Rais Samia amesema anarejesha mahusiano na nchi za Ulaya. Je, kukopa ndio njia bora ya kufanya hivyo?

Ulaya bila kukopesha inapotea mazima! Kukopesha ni moja ya shamba lao kubwa la kuna. Hata kama hutaki watakubembeleza wee ama watakusulubu wuu mpaka uingine kwenye shamba lao "uvunwe".
===
Tukiwa wajanja tunaweza kuingia kwenye shamba lao lakini tukagoma kuvunwa.
Tatizo ni kuwa fedha wanazotoa ni kwa miradi ambayo sio endelevu.

Ila inakufanya uwe tegemezi kwao mtego uko hapo.

Tujutahidi ama tukope tufanye miradi yenye manufaa kwetu au tutumie vyanzo mbadala kuongeza fedha za ndani.
 
Ombaomba hawezi kuwa na akili sababu anao uhakika
 
Sio kweli kwamba fedha zote zinazokopwa ni kwa ajili ya miradi iliyoachwa Magufuli.

Fedha za Uviko zilikwenda kwenye madarasa na vyoo hazikwenda SGR wala Stiglers.

Fedha toka world bank - usalama wa Ardhi.

Fedha za Ufaransa - Miradi Tanga na Pemba.

Hivyo ukiangalia kwa haraka utaona kwamba mikopo imechukua sehemu kubwa sana ya mahusiano yetu na Ulaya jambo ambalo linashitua.
Unataka tuwakaushie wazungu wakati hao ndio watalii wanaoingiza pesa katika mbuga zetu za kaskazini?.

Nchi yetu ni tajiri wa rasilimali lakini kiuhalisia bado ni maskini. Kila rais anayo haiba yake yenye kutofautiana na ya mwenzake.

JPM aliamua kuwafungia vioo wazungu kwani mambo ya diplomasia hakuyaweza na hakuwa na akili za kibiashara.

Jaribu kufuatilia ni biashara ngapi zinazoanzishwa Tanzania kuanzia mwaka jana kati ya wazalendo na wazungu ndio utaelewa haiba ya SSH kimataifa ipo vipi.
 
Mh. Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha.

Observation yangu ndogo ya matendo yatokanayo na jitihada hizo za kurejesha mahusiano na nchi za ulaya yanaonesha kwamba kasi ya ukopaji na misaada toka nchi za Ulaya na taasisi za kifedha imeongezeka.

Rais mwenyewe anakiri kwamba kuna fedha zilikuwa withheld ila kuna possibility kubwa sasa zikaachiwa.

Kauli ya Rais Magufuli mara kwa mara ilikua kukataa mikopo na misaada yenye masharti magumu kwa Taifa.

Ushahidi wa kauli za Magufuli za kukataa kwa mikopo awamu ya tano ni kwa kauli ya Rais hivi majuzi kuwa kuna fedha zilizuiwa.

Kwakua sasa misaada na mikopo imeanza kumiminika kwa wingi ni wazi kwamba uongozi wa awamu hii unakubaliana na masharti ya mikopo hiyo.

Swala hapa la kujiuliza ni je masharti hayo yana madhara gani kwa Taifa letu.

Na kama yana faida basi tuambiwe faida hizo ni zipi?

Ninachoomba tu kwa Serikali ni kuwa makini wakati inapokubaliana na masharti hayo ya mikopo na misaada isiwe tunafanya tu kwa lengo la kuwafurahisha nchi za ulaya wakati kwa uhalisia tunaoumia ni sisi na vizazi vyetu huku wao na vizazi vyao wakinufaika.

Pia ningependa kujua, je ni lazima tukope na kupokea misaada toka nchi za Ulaya ili mahusiano yetu na wao yawe mazuri.

Kwani hatuwezi kuwa na mahusiano nao mazuri bila kukopa na kupewa misaada.

Nasema hivi kwani inaonekana kwamba kukopa na kuomba misaada ndio njia pekee ya kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya.

Nachelea kusema kwamba Nchi za Ulaya zinanufaika mno na mikopo na misaada wanayotupa maana wasingepata hasira kwa sisi kukataa mikopo na misaada yao.

Tuwe makini.
CCM mbele kwa mbele.....
 
Kwani wewe unawazaje.
 
Mwanaume ameumbwa kutafuta,mwanamke ameumbwa kusaidiwa, na sio kutafuta.hiyo ndio tofauti ya rais mwanaume na rais mwanamke. Vyanzo vingi vya ndani havikusanyi tens,tutaenda mwendo huo huo usishangae
 
Mh. Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha.

