance zao zilizo nyingi zipo kwenye salary slip zao ndo maana ongezeko kubwa
Lakini watumishi wengine hasa Tamisemi ambao posho na allowance zote utalipwa na mwajiri wako ambaye ni mkurugenzi salary slip yako ina mshahara tu lazima uzimie(haya najiuliza kwa watumishi wengine posho zao na allawance zisiingizwe kwenye salary slip badala yake unaambiwa mkurugenzi atalipa mkurugenzi halipi na ukidai hizo stahiki utaambiwa mkorofi na taabu utaipata na unaweza kupelekwa polini huko hata kuja mjini unajifikiria huku ni kurusu kundi flani kula pesa za watumishi)
 
Hakuna shida, tutaendelea kuiba na kula rushwa. Rushwa na uwizi nchi nyingine walipunguza kwa kuangalia haki na stahiki za mtumishi pamoja na kudhibiti mfumuko wa Bei ili kufanya balancing ya anachopokea mwananchi na anachotumia.

Wewe endelea kufurahia unaowaita walimu/wafanyakazi kutokulipwa 23% Kama nyongeza, wakati huohuo watu wanapitisha mizigo kwenye miboti bure bila kulipa kodi kwenye bandari zetu.
Naunga mkono hoja.
Ukipata Target lenga
 
😀😀😀 ukiachana na nyuzi za kuchakatana , nyuzi hizi pia za 23.3% huwa zinakuaga ndefu kishenzi !!! Wengine tuko chimbo tunakomaa boss nae hela ya boda boda anataka hadi jumapili !! Mkiongezewa ,msipoongezewa mtajijua
Sema msiparurane bhana !!! 😀 nimesoma toka mwanzo mishahara ni watumishi wote !! Ila anayewashiwa moto ni Teacher !! Kumbe na daktar nae anasikilizia , mhasibu nae haelewi.
Tupendane wadau
 
Kila jicho linalosubiria ongezeko la mshahara hatimaye litaona kilichoongezwa. Tusitukanane na kubezana.

Kama mtoa mada kamba yake ni ndefu (pengine ukuu wa wilaya manake ana kawaida ya kumsifia mkuu wa wilaya fulani) ale kwa utulivu. Kamba huwa zinakatika wakati mwingine by surprise.
 
Chifu Hangaya kawakaanga watumishi! Ni vilio na majonzi kwa wananzengo wa "wako mtiifu"
Utakumbukwa Sana JPM kwa KUSEMA UKWELI, asilimia 23. 3% ndiyo sh. 8,000 elfu nane kweli!
Poleni Sana watumishi wa imma, njoooni huku kwenye dhahabi tupige pesa!
Toa uelekeo wa lilipo hilo chimbo la dhahabu mkuu. Hakuna asiyependa kufanikiwa.
 
Inabidi iandikwe: mtu hataishi kwa mshahara tu, bali kwa kujiongeza na vishughuli vya ujasiriamali.
 
1. Mtoa mada, uwaombe radhi walimu kwa kuwashambulia bila kuweka bayana uthibitisho wa kada hiyo ilivyolaumu.

2. wewe mwenyewe ktk mada hii umedhihirisha kuwa haujui lolote juu ya Namna nyongeza za mishaha zinavyokokotolewa, vinginevyo basi ungeweza kuwaelimisha hao unaowalaumu zaidi tu umewashambulia kwa maneno ya ujinga wako.

3. Labda tu ufahamu kuwa hata hawa wanaojadili humu wengi si walimu hivyo punguza mtazamo hasi juu ya walimu huku ukikumbuka kuwa hata huu ujinga unaowarushia pengine unatumia vibaya maarifa yao waliyokupatia.

4. Nikufahamishe kuwa walimu wanajua vema namna mishahara inavyoongezwa na walilielewa vema tangazo la Rais.

Kwa ufupi tu ni kwamba wanaposema nyongeza ni 23.3% kwa kima cha chini ni kwamba atakayeongezewa hizo asilimia kama zilivyo ni mtumishi wa Daraja la kima cha chini, madaraja mengine yatakuwa yanapata nyongeza pungufu kutokana na kanuni yahesabu itakavyokuwa imepigwa (hii nayo utapewa elimu ukiihitaji). Hufanyika hivi ili kuweza kuwa na nyongeza inayokaribiana kwa madaraja yote maana wakifanya sawia walio na daraja la juu Sana watapanua wigo wa tofauti kubwa ya mshahara.
Mwalimu again....
 
