Pre GE2025 Rais Samia ameahidi kujenga Msikiti wa Kisasa Vigwaza/Migude wenye hadhi ya Rais. Sheikh Walid ampigia debe urais 2025

Pre GE2025 Rais Samia ameahidi kujenga Msikiti wa Kisasa Vigwaza/Migude wenye hadhi ya Rais. Sheikh Walid ampigia debe urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Una faida gani huoo msikitini kwetu sisi wafrica yaan msikiti ndio tumpigiee kula shekhe una ujinga sana wewe msikitini ni maendeleoo gani
 
Miezi kadhaa nilipita Glasgow, wazanzibari wanavita ya mchango wa msikiti na wenyewe huko.

Awasaidie ndugu zake, vita ni kubwa ya namna ya kuchangishana. Miji yote mikubwa watanzania wana misikiti Glasgow hawana.

Walau atafute dhawabu na yeye kama hakina Lugumi na mafisadi wengine kwa kuwachangia wenye shida.

Ndugu zake wanataka kukatana mapanga kisa mchango wa msikiti.
 
Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu tukiomba.

Mungu tunaomba utende miujiza yako kuinusuru Taifa la Tanzania.
 
sasa hapo Chalinze tu vigwaza hatua chache kutoka Mkoa Dar es salaam watu wanaishi nyumba za udongo.

Kuwepo msikiti wa udongo au kutokuwepo kabisa ni dalili za umasikini wa jamii husika, kazi ya sheikh baadala ya kumuombe Rais kura alipaswa kukemea mamlaka na kuzipigia kelele kuutokomeza umasikini kwa watu wake..

Uliona wapi UAE, Kuwait, Qatar kuna misikiti ya udongo au haipo kabisa Kwa sababu ya watu kuwa masikini?.

Mama tunaomba utujengeee misikiti kila kijiji kila wilaya kila Mkoa, utujengeee makanisa hivyohivyo, utujengee temple za wahindu, mabutha nk.

Tuache cheap politics, shida ya hii nchi ni umasikini wa wananchi ulioletwa na CCM kwa maslahi ya CCM, Ukiutokomeza umasikini kwa Raia hizi nyumba za Ibada watazijenga wananchi wenyewe na kujipatia swawabu.
 
Hiyooo kweli mtu akaswali msikitini wa gorofa halafuu hajala si upuuzii huòoo
 
Nyerere aliwahi kusema ukiona mtu anang'ang'ania kubaki Ikulu huyo mtu ni wa kuogopwa kama ukoma

View: https://youtu.be/PGcgyOd8TFc?si=QOt8kFjpEMSsLqun

Hii sawa hii jamani ?

Katuma Shehe Mkuu wa D'Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa, mtu mzima na heshima zake, kasimama mbele ya camera akasema Rais kantuma ameona msikitiki wenu chakavu, sasa anajenga wa hadhi ya Rais.

Lakini Rais kasema niwaambieni huu ni mwaka wa uchaguzi, mumrudishe madarakani.
---------------

Hii ni nchi ya vyama vingi jamani, Waislamu si wote wnaaipenda CCM na Rais wa CCM kumsikia masikioni mwao akinadiwa wakiwa msikitini. Kutumia mbinu zozote ziwezekanazo kubaki madarakani si sawa!

Ndivyo mnavyoharibu nchi zetu hizi za dunia ya tatu, kwa nini mko hivyo ???
 
Wakati Mama Samia anachangia 150m za ujenzi wa kanisa mbona hamkupiga kelele? Acheni roho mbaya
 
Back
Top Bottom