Observation yangu ndogo ya matendo yatokanayo na jitihada hizo za kurejesha mahusiano na nchi za ulaya yanaonesha kwamba kasi ya ukopaji na misaada toka nchi za Ulaya na taasisi za kifedha imeongezeka.

Rais mwenyewe anakiri kwamba kuna fedha zilikuwa withheld ila kuna possibility kubwa sasa zikaachiwa.

Kauli ya Rais Magufuli mara kwa mara ilikua kukataa mikopo na misaada yenye masharti magumu kwa Taifa.

Ushahidi wa kauli za Magufuli za kukataa kwa mikopo awamu ya tano ni kwa kauli ya Rais hivi majuzi kuwa kuna fedha zilizuiwa.

Kwakua sasa misaada na mikopo imeanza kumiminika kwa wingi ni wazi kwamba uongozi wa awamu hii unakubaliana na masharti ya mikopo hiyo.

Swala hapa la kujiuliza ni je masharti hayo yana madhara gani kwa Taifa letu.

Na kama yana faida basi tuambiwe faida hizo ni zipi?

Ninachoomba tu kwa Serikali ni kuwa makini wakati inapokubaliana na masharti hayo ya mikopo na misaada isiwe tunafanya tu kwa lengo la kuwafurahisha nchi za ulaya wakati kwa uhalisia tunaoumia ni sisi na vizazi vyetu huku wao na vizazi vyao wakinufaika.

Pia ningependa kujua, je ni lazima tukope na kupokea misaada toka nchi za Ulaya ili mahusiano yetu na wao yawe mazuri.

Kwani hatuwezi kuwa na mahusiano nao mazuri bila kukopa na kupewa misaada.

Nasema hivi kwani inaonekana kwamba kukopa na kuomba misaada ndio njia pekee ya kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya.

Nachelea kusema kwamba Nchi za Ulaya zinanufaika mno na mikopo na misaada wanayotupa maana wasingepata hasira kwa sisi kukataa mikopo na misaada yao.

Tuwe makini.
sante kwa bandiko / uzi wako mzuri , kuna watu mpo special majukwaani kwa kutoa ushauri wenye tija

wapo watu special jukwaani kwa kuwapinga wale wenye mawazo chanya juu ya serikali / nchi yao

hayo mambo unayoyazungumzia upo uzi nimeuweka mimi kuhusu serikali kukopa kupita kias cha kuskitisha nimeonekana mjinga sana japo wapo watu walioafika mawazo yangu

kimsingi mikopo sio jambo la kulifurahia sana kwaiyo tunapoishauri serikali juu ya jambo hili ni vyema ikajitathmin kwanza
 
Kauli za JPM zilikuwa hazifanani na matendo yake mbali na majukwaa ya siasa. Aliwajaza watu kiburi cha kujitegemea wakati kiuhalisia tupo mbali sana na uwezo wa kushindana kiuchumi na mataifa ya Ulaya.

Mzungu anayo know how (maarifa) na ndio kitu ambacho kinampa umaarufu mchina kwa sasa, utundu na ubunifu wa hali ya juu.

Huwezi kushinda na mzungu mwenye taasisi zote za pesa, utakuwa unajisumbua bure tu. Nyerere aliwawekea kiburi na haikumsaidia chochote ndio akaingia Mwinyi madarakani akawapigia magoti wazungu.

Huu ni utamaduni wa kidunia, huwezi kuwavimbia waliotutawala halafu ukawa na uchumi endelevu
Onaga aibu basi kuwasifia hao washenz wanaopata maendeleo kwa kuiba resources za nchi yako kupitia mikataba mibovu.

Weng mnaomlaumu magu ninyi ni bendera fuata upepo, hiv unaweza orodhesha hayo aliyowajaza watu ambayo hayana ukweli?

Ni kweli kukopa kwa mataifa yaliyokuweka utumwani si vzr, lkn kuna muda hutakiwi kuchagua jembe ili ulime, as long as ni mikopo na utairejesha, so ni pesa yako, biashara haibagui toafuttza kiitikadi.

Kujitambua na kujua umuhimu wa kujitegemea ni njia bora ya kufikia malengo, hata baba wa taifa alifundisha hayo mambo lkn pia alikopa na kupata misaada.

Acheni chuki za kipumbavu, si ajabu huyo mzee ktk ukoo wako ni wew mpumbavu mmoja unayeona mabaya yake tu.
 
