Rais Samia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya

Huu muda uliobaki kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na Uchaguzi Mkuu wa 2025, napata mashaka kama utatosha kwetu kuipata hiyo Katiba Mpya..

Sijui ni kitu gani kinachochelewesha hili zoezi, linaonekana kwenda taratibu bila sababu za maana licha ya kuwa na hatua nyingi na ngumu mbele ya safari, mfano mpaka leo tunaimbishwa tu Katiba Mpya, lakini wengi bado hatujajua kama itakuwa ni ile Rasimu ya Warioba, au Katiba Pendekezwa ya CCM.

Naamini huu ucheleweshwaji wa makusudi unaoendelea yote ni mipango inafanyika kwa manufaa ya mtawala, ajabu wengi mnaonekana kushangilia hatua hizi zinazokwenda taratibu huku zikisubiri mpaka "michakato" isiyojulikana itakwisha lini ikamilike!.
 
"kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa" Yenye lengo..." lakutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini"

Halafu..."wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya."

Wakati huo huo....
 
Jema
 
HUU NI USHINDI MWINGINE MKUBWA KWA CHADEMA. Najua hamtakubali ila ukweli ndio huu
 
Wakati wa awamu ya 5, huyu Mtungi aliamua kuwa kikaragosi, aliamua kuishi na kutenda kama mtu asiye na utimamu. Sasa hivi tuna uhakika gani atakuwa amerudiwa na akili?
Anafuata tu maelekezo sio taaluma yake Wala utashi wake, wasomi wetu ni shida tupu
 
Kwanini kikosi kazi kilitukwepa wananchi? Ile tume ya Warioba iliwashirikisha wananchi kwa kukutana nao moja kwamoja.
Kwa afya ya siasa bora ni vizuri amuondoe huyo Jaji Mutungi kwana bado anayo masalia ya chuki aliyopandikizwa dhidi ya vyama na viongozi nje ya CCM.
 
Ile ishapitwa na wakati na haitufai kwa wakati huu.
Yale maoni yana miaka 9 kuelekea 10
 
Kimsingi Mutungi hakutakiwa kuhusishwa kwenye mambo haya , huyu ni sehemu iliyohusika kuua Demokrasia , Alipaswa kufukuzwa
Ndio maana sheria hizo zinarekebishwa ili kutoa nafasi katiba iweze fanyika
 
Wakati wa awamu ya 5, huyu Mtungi aliamua kuwa kikaragosi, aliamua kuishi na kutenda kama mtu asiye na utimamu. Sasa hivi tuna uhakika gani atakuwa amerudiwa na akili?
Watanzania wengi ni vinyonga
 
Habari hii akiiona ama kuisikia Tulia Akson atavaa mpk pampasi kuzuia kubwa isichafue nguo maana salama na hatima ya uspika wake ulitegemea sana ubovu wa katiba iliyopo.
Maana wakurugenzi ambao wamekuwa wakitumika kama mihuri wataondolewa, hivyo lile swala la kupita bila kupingwa linakuwa limefutika
 
Katiba haitapatikana mwakani.

Hapo wataitwa vyama vyote watakubaliana kurekebisha sheria ili kuruhusu wote kupata wawakilishi bungeni ili wakajadili katiba ambayo itaanza kazi 2030
 
Endelezeni hoja zenu zisizo na mashiko halafu mgomee mchakato wa katiba mpya Kama mlivyofanya kipindi kile

Wapinzan ndiyo walioharibu mchakato sasa hivi tungekuwa na Katiba mpya walisusa wakatoka nje
 
Kimsingi Mutungi hakutakiwa kuhusishwa kwenye mambo haya , huyu ni sehemu iliyohusika kuua Demokrasia , Alipaswa kufukuzwa
Naunga mkono lakini atabadilika tu. TZ shida huwa iko pale juu whute house hawa wengine huwa ni wadata mkumbo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…