Rais Samia amerithi nchi iliyofilisika kifedha na kiuchumi

hii propaganda haijakaa vizuri bwashee.
unaweza kuwa na ukweli lakini tumia akili ueleza ukweli wako.

Baada ya MAGUFULI kulala usingizi wa milele, yameibuka mengi.TOZO lukuki.kwamba hali ya uchumi iko mbaya ndiyo maana SGR na BWAWA la umeme wa NYERERE haviwezi kujengwa ??? hahahhaaa.unafiki bana.tunajua kuna wafanyabiasha wenye maloli hawataki SGR ijengwe ,unafikiri hatujui? tunajua kuna makapuni ya kufua umeme kwa njia ya upepo unajua hatujui?acha kumharibia mama ,na kama ni TISS wamekutuma kupima upepo wambia mmenidanganya aisee,tena mnamharibia mama. uchumi umeharibika huku mishahara ikiongezwa ,posho zikiongezwa,perdiem zikiongezwa,safari za kila siku zikipamba moto nk . Yani wewe mwenye thread hii nikikwita mwehu nafikiri nitakuwa sijakosea .

sisi wananchi siyo kwamba hatutaki kulipo kodi na tozo mbali mbali.kama kodi na tozo mbalimbali zinaenda kujenga SGR,Bwawa la umeme,fyeover,vivuko ,kununua dawa za hospitali,kujenga vituo vya afya ,kuboresha elimu nk mbona hatuna shida kuliko kutuambia upumbafu ati hayati Magufuli aliharibu uchumi?? Kama umetumwa na CCM kwa hakika tumerudi nyuma kwa kasi ya ajabu .unakumbuka 2014 -2015 ukivaa kofia au nguo ya CCM ulivyoonekana jangili fulani? 2025 siyo mbali
 
Pamoja na kwamba rais aliyepita Kuna mambo aliharibu , isiwe ndiyo excuse ya mambo jinsi yanavyoenda mama,, kusema ule ukweli mchungu ni kwamba rais amekosa watu ambao ni think tank ambao wangemsaidia kuufufua uchumi unaoelekea shimoni, yani hauwezi kukuza uchumi kwa kukwangua pesa za walalahoi na kuzilundika hazina na kwenye ma account ya serikali kwakua haitaongeza thamani, Sasa waziri wa fedha analeta double taxation kwa watu ambao vipato vyao havijaongezeka!!! Zaidi zaidi anasababisha purchasing power ya raia wake ipungue, then what next, ?hiyo Wizara ampe mtu ambaye atakua na maono thabiti Ila siyo huyu anayekuja na solution ya kwamba kama mtu hataki tozo ahamie Burundi, what the Joke?
 
Wewe ndo mpumbavu kwa Nini usidadavue kwa hoja Kama mleta mada? Unakuja na vijimaneno viwili vitatu halafu unatukana.
Tumia akili boya wewe huyo mnayemsema kakopa sana ni shilingi ngapi na ndani ya muda gani na kumbuka alikuwa anafanya project gani na ngapi,compare na huyu shangazi yako amekopa 10 T ndani ya mwaka mmoja na bado anaendelea kutuumiza wananchi na vitozo vya kithenge na hakuna project yoyote aliyoanzisha zaidi ya matundu ya choo achana na hela za covid,mchukieni magufuli, lakini mazuri yake ni mengi kuliko hayo mabaya mnayo yasambaza kwa nguvu zenu zote.....pamoja na hayo yote watanzania hapo na nyie mafisi wenye uchu na mali zao.
 
Yaani sitasahau sekta ya kilimo alivyoivuruga bwana yule! Unatumia 2.5m kwa kilimo unakuja kuuza less than 1m dah sitasahau..pembejeo juu, mbolea juu halafu unapangiwa Bei ya kuuza! Halafu wale wa ntwara koro show iliishia wapi?
Wewe ni mjinga mpumbavu na unajifunza uchawa kutoka kwa machawa wenzako, unasema pembejeo kipindi cha magufuli bei ilikuwa juu shilingi 47000 mpaka 52000 kwa 50 kg na vocha kama zote kwa wakulima utalinganisha na sasa hivi mfuko wa kg 50 unauzwa 140000 mara tatu ya bei kwa jpm ,na kibaya zaidi pembejeo zimepanda kabla ata rusia na ukraine hawajaanza chokochoko na kuanza kupigana ,
Usiongee vitu kama vile watanzania walikuwa wameenda burundi wakati ule na wamerudi sasa nchini mwao.
 
