Rais Samia Amefanikiwa kujenga matumaini katika Mioyo ya Watanzania, Ndio Sababu ya kutamalaki kwa Amani na Utulivu hapa nchini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Ni ngumu Sana kuongoza watu walio kata tamaa,walio jaa hasira , wanaolia na kuvuja machozi mioyoni mwao, Ni ngumu kuongoza na kusikilizwa na watu wasioona mbele kwa matumaini, Ni ngumu Taifa kutulia na kuwa lenye amani na mshikamano ikiwa limejaa watu ambao hawajuwi hatima ya maisha yao ya kesho, Wala hatima ya watoto wao , Wala namna watakavyoinuka kiuchumi kutoka katika Hali zao,

Rais Samia Amefanikiwa kwa asilimia zote kuwa fanya watanzania kuwa na matumaini ya maisha yao ya kesho, watanzania kwa Sasa mioyo yao imejaa amani na furaha kwa kuwa kila mtu ameguswa na utumishi wa mh Rais wetu, kila mtanzania mwenye kero au shida anamatumaini kuwa kesho itapatiwa suluhisho na atasikilizwa,

masikio ya mama yanamsikiliza kila mtu, macho ya mama yanamtazama kila mtu kwa huruma upendo na uwajibikaji, mikono ya Mama inamgusa kila mtanzania mwenye kuhitaji kushikwa mkono na kuinuliwa, miguu ya mama inamfikia kila mtu mwenye kuhitaji kufikiwa, Sauti ya mama inasikika na kufika kwa watu wote na kwa kila mtu, Tabasamu la mama Ni kwa watu wote, moyo wa mama Ni kwa watanzania wote, akili ya mama Ni kwa kila Raia wa nchi hii, Kauli za mama Ni za haki na upendo kwa mtanzania, Ulimi wa mama Ni wa upendo kwetu sote, maamuzi ya mama Ni kwa maslahi yetu watanzania

Ndio sababu husikii watu wakimlaani mh Rais wetu mpendwa zaidi ya kila mtu kumwombea Afya njema na maisha marefu yenye heri na baraka,husikii watu wakiwa wamekata Tamaa kimaongezi maana wanaona juhudi za mh Rais wetu mpendwa katika kushughulika na kero yoyote inayojitokeza mbele yetu,

Wakulima wanamatumaini na maisha yao kuwa Bora kesho kwa kuwa wanaona juhudi za mh Rais wetu kuwainua kiuchumi kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini iliyopelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni,lakini pia kwa Sasa soko ni la uhakika kwa mkulima Tangia wakati wa mavuno

Ukienda kwa vijana nako unakuta mh Rais wetu mpendwa ametupatia matumaini makubwa Sana ya kesho yetu kuwa njema hasa baada ya kuona akijitahidi kwa nguvu zake zote kutoa ajira kwa kadri Hali ya uchumi inavyoruhusu hivyo kujenga matumaini kwa vijana kufaidika na ukuaji wa uchumi katika nchi yetu

Ukienda kwa wafanyabiashara nao pia wanamatumaini makubwa na mh Rais wetu mpendwa baada ya kuwa mazingira ya kibiashara na kiuwekezaji kuwa yameboreshwa vizuri na kuwa rafiki kwa wafanyabiashara, Biashara zinazidi kufunguliwa kila Kona ya nchi hii na siyo kufungwa kila siku, Jambo linalochochea kuongezeka kwa mapato yatakayosaidia kuwekeza katika huduma za kijamii na uendeshaji wa serikali

Huduma za kijamii pia zimeendelea kujengwa na kusogezwa karibu ya mwananchi na kumpunguzia mtanzania adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma, hivyo kufanya watanzania kutumia muda wao katika shughuli za kiuchumi

Ukienda katika Elimu utakuta mama amefanya makubwa Sana hasa baada ya kutoa hakikisho hata kwa watoto wanaotoka familia maskini kupata Elimu bila shida baada ya uamuzi wake wa kugharamia Ada kwa wanafunzi wote wanaojiunga na Elimu ya msingi Hadi sekondari, hata kwa wa Elimu ya juu nako ameongeza bajeti ili kuwafanya wengi kupata mikopo ya Elimu ya juu

Kwa ufupi Ni kuwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani amefanikiwa kugusa kila eneo na kumgusa kila mtanzania kwa utumishi wake uliotukuka na uliyoleta nuru na matumaini kwa maisha ya watanzania

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Chai toka Mufindi
Kwani wewe hapo ulipo hujafikiwa au hujaona mambo makubwa yaliyofanywa na mh Rais, shule hazipo hapo? Vituo vya Afya havipo hapo? Mwanao analipa Ada shule? Kama wewe Ni mkulima kwamba hujaona namna mbolea zilivyoshuka Bei?
 
Hata kama kajenga matumaini lakini mambo ya maridhiano na mchakato wa katiba mpya yako bery slow.

Ili tumuamini Raisi wetu mpendwa, ayasukume mambo haraka ili uchaguzi mkuu ujao tuwe na free and fear election.
 
JF haitakusaidia , uchawa wa hapa hupati UDC!
 
Hata kama kajenga matumaini lakini mambo ya maridhiano na mchakato wa katiba mpya yako bery slow.

Ili tumuamini Raisi wetu mpendwa, ayasukume mambo haraka ili uchaguzi mkuu ujao tuwe na free and fear election.
Kuna kikosi kazi kilichoundwa ambacho kimekuwa kikikusanya maoni ya wadau juu ya mwaswala mbalimbali ya kuona namna gani mazingira ya kisiasa yanaboreshwa hapa nchini, pia milango ya maridhiano na mazungumzo ipo wazi kwa mh Rais wetu mpendwa , maana sisi sote Ni mashahidi katika Hilo kwa namna mh Rais wetu mpendwa ambavyo amekuwa akifanya juhudi za kujenga umoja wa kitaifa
 
Wewe ni msemaji wa hao watanzania?
Mimi mwenyewe Ni mtanzania na naziona nyuso za watanzania zikiwa na furaha na matumaini makubwa pale wanapomzungumzia mh Rais wetu namna anavyowatumikia na kuwajengea matumaini ya kesho iliyo Bora zaidi ya Leo
 
Kuna kikosi kazi kilichoundwa ambacho kimekuwa kikikusanya maoni ya wadau juu ya mwaswala mbalimbali ya kuona namna gani mazingira ya kisiasa yanaboreshwa hapa nchini, pia milango ya maridhiano na mazungumzo ipo wazi kwa mh Rais wetu mpendwa , maana sisi sote Ni mashahidi katika Hilo kwa namna mh Rais wetu mpendwa ambavyo amekuwa akifanya juhudi za kujenga umoja wa kitaifa
Tunamuunga mkono Raisi wetu mpendwa ila tunajua Makada wengi huko CCM wamezoea vya kunyonga vya HALALI hawaviwezi.
 
CCM Ni chama chenye ajenda na Sera zenye kugusa maisha ya watu Hivyo kinapewa kura kwa upendo na siyo janja janja
 
Ukweli ndio huo kuwa hapa nchini Hakuna chama chenye Sera ajenda na ilani Bora na za muda wote na kugusa maisha ya watu Kama ilivyo CCM
Najua huwezi kusema ukweli kwa kuogopa kifukuzwa kazi.

Ila ukweli unaujua.
 
Back
Top Bottom