Rais Samia amefanya makubwa kuliko Marais wote Tanzania ila vijana wameharibiwa na Mange Kimambi

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Rais Samia ameajiri vijana kuanzia wale wa 2015 mpaka 2025 . Wale ambao Magufuli hakuwa na fedha za kuwalipa kama angewaajiri. Akasingizia uhakiki. Yeye kaajiri waliopaswa kuajiriwa kipindi cha Magufuli na wa kipindi chake.

Watumishi wa umma sasa hivi ukitaka kufanya kubadili taaluma on the spot unabadili na kulipwa mshahara mpya any time tofauti na kipindi cha Magufuli. Ndani ya miaka 5 ya Rais Samia watumishi tumepanda vyeo mara mbili kitu ambacho Magufuli alishindwa kufanya miaka yote ya Urais wake.

Sasa hivi ukitoka Dar es salaam unafika kila mkoa kwa barabara ya rami. Kila mtaa/kijiji Samia kaweka zahanati na zile zahanati za kata sasa zinageuzwa kuwa Health center. Vifaa ambavyo ulikuwa unavukuta hospitali za wilaya sasa utavikuta katani.

Wakulima wa kusini kwa miaka sasa tangu Rais Samia aingie wanapata ruzuku za mbolea na dawa za mikorosho ambazo ni ghari, wengi hawawezi kuzimudu. Nyie mashahidi kipindi cha Magufuli magari ya umma hasa majeshi kama Magereza, polisi, yalikuwa trip garage trip job.

Samia kayaweka Kando yote kaweka magari mapya. Hali ya wafanyabiashara ilikuwa ngumu sana kipindi cha Magufuli. Kila wakati Magufuli aliwaza kuvuna asichopanda. Alikuwa na roho ya umaskini, akiona million mia tu kwenye account ya mtu anatuma vijana. usipotoa chochote kitu anakwapua zote.

Mwishoni kafa , Chato mihela ilijaa store. Katika kipindi hichi cha Samia Kasi ya ujenzi wa makazi bora na maeneo ya huduma Dar es salaam imepanda kwa zaidi ya 400% compared na kipindi cha Magufuli mnayemtukuza.

Watanzania wazawa wengi sasa waneingia kwenye ubilionea baada ya serikali kuachilia tenda mbalimbali kwa kampuni za kizawa. Vijana mnataka nini?

Maelfu ya Watanzania vijana wanapata scholarship za serikali kila mwaka, Ajira za nje hasa falme za Kiarabu sasa ziko rasmi na zenye mikataba mzuri.
Kelele za nini?
Ni udini?
Ujinga?
Mkumbo wa kimtandao?
Mnamtaka mtu wa namna gani?

Mara ooho kauza bandari, kauza KIA, lakini cha ajabu hivyo vitu sasa ndo vinaleta mabilioni kuliko kipindi chochote. Watu walizoea kupitisha mizigo ya mabilioni bandarini huku wakinufaika wao tu.
 
Tuma salami Kwa watu watatu! Kajambe mbele huko
 
Hakika takwimu zinambeba, ndio raisi ameua maelfu ya watanzania ili abaki madarakani, haswa ni kweli takwimu zinambeba ni rais ambaye ameshinda kwa kishindo kikubwa asilimia 98% lakini bado anaomba maridhiano sijui kwa nini,

Hivi Bwawa la Nyerere limefikia wapi, tulitakiwa tuwe tunauza umeme nje , bahati mbaya gharama za umeme ni kubwa mno

Kwa habari ya takwimu kwa maraisi wote waliotangulia hakika yeye zinambeba
 
Rais anapiga vijembe huyo, anasuta hatari
Popote ukiona mtu mwenye hayo mambo mawili, ni mtu asiye na uwezo wa kujenga hoja, logic hakuna
Hata bei ya dola hajui kumbuka suala la bei ya mafuta
ila wasaidizi wake wanampenda maana hajui lolote wao ni kupiga tu watu wanajichotea wajuavyo
 
Huo ndiyo ukweli mkavu ambao wapinzani wake hawaukubali. Lakini subiri 2030 akishatoka, kazi ya Samia kujenga uchumi itaonekana wazi.
 
DP World, kuhamisha wamasai Ngorongoro, kumteua mtoto na mkwe kwenye uwaziri... hizo sababu hazihusiani na Mange.
Hayo mambo ya kuangalia mtoto wake kuwa Wzziri ni wivu wa kipumbavu. Angalia big picture ya anavyojenga uchumi, period.

Hiyo DP WORLD umefuatilia takwimu za mizigo inayoluja nchini na mapato? Au umekaeirishwa tu na ukipofu ww akina Mwabukusi, Kitima na Lissu. Ipime SP WORLD kwa kasi ya kupakua meli na kuindosha mizigo bandarini
 


Usimdanganye mtu. Mambo gani ya ajabu zaidi ya kuona chuki ambayo hakuna mtu mwingine mwenye madaraka kama hayo amepata?
 
Rudia maneno yako mara kumi iwapo unakiamini ukisemacho,ukiwa na akili timamu na bila kushurutishwa na yeyote,ama hali au mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…