Rais Samia amesema anarejesha mahusiano na nchi za Ulaya. Je, kukopa ndio njia bora ya kufanya hivyo?

Tatizo ni kuwa fedha wanazotoa ni kwa miradi ambayo sio endelevu.

Ila inakufanya uwe tegemezi kwao mtego uko hapo.

Tujutahidi ama tukope tufanye miradi yenye manufaa kwetu au tutumie vyanzo mbadala kuongeza fedha za ndani.
 
Ombaomba hawezi kuwa na akili sababu anao uhakika
 
Unataka tuwakaushie wazungu wakati hao ndio watalii wanaoingiza pesa katika mbuga zetu za kaskazini?.

Nchi yetu ni tajiri wa rasilimali lakini kiuhalisia bado ni maskini. Kila rais anayo haiba yake yenye kutofautiana na ya mwenzake.

JPM aliamua kuwafungia vioo wazungu kwani mambo ya diplomasia hakuyaweza na hakuwa na akili za kibiashara.

Jaribu kufuatilia ni biashara ngapi zinazoanzishwa Tanzania kuanzia mwaka jana kati ya wazalendo na wazungu ndio utaelewa haiba ya SSH kimataifa ipo vipi.
 
CCM mbele kwa mbele.....
 
Kwani wewe unawazaje.
 
Mwanaume ameumbwa kutafuta,mwanamke ameumbwa kusaidiwa, na sio kutafuta.hiyo ndio tofauti ya rais mwanaume na rais mwanamke. Vyanzo vingi vya ndani havikusanyi tens,tutaenda mwendo huo huo usishangae
 
sante kwa bandiko / uzi wako mzuri , kuna watu mpo special majukwaani kwa kutoa ushauri wenye tija

wapo watu special jukwaani kwa kuwapinga wale wenye mawazo chanya juu ya serikali / nchi yao

hayo mambo unayoyazungumzia upo uzi nimeuweka mimi kuhusu serikali kukopa kupita kias cha kuskitisha nimeonekana mjinga sana japo wapo watu walioafika mawazo yangu

kimsingi mikopo sio jambo la kulifurahia sana kwaiyo tunapoishauri serikali juu ya jambo hili ni vyema ikajitathmin kwanza
 
Onaga aibu basi kuwasifia hao washenz wanaopata maendeleo kwa kuiba resources za nchi yako kupitia mikataba mibovu.

Weng mnaomlaumu magu ninyi ni bendera fuata upepo, hiv unaweza orodhesha hayo aliyowajaza watu ambayo hayana ukweli?

Ni kweli kukopa kwa mataifa yaliyokuweka utumwani si vzr, lkn kuna muda hutakiwi kuchagua jembe ili ulime, as long as ni mikopo na utairejesha, so ni pesa yako, biashara haibagui toafuttza kiitikadi.

Kujitambua na kujua umuhimu wa kujitegemea ni njia bora ya kufikia malengo, hata baba wa taifa alifundisha hayo mambo lkn pia alikopa na kupata misaada.

Acheni chuki za kipumbavu, si ajabu huyo mzee ktk ukoo wako ni wew mpumbavu mmoja unayeona mabaya yake tu.
 
Wazungu hawakuacha kuja kutalii kipindi cha Magufuli, Wakati huo bishara ilikuwa nzuri tu kwani sisi tulikua moja wapo ya nchi chache ambazo hatukua na lock down.

Aidha biashara ya nje ya nchi ilikua sana kipindi chake.

Mwaka 2018 tulifanya export nyingi na kupata faida tofauti na sasa ambapo inasemekana nchi imefunguliwa.

Kinachosemekana mahusiano mabaya ni kukataa masharti yao ya kipuuzi kwenye mikopo na misaada yao.

Masharti ya kinyonyaji na kitumwa.
 
Kwani wewe unawazaje.
Tunaweza kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya bila kuwakopa kopa na kuwaomba omba.

Yaani kati ile level ya partners katika biashara na sio level ya mfalme na mtwana.
 
