Rais Samia Amefanikiwa kujenga matumaini katika Mioyo ya Watanzania, Ndio Sababu ya kutamalaki kwa Amani na Utulivu hapa nchini

View attachment 2373035
Watanzania ni masikini sana na bado wanakatwa sana.

Samia anatakiwa kuwa makini sana anyway... bado tunampenda for now.
Nashukuru kwa Kuendelea kumpenda mh Rais wetu mpendwa, Hayo ndio yanayomuumiza mh Rais wetu na kumfanya akose hata muda wa kupumzika, mh Rais anaumizwa na umasikini wa watu wake ndio sababu ya kufanya juhudi kubwa za kutukwamua watanzania kiuchumi na kuondokana na Hali ya umasikini
 
Ajenda sasa hivi ni kutegemea vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi kutangazwa washindi kwa shuruti. Hizo ndio sera zetu majizi ya kura.
Ni ajenda ya CCM kuhakikisha kuwa inajenga uchumi shirikishi wa kugusa maisha ya kila mtanzania, Ndio sababu ya kuona imeamua kuweka juhudi za makusudi katika kilimo ambayo ndio secta iliyo ajiri kundi kubwa la watanzania , hapa Nazani umeona namna serikali ilivyotoa mabillioni ya Ruzuku na kuhakikisha pia soko linakuwa Ni la uhakika kwa mkulima Tangia wakati wa mavuno
 
Nashukuru kwa kukiri na kukubali kuwa bado unayo Imani na mh Rais wetu mpendwa mama Samia, Siyo wewe Bali Ni mamilioni ya watanzania wenye Imani na matumaini makubwa Sana na mh Rais wetu Mama Samia katika kutuongoza na kututumikia
Sina matatizo na Raisi wangu mpendwa Samia, ila atimize zile ahadi kwa vitendo.

Baada ya kuondoka kwa Utawala,wa MABAVU wa Magufuli tunamuona Samia kama Malaika fulani, airudishe Nchi kwenye mrengo wa utawala wa SHERIA naHAKI za Binadamu, DEMOKRASIA na Utawala BORA
Afungue Nchi WAWEKEZAJI waje kwa wingi, ili Vijana hawa wanorandaranda mitaani wapate AJIRA ili wasijingize kwenye vikundi vya kihalifu.

Sasa Mpira uko kwake

Mungu Ibariki TANZANIA.
 
Ni sahihi kabisa mkuu Lucas mwashambwa
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 

Tulia ww chawa wa majizi ya kura.
 
Amani imetamalaki!! Kwako mwenzetu wimbi la ujambazi wakiwemo panya road ndio amani kutamalaki! Kupanda kqwa bidhaa muhimu kama unga na mchele ni amani kutamalaki!! Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!
 
Hao panya Road wanaendelea kusakwa kila eneo walikojificha, Hakuna watakakojificha iwe shimoni au darini watafuatwa na kukamatwa tu
Amani imetamalaki!! Kwako mwenzetu wimbi la ujambazi wakiwemo panya road ndio amani kutamalaki! Kupanda kqwa bidhaa muhimu kama unga na mchele ni amani kutamalaki!! Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!!
 
Mimi mwenyewe Ni mtanzania na naziona nyuso za watanzania zikiwa na furaha na matumaini makubwa pale wanapomzungumzia mh Rais wetu namna anavyowatumikia na kuwajengea matumaini ya kesho iliyo Bora zaidi ya Leo
Soma hapo
 

Njaa ni mbaya
 
Uko sahihi kwa 100%
 
Huyu jamaa anakaa wapi,Masaki?Ana v8? Kama hana vyote apewe anajitahidi sana😀
 
Nilichompendea huyu bwana Mwashambwa haporomoshi matusi.
 
Aman na utulivu wakat ndugu zako Wanakula mlo wa mpakani (haijulikani kama nicha mchana au cha usku)
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima ametahadharisha unafiki wa kisiasa unaoendelea miongoni mwa Watanzania kwa sasa kwa kupenda kusifia kila jambo kuwa utaliua taifa.

Amesema tabia hiyo inaendelea kupata mashiko nchini kutokana na upeo mdogo wa watu kushindwa kujua misingi ya haki za binadamu na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele .

Akizungumza leo Dar es Salaam, Septemba 30, 2022 katika kongamano la viongozi wa dini zote linaloangazia haki za binadamu nchini, kiongozi huyo amesema tabia hiyo iliyojengeka isipokomeshwa ni wazi mahusiano mazuri miongoni mwa Watanzania yanaenda kupotea.

"Unafiki unaharibu nchi, unafiki wa kisiasa uliopo miongoni mwa Watanzania kupenda kusifia viongozi ili tu kujipendekeza wapate vyeo unaenda kuliua Taifa na tatizo hili linaendelea kwa sababu watu hawajui misingi ya haki za binadamu," amesema Padri Kitima

Kiongozi huyo wa kiroho amesema hata kujitoa kwenye mahakama ya haki iliyopo Arusha na kuwahamisha wananchi kutoka Loliondo kwenda Handeni mkoani Tanga ni uvunjivu wa haki za binadamu.

"Kwa sababu nchi imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki za binadamu," amesema

Amesema wao kama viongozi wa dini baada ya kuona tabia hiyo hususan miaka mitano iliyopita, mwaka 2020 walianza kuandika kitabu Cha elimu ya haki za binadamu kwa lengo la kuanza kutoka elimu watu wote.

"Haki za binadamu haziombwi, zinapiganiwa, dini ni kiungo muhimu na tumeona tufanye hivi na tunatarajia kuwafikia viongozi 16,000 nchi nzima na kushuka kwa Watanzania wote," amesema

Chanzo: Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…