Rais Samia amesema anarejesha mahusiano na nchi za Ulaya. Je, kukopa ndio njia bora ya kufanya hivyo?

Rais Samia amesema anarejesha mahusiano na nchi za Ulaya. Je, kukopa ndio njia bora ya kufanya hivyo?

Mtoa mda