Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais Samia ameahidi kujenga msikiti wa kisasa wenye hadhi ya Rais katika Kitongoji cha Migude, Kijiji cha Milo, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omary wakati alipotembelea msikiti huo ambao hali yake haidhirishi katika kufanya ibada jambo ambalo lilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa Kijiji cha Milo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mara baada ya kuuona msikiti huo Sheikh Alhad Walid Omary amewatoa wasiwasi wakazi wa eneo hilo kwamba msikiti huo utajengwa na Rais Dkt Samia ili wakazi hao waweze kufanya ibada zao katika mazingira yaliyo bora.
Kwa upande wake Sheikh wa Kata ya Vigwaza, Shaban Haroun Mshauri amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan huku wakimuombea kila lenye heri yeye pamoja na wasaidizi wake.
Chanzo cha ahadi ya kujengwa kwa msikiti huo katika kijiji cha Migude kilitokana na video iliyosambaa mitandaoni kupitia kwa Mwandishi wa habari nchini Mbarouk Khan.
Credit: EFM Tanzania
Soma, Pia