Akikujibu niite mbwaa nimekaa pale.
 
Unajilisha upepo siyo? Hizo project za mfukoni ndo zimetufikisha hapa! Unajua biashara ngapi aliua huyo mtu wenu? Sekta binafsi zilikuwa hoi bin tete...ikaja kubainika mashirika ya umma yalijiendesha kwa hasara halafu bado yalitoa gawio kwa bwana yule. Ila sisi watanzania aliyeturoga alaaniwe kabisa alichofanikiwa yeye ni kutushikisha adabu na kutuziba midomo. Huwezi ukaua biashara za watu kwa kuwabambikizia mikodi ya ajabu ajabu...hivi huwa unasoma hata ripoti za CAG wewe?
 
Na wewe pia ni wa Chato
 
Wewe lofa Mimi nimeingia field siyo kilimo Cha mtandaoni unajua kiazi kimeuzwa Bei gani 2019? Au kisa unakula chipsi kavu za buku jero hapo mzizima unahisi umeyapatia maisha? Nenda kaone vilio vya wakulima walivyolia huko mikoani ndo uje uharishe hapa. Anyway mungu fundi alituamulia
 
umepewa buku ya bando unakuja kuharaaa mtandaoni!acha unafki na maisha huna.
Uzuri ni kwamba wapiga kura hawapo jf Wala Twitter ingekuwa hivyo sawa. Ila tuliopo field ndo tunajua. Sasa hivi tuna amani na hata transparency ipo hivi bwana yule alivyokuwa kamanda kwelikweli ...hata angeanzisha hizi tozo unadhani Kuna nyumbu ingethubutu kuhoji?
 
Hivi wewe ulikuwa wapi kipindi MAGUFULI anatawala? Mbona mnapenda mambo ya kijinga. Nani asie jua kama FASHISTI MAGUFULI alikuwa ashauriki samaia angefanya Nini? Yule Jamaa alikuwa Zaid ya shetani....
 
Nitajie biashara tano alizoua jpm namimi nikutajie project kumi ambazo zilikuwa zinaendelea vizuri pasipo mwananchi kubebeshwa zigo la tozo wala kuwepo na mfumuko wa bei .
 
Ndo maana nasisitiza wewe ni mpumbavu pro na kibaya zaidi uchawa hauwezi ndo unajifunza baby class hivyo viazi unavyo vizungumzia vililimwa mbolea iko na bei gani? Je unajua supply ya viazi mwaka huo ilikuwa ni kubwa kiasi gani mpaka tukawa tunazuia viazi visiingie kutoka kenya,wenzako wanalima kwa ramani weee unalima kwa kujidanganya kijiweni fala wewe
 
Nitajie biashara tano alizoua jpm namimi nikutajie project kumi ambazo zilikuwa zinaendelea vizuri pasipo mwananchi kubebeshwa zigo la tozo wala kuwepo na mfumuko wa bei .
1. Efatha
2.Covenant Bank,
3. KILIMANJARO COMMUNITY BANK
4. Njombe Community Bank,
5. Kagera Farmers’ Cooperative Bank, and
6. Meru Community Bank
7. Federal Bank of the Middle East
8. Tanzania Investment Bank (TIB)
9. China Commercial Bank Limited
10. Bank M
11. Twiga Bank
12. Mbinga Community Bank

Hizo ni bank tuu ngoja nifanye miamala nilipe tozo tujenge nchi ntarudi na sekta zingine
 
Brother hiyo biashara sikuianza huo mwaka.. inflation ilikuwepo Ila siyo ya kiasi kile. Kwani hao Kenya walikuwa hawalimi toka zamani? Haya na korosho, mbaazi, kahawa nk. Nani aliua? Kuna mengi JPM alifanya Ila kwenye sekta ya kilimo na elimu alifeli vibaya...kipindi chake ndo tuliona 60% ya wanafunzi shule fulani wanapata div one 7pts halafu ndo kipindi chuo kikuu wamedisco Sana.
 
Unaandika huku unatetemeka.
Yah natetemeka kwa hasira. Ila tuacheni utani lipa tozo zote ishakuwa Sheria huna namna, mlimpigia makofi Sana marehemu alipopora uchaguzi Sasa hakuna wa kuwatetea tunalipa pamoja...hutaki chukua ushauri wa Mwigulu hamia hata Burundi tu 😀😀ukawatumikie hata waasi
 
 
Kwamtu aliye kuwa anamfaham vizuri jpm si Hilo si swali la kuuliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…