Rais Samia amaliza mgogoro wa miaka kumi kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Rais Samia amaliza mgogoro wa miaka kumi kati ya Tanzania na Afrika Kusini

Nani mwanzilishi wa huko kutokuelewana kwa miaka 10 na Nini chanzo
 
If you take all the Credit when things go Right remember to take some of the Blame when they go Wrong...

Kwa sasa hapa kitu kilichopo wazi ni huu Mgao wa Umeme.., Ni sawa mtu unahangaika kuweka viraka kwenye soksi wakati viatu vyako havina soli...
 
Kumekuwa na mgogoro mkali wa kibiashara hasa ya Parachichi baina ya Tanzania na Africa ya Kusini uliodumu kwa mwongo mzima (miaka kumi) sasa bila muafaka wowote.

Mtakumbuka February, 2021 kabla ya ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan Jumla ya tani 3.514 za avocados|parachichi toka Tanzania zilizokuwa zinasafirishwa kwenda Africa ya Kusini mali ya Kuza African Company ziliharibiwa vibaya na mamlaka za Serikali ya Africa kusini.

Leo miezi tisa baadae chini ya Utawala madhubuti na imara uliojaa neema na furaha wa Rais Samia Suluhu Hassan Sasa rasmi ni ruksa kwa Mtanzania kuingiza na kuuza Parachichi Africa ya kusini,Hivi Watanzania tumtake nani kama sio Samia Suluhu Hassan?

Hili linafuatia ikiwa ni baada ya Serikali ya Africa ya kusini kupitia kwa taasisi yake inayoshughulika na Uhifadhi wa Mimea yaani National Plant Protection Organisation of South Africa (NPPOZA) kukubali kuruhusu biashara hii baada ya miaka kumi ya msuguano mkali baina ya nchi hizi mbili.

Makubaliano haya ni kwa mujibu wa barua kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Mimea Africa ya Kusini yaani South African Plant Health Ndg Jan Hendrik Venter ya tarehe 16|11| 2021 ikiwa ni baada ya nchi hizi mbili kukubaliana kwa njia ya Mtandao.
Hakuna Cha ajabu alichofanya,hizo ni diplomasia tu,hapo lazima na sie tumeachia kidogo.
 
If you take all the Credit when things go Right remember to take some of the Blame when they go Wrong...

Kwa sasa hapa kitu kilichopo wazi ni huu Mgao wa Umeme.., Ni sawa mtu unahangaika kuweka viraka kwenye soksi wakati viatu vyako havina soli...
Umeme kesi Closed sooner
 
Soko litakaa vizuri soon, tuchape kazi kwa bidii
Vipi exchange kati ya parachichi ya Tanzania kwenda Afrika Kusini na apple chotara za Afrika Kusini kuingia Tanzania ikoje? Kuna uwiano wowote wa biashara? Sababu ya hizi nchi mbili kuingia kwenye mgogoro huo ni kulazimisha Tanzania kuwa dampo la apple zao. Tanzania ikaona ushenzi.
Kama nchi tusikubali kuwa dampo la mazao ya nchi nyingine kiasi cha kutofuata SPS na food safety requirements ya nchi yetu. Juisi ya Ceres ya Afrika Kusini imepigwa marufuku kwingineko duniani kwa sababu ya health issues lakini hapa Tanzania naona zimejaa kwenye shelves madukani.
 
Hata kama tutakubali soko Litaamu mkuu wangu,
 
Kwa taarifa zilizokuwepo, awali wakulima wa maparachichi huko SA walilalamikia soko lao la zao hilo kuingiliwa na Watanzania na hivyo kushusha bei yake huko kwao.

Yaelekea kwa sasa hali ya hewa si nzuri na hivyo maparachichi yameadimika huko. Kwa hali hiyo basi wameruhusu tuuze haya ya kwetu huko. Huu ndio ukweri!
Ukweli ni kwamba soko la avocado duniani ni kubwa mno hajui tu. Mimi niliagizwa na mfanya biashara mmoja wa Dubai mwaka jana alikuwa anahitaji tani 300 acheni kumpa mtu misifa ya uongo
 
Ukweli ni kwamba soko la avocado duniani ni kubwa mno hajui tu. Mimi niliagizwa na mfanya biashara mmoja wa Dubai mwaka jana alikuwa anahitaji tani 300 acheni kumpa mtu misifa ya uongo
Sifa ya Uongo ipi mkuu?
 
Kumbe miaka kumi tulizuiwa kupeleka parachichi Africa kus
Magufuli aliharibu uhusiano wetu na Nchi nyingi kibiashara, huyu mama kwakweli Mungu ambariki Sana,huko tunakoendea mambo yatakuwa mazuri zaidi
 
Back
Top Bottom