Rais Samia ameonesha ushupavu na umadhubuti katika kuongoza nchi na kukabiliana na changamoto

Ungekuwa mzalendo usingeweka namba hapo, umeweka namba Ili wakurushie hela ya bando huna uzalendo kabisa
Naingia humu jukwaani kwa jasho langu na nguvu yangu mwenyewe ya kununua vocha na siyo kumtegemea mtu na Kama Ni nikumtegemea mtu Basi nisingeweza kuingia kabisa mtu, hata wewe pia naamini unaingia humu kwa gharama zako mwenyewe za vocha
 
Tanzania haijawahi kupata Rais wa hovyo na hopeless kama huyu.Uwezo wake hakustahili hata kuwa kiranja wa shule.Anapaswa kujiuzulu
Uwe na adabu na heshima kwa Rais wetu na kiongozi wetu, huwa naona michango yako mingi Sana humu ambayo inaonyesha kuwa Ni mtu usiye na ustaarabu heshima na busara, Ni mtu unaye onekana kukosa malezi Bora ya wazazi wako, ni mtu unayeonekana Ni Kama hukulelewa na kukuzwa na wazazi wako kimaadili, ndio sababu umekosa maadili na heshima kwa kila mtu, ndio sababu ya kuonekana kichwani hupo vizuri na una matatizo kichwani yanayohitaji matibabu, usimzoee Rais kumshambulia kwa maneno yako yaliyokosa adabu, Rais Ni Taasisi inayolindwa kwa nguvu zote, huwezi ukaichafua na kuidhalilisha Kama ufanyavyo, jifunze kukosoa kwa heshima na staha, jifunze kuheshimu mawazo ya wengine,jifunze kuwa na kifua na mrudie muumba wako aliye kuumba
 

Watu hawataki magari wanataka maji, hiyo kuonyesha magari ni kiki za kijinga.

Mahitaji ya umeme kuongezeka ilikuwa ni jambo la kustukiza kiasi kwamba hamjui nini kilitakiwa? Wakati wa JK porojo ilikuwa ni kuzalisha umeme wa gas 5,000mg, leo hata 1,000mg za gas hakuna. Cha kushangaza tumeachana na umeme wa gas tumerukia umeme wa maji wakati tunalalamika matatizo ya tabia nchi. Au mtazindua tena magari ya kuchimba maji kulisha hilo bwawa?
 
Huu mgao wa umeme na maji ndio ushupavu. Hivi chawa hamuoni aibu kwenye mapambio yenu?
Sasa hapo unanishangaza unaposena watu hawataki magari wanataka maji, kwa hiyo unafikiri hayo maji yanakuja kwa kuletwa na bodaboda Tindo? Hayo magari ndio yanayokwenda kuchimba visima virefu na kumaliza tatizo la maji
 
Njaa tu hizi huna lolote.

Samia kafanya nini kuyafanya maisha yako yawe mazuri?

Zaidi kawafanya machinga wawe panya road.
 
Haya tumekusikia kijana mzalendo.

Sisi tunaokosoa hatuthubutu kuweka namba zetu kwa sababa mfumo uliopo unawalinda wapiga korasi, chawa fulani fulani hivi.

Na mngegundua App inayoweza mawazo ya watu mngewekeza sana kwenye ununuzi wa silaha za kuwaangamiza maadui wa ndani
 
Naingia humu jukwaani kwa jasho langu na nguvu yangu mwenyewe ya kununua vocha na siyo kumtegemea mtu na Kama Ni nikumtegemea mtu Basi nisingeweza kuingia kabisa mtu, hata wewe pia naamini unaingia humu kwa gharama zako mwenyewe za vocha
Ukitoa mabandiko kwa nini uweke namba ya simu?
 

Ulianza nyuzi zako kwa kuiponda CHADEMA ukaona hailipi, ukahamia kuisifu CCM ukaona hailipi Sasa hivi umehamia kwenye kumsifia Rais Samiah hata kwenye uongo. Na Cha kuchekesha baada ya kuona hakuna yupo interested na wewe umeamua kuweka namba ya simu.
 
Njaa tu hizi huna lolote.

Samia kafanya nini kuyafanya maisha yako yawe mazuri?

Zaidi kawafanya machinga wawe panya road.
Mimi Kama mkulima na wakulima wengine tunamshukuru mh Rais kwa kutupatia mbolea za Ruzuku ambapo serikali yake ikitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, lakini pia Tumeona namna huduma za kijana zilivyo boreshwa na kusogezwa karibu yetu, Tumeona Elimu ikitolewa bure Hadi kidato Cha sita na mengine mengi tu
 
Naingia humu jukwaani kwa jasho langu na nguvu yangu mwenyewe ya kununua vocha na siyo kumtegemea mtu na Kama Ni nikumtegemea mtu Basi nisingeweza kuingia kabisa mtu, hata wewe pia naamini unaingia humu kwa gharama zako mwenyewe za vocha

Mimi tangu nikuone unaweka namba ya simu nikajua ni msaka fursa baada ya kushindwa kujiajiri. Mind you kuweka namba namba ya Siri umekubali kujiexpose na incase ukaongea Jambo sensitive kwa seriklai, utajua hujui. Maana kwa Sasa umejipa kazi ya msemaji wa mama Samiah , wakati kipo kitengo kwa kazi hiyo. Kuwa makini.
 
Hili nalo kalitazameni.
 
Namba ya simu inaondoa uhalali wa ulichokiandika. Ni Kama unaandika watu fulani wakuone wakutumie kiasi kidogo Cha pesa.
Hapana hii siyo barua ya maombi ya hela au sms ya kuomba hela, Ni Kama mwandishi anavyoweza akaweka habari gazetini halafu mwishoni kunakuwa na namba. Je waandishi huweka namba kwa ajili ya kuomba hela?
 
Mimi Tayari nilishajiajiri katika kilimo, nguvu zangu ndio mtaji wangu, jembe langu begani ndio kalamu yangu,shamb langu ndio daftari langu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…