Unataka tuwakaushie wazungu wakati hao ndio watalii wanaoingiza pesa katika mbuga zetu za kaskazini?.

Nchi yetu ni tajiri wa rasilimali lakini kiuhalisia bado ni maskini. Kila rais anayo haiba yake yenye kutofautiana na ya mwenzake.

JPM aliamua kuwafungia vioo wazungu kwani mambo ya diplomasia hakuyaweza na hakuwa na akili za kibiashara.

Jaribu kufuatilia ni biashara ngapi zinazoanzishwa Tanzania kuanzia mwaka jana kati ya wazalendo na wazungu ndio utaelewa haiba ya SSH kimataifa ipo vipi.
Wazungu hawakuacha kuja kutalii kipindi cha Magufuli, Wakati huo bishara ilikuwa nzuri tu kwani sisi tulikua moja wapo ya nchi chache ambazo hatukua na lock down.

Aidha biashara ya nje ya nchi ilikua sana kipindi chake.

Mwaka 2018 tulifanya export nyingi na kupata faida tofauti na sasa ambapo inasemekana nchi imefunguliwa.

Kinachosemekana mahusiano mabaya ni kukataa masharti yao ya kipuuzi kwenye mikopo na misaada yao.

Masharti ya kinyonyaji na kitumwa.
 
Kwani wewe unawazaje.
Tunaweza kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya bila kuwakopa kopa na kuwaomba omba.

Yaani kati ile level ya partners katika biashara na sio level ya mfalme na mtwana.
 
Wazungu hawakuacha kuja kutalii kipindi cha Magufuli, Wakati huo bishara ilikuwa nzuri tu kwani sisi tulikua moja wapo ya nchi chache ambazo hatukua na lock down.

Kinachosemekana mahusiano mabaya ni kukataa masharti yao ya kipuuzi kwenye mikopo na misaada yao.

Masharti ya kinyonyaji na kitumwa.
Masharti kuwa ya kitumwa ni tangu miaka ile ya Structural Adjustment Programme SAP, haijaanza leo wala jana. Tuwe wapole tu ndio utamaduni unaoiendesha hii dunia.
 
Tunaweza kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya bila kuwakopa kopa na kuwaomba omba.

Yaani kati ile level ya partners katika biashara na sio level ya mfalme na mtwana.
Mmesahau kama mlisema mnaweza kusimama Kwa miguu yenu wenyewe bila kumtegemea beberu🤔.Au unajitoa akili na kutuaminisha Leo tunawahitaji mabeberu bila kukopa, ukiwa mnaa kumbuka na kuficha sura😃
 
Tatizo ni kuwa fedha wanazotoa ni kwa miradi ambayo sio endelevu.

Ila inakufanya uwe tegemezi kwao mtego uko hapo.

Tujutahidi ama tukope tufanye miradi yenye manufaa kwetu au tutumie vyanzo mbadala kuongeza fedha za ndani.
Haya mambo ya wachumi pasua kichwa. Nakopa halafu napangiwa tumieje mkopo huo. Hivi hapo nimekopa kweli ama natumikishwa...yaani nimefunguliwa genge na bosi jioni mahesabu? Wachumi nisaidieni jamani nielewe mambo haya.
 
Masharti kuwa ya kitumwa ni tangu miaka ile ya Structural Adjustment Programme SAP, haijaanza leo wala jana. Tuwe wapole tu ndio utamaduni unaoiendesha hii dunia.
Kuwa wapole ni makosa na kukubali kuendelea kuwa katika hali hiyo ni makosa zaidi.

Kumbuka wenzetu wote tuliokuwa nao sawa miaka 60 iliyopita leo wanatupa misaada.

Kwanini sisi tusiachane na hii kasumba ya kukubali kwamba hizi ndio kanuni za kidunia??

Hizo ni propaganda tu za kutufanya tuogope kuachana na utumwa wao.
 
Mh. Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha.

Observation yangu ndogo ya matendo yatokanayo na jitihada hizo za kurejesha mahusiano na nchi za ulaya yanaonesha kwamba kasi ya ukopaji na misaada toka nchi za Ulaya na taasisi za kifedha imeongezeka.

Rais mwenyewe anakiri kwamba kuna fedha zilikuwa withheld ila kuna possibility kubwa sasa zikaachiwa.

Kauli ya Rais Magufuli mara kwa mara ilikua kukataa mikopo na misaada yenye masharti magumu kwa Taifa.

Ushahidi wa kauli za Magufuli za kukataa kwa mikopo awamu ya tano ni kwa kauli ya Rais hivi majuzi kuwa kuna fedha zilizuiwa.

