CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 6,157
- 5,451
Rais Samia amejenga vyuo vya VETA 94 na amekarabati vyuo 29 Wanafunzi 440,000 wanaendelea na masomo kama msingi wa Dira2050.
Serikali ya Rais Samia imekamilisha ujenzi wa vyuo 29 vya mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimeanza kutoa mafunzo, kuendelea na ujenzi wa vyuo 65 na kukarabati vyuo 29 vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi. Jitihada hizo zimewezesha ongezeko la udahili wa wanafunzi katika vyuo vya elimu ya ufundi kutoka wanafunzi 344,815 mwaka 2020 hadi 440,000 mwaka 2024. Aidha katika kuhakikisha watoto kutoka familia zenye kipato cha chini wanapata fursa sawa ya elimu hii, Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kiongozi msikivu na mwenye kujali imeanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati kwa kozi za kipaumbele.
Hawa vijana 440,000 wakitoka tayari wanaajira zao mkononi, Tukisema mama Samia anatufaa hadi 2030 hiki ndicho kinatuvutia