Acha kejeli kijana watu wanafanya kazi kwa uvumilivu wa dhiki sio uzalendo
1)wengi wetu tumetoka familia duni,huo ualimu ndo cheo kikubwa kwenye familia
2)ujasilia mali unahitaji mtaji na wakati mwingine unajionea wezio wanaofanya ujasiliamali wanavyonyanya kwa kubomolewa vibanda na kufukuzwa unakataa tamaa na unaamua kubaki kufundisha

Kama wewe umebahatika kutoka kwenye familia nzuri na unapata maslahi mazuri mshukuru Mungu kwa kukupa upendeleo katika maisha na wengine tuliokosa tuhurumie na kutuombea ni watu tuliokosa tumaini na maisha.maana siku uvumilivu wa dhiki ikitoka mioyoni mwetu na kusema bac inatosha sijuwi kama tutabaki salama(watu wanamaumivu na haya maisha acheni kejeli)
Mimi naelewa yote hayo, tatizo ni mawazo na michango yenu sehemu mbalimbali zimewa-expose na kuwafanya muonekane watu wenye upeo mdogo sana. Pitia haya hii thread utaelewa
Walimu wa miaka ya 90 walikua vizur na akili ilikuwepo.
 
Hata hivyo tukirudi kwenye uhalisia kwa uchumi ulivyoyumba duniani na Tanzania tukiwemo, unawezaje kuhitaji ongezeko la 23.3%? Kwa kazi gani hasa unazofanya?
Najua una nia ya kuhujumu morali ya wafanyakazi wa Umma lakini hautafanikiwa. Wafanyakazi wa Umma wana uzalendo sana na nchi Yao. Wamevumilia miaka sita huku stahiki zao zikitumika kufanya miradi ya maendeleo bila kunung'unika. Kwa hiyo kupanda kwa asilimia 23.3 si issue kwao.
 
kakweli,NMB 2018 niliomba mkopo kwao ulikaa miezi 3 sijapata.

CRDB nao wanataka mshahara upitie kwao[emoji2][emoji2].
nipo hapa kuwa okoa watumishi ambao walio wengi hutegemea mikopo, chondechonde msikimbilie kukopa NMB hawafai, wanawaumiza watumishi badala ya kuwaokoa hivyo ni bora kwenda CRDB ambao wanamikopo ya magari, bajaji, pikipiki, nyumba n.k
 
Mtoa mada ni mfuasi wa mwendazake..hapa yuko kwenye ramli. Atafurahi ikiwa ongezeko litakuwa dogo. Atachukia ikiwa ongezeko litakuwa kubwa.
 
Mimi naelewa yote hayo, tatizo ni mawazo na michango yenu sehemu mbalimbali zimewa-expose na kuwafanya muonekane watu wenye upeo mdogo sana. Pitia haya hii thread utaelewa
Walimu wa miaka ya 90 walikua vizur na akili ilikuwepo.
Unaweza kinipa mchango mmoja uliotolewa na walimu ambao unaonyesha kuwa upeo wao mdogo sana.
Naomba uelewe kuwa walimu wanatumika kwenye kazi nyingi za serikali kutokana na uwingi wao na utii wao katika kazi
Kwahiyo usione kundi la walimu au mwl fulani fulani katoa mchango kwenye ghafla ya serikali ukamwona ana upeo mdogo hawezi kwenda kinyume na matakwa ya serikali na wakati mwingine hotuba unaandaliwa na kuambiwa ukasome na mkiandaa wenyewe watu wa serikali wanaichukua na kuisoma na kufanyiwa editing baadhi ya mambo ambayo yako kinyume na serikali
Hujawaona mawaziri na wanasiasa wengine wakitoa matamko ambayo hata mtoto wa darasa la saba anashangaa unafikiri ni akili yao au wnapenda? Ni maelekezo ya serikali
Kiufupi bado mchanga sana kwenye mambo ya serikali huyajuwi ni bora ukakaa kimya kuliko kukera wa2
 
Back
Top Bottom