Masharti kuwa ya kitumwa ni tangu miaka ile ya Structural Adjustment Programme SAP, haijaanza leo wala jana. Tuwe wapole tu ndio utamaduni unaoiendesha hii dunia.
 
Tunaweza kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya bila kuwakopa kopa na kuwaomba omba.

Yaani kati ile level ya partners katika biashara na sio level ya mfalme na mtwana.
Mmesahau kama mlisema mnaweza kusimama Kwa miguu yenu wenyewe bila kumtegemea beberu🤔.Au unajitoa akili na kutuaminisha Leo tunawahitaji mabeberu bila kukopa, ukiwa mnaa kumbuka na kuficha sura😃
 
Tatizo ni kuwa fedha wanazotoa ni kwa miradi ambayo sio endelevu.

Ila inakufanya uwe tegemezi kwao mtego uko hapo.

Tujutahidi ama tukope tufanye miradi yenye manufaa kwetu au tutumie vyanzo mbadala kuongeza fedha za ndani.
Haya mambo ya wachumi pasua kichwa. Nakopa halafu napangiwa tumieje mkopo huo. Hivi hapo nimekopa kweli ama natumikishwa...yaani nimefunguliwa genge na bosi jioni mahesabu? Wachumi nisaidieni jamani nielewe mambo haya.
 
Masharti kuwa ya kitumwa ni tangu miaka ile ya Structural Adjustment Programme SAP, haijaanza leo wala jana. Tuwe wapole tu ndio utamaduni unaoiendesha hii dunia.
Kuwa wapole ni makosa na kukubali kuendelea kuwa katika hali hiyo ni makosa zaidi.

Kumbuka wenzetu wote tuliokuwa nao sawa miaka 60 iliyopita leo wanatupa misaada.

Kwanini sisi tusiachane na hii kasumba ya kukubali kwamba hizi ndio kanuni za kidunia??

Hizo ni propaganda tu za kutufanya tuogope kuachana na utumwa wao.
 
Kwani mahusiano yalikuwa yamekufa? Hii ni lugha mbaya ya kujikweza tu; Tanzania haijawahi kuvunja mahusiano yoyte na nchi za ulaya. Kuna nchi hazikufurahia maamuzi ya serikali ya Tanzania lakini siyo kuwa mahusiano yalikuwa yamevunjika. Ni afadhali aseme kuwa amezifurahisha nchi za ulaya lakini siyo kuwa karudisha mahusiano na nchi za ulaya.
 
Haya mambo ya wachumi pasua kichwa. Nakopa halafu napangiwa tumieje mkopo huo. Hivi hapo nimekopa kweli ama natumikishwa...yaani nimefunguliwa genge na bosi jioni mahesabu? Wachumi nisaidieni jamani nielewe mambo haya.
Logic ni kwamba mtu unakopa kulingana na business plan yako ila kilichopo hapa ni kuwa anayekupa fedha anakuchagulia cha kufanya na namna ya kurejesha.

Halafu usipokopa unageuka adui.
 
Ulichosema ni sahihi mkuu,
 
Utumwa unaanzia kwetu wenyewe, kukataa kufanya kazi kwa bidii, kukosa nidhamu kuanzia utotoni.

Wenzetu wanafundishwa kujinyima tangia utotoni, sisi tunaachiana tu, tunaishi tu.

Kuomba omba kuna malengo yake maalum, ni kufanikisha miradi na kuendesha uchumi wa nchi.

Kusema sisi ni matajiri wakati hatuna cha kwetu tulichovumbua, ni sawa na kupaka rangi upepo.
 
Umesema kwamba wenzetu wanafundishwa tangu utotoni well magufuli kusema kwamba sisi ni matajiri alikuwa anasema ukweli ukweli ambao ungewasaidia watoto wa sasa kutambua potential ambayo nchi hii inayo na hivyo kuitumia vyema.

Magufuli alihimiza nidhamu na uchapa kazi (falsafa ya hapa kazi tu) hili limesaidia wengi waliopo sasa na wanaokuja kushika nafasi kwa baadae.

Kuwa omba omba ni laana.

Tuondoe hii laana ya mikopo na misaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…