Kwakua sasa misaada na mikopo imeanza kumiminika kwa wingi ni wazi kwamba uongozi wa awamu hii unakubaliana na masharti ya mikopo hiyo.

Swala hapa la kujiuliza ni je masharti hayo yana madhara gani kwa Taifa letu.

Na kama yana faida basi tuambiwe faida hizo ni zipi?

Ninachoomba tu kwa Serikali ni kuwa makini wakati inapokubaliana na masharti hayo ya mikopo na misaada isiwe tunafanya tu kwa lengo la kuwafurahisha nchi za ulaya wakati kwa uhalisia tunaoumia ni sisi na vizazi vyetu huku wao na vizazi vyao wakinufaika.

Pia ningependa kujua, je ni lazima tukope na kupokea misaada toka nchi za Ulaya ili mahusiano yetu na wao yawe mazuri.

Kwani hatuwezi kuwa na mahusiano nao mazuri bila kukopa na kupewa misaada.

Nasema hivi kwani inaonekana kwamba kukopa na kuomba misaada ndio njia pekee ya kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya.

Nachelea kusema kwamba Nchi za Ulaya zinanufaika mno na mikopo na misaada wanayotupa maana wasingepata hasira kwa sisi kukataa mikopo na misaada yao.

Tuwe makini.
Kwani mahusiano yalikuwa yamekufa? Hii ni lugha mbaya ya kujikweza tu; Tanzania haijawahi kuvunja mahusiano yoyte na nchi za ulaya. Kuna nchi hazikufurahia maamuzi ya serikali ya Tanzania lakini siyo kuwa mahusiano yalikuwa yamevunjika. Ni afadhali aseme kuwa amezifurahisha nchi za ulaya lakini siyo kuwa karudisha mahusiano na nchi za ulaya.
 
Haya mambo ya wachumi pasua kichwa. Nakopa halafu napangiwa tumieje mkopo huo. Hivi hapo nimekopa kweli ama natumikishwa...yaani nimefunguliwa genge na bosi jioni mahesabu? Wachumi nisaidieni jamani nielewe mambo haya.
Logic ni kwamba mtu unakopa kulingana na business plan yako ila kilichopo hapa ni kuwa anayekupa fedha anakuchagulia cha kufanya na namna ya kurejesha.

Halafu usipokopa unageuka adui.
 
Kwani mahusiano yalikuwa yamekufa? Hii ni lugha mbaya ya kujikweza tu; Tanzania haijawahi kuvunja mahusiano yoyte na nchi za ulaya. Kuna nchi hazikufurahia maamuzi ya serikali ya Tanzania lakini siyo kuwa mahusiano yalikuwa yamevunjika. Ni afadhali aseme kuwa amezifurahisha nchi za ulaya lakini siyo kuwa karudisha mahusiano na nchi za ulaya.
Ulichosema ni sahihi mkuu,
 
Kuwa wapole ni makosa na kukubali kuendelea kuwa katika hali hiyo ni makosa zaidi.

Kumbuka wenzetu wote tuliokuwa nao sawa miaka 60 iliyopita leo wanatupa misaada.

Kwanini sisi tusiachane na hii kasumba ya kukubali kwamba hizi ndio kanuni za kidunia??

Hizo ni propaganda tu za kutufanya tuogope kuachana na utumwa wao.
Utumwa unaanzia kwetu wenyewe, kukataa kufanya kazi kwa bidii, kukosa nidhamu kuanzia utotoni.

Wenzetu wanafundishwa kujinyima tangia utotoni, sisi tunaachiana tu, tunaishi tu.

Kuomba omba kuna malengo yake maalum, ni kufanikisha miradi na kuendesha uchumi wa nchi.

Kusema sisi ni matajiri wakati hatuna cha kwetu tulichovumbua, ni sawa na kupaka rangi upepo.
 
Umesema kwamba wenzetu wanafundishwa tangu utotoni well magufuli kusema kwamba sisi ni matajiri alikuwa anasema ukweli ukweli ambao ungewasaidia watoto wa sasa kutambua potential ambayo nchi hii inayo na hivyo kuitumia vyema.

Magufuli alihimiza nidhamu na uchapa kazi (falsafa ya hapa kazi tu) hili limesaidia wengi waliopo sasa na wanaokuja kushika nafasi kwa baadae.

Kuwa omba omba ni laana.

Tuondoe hii laana ya mikopo na misaada.
 
Back
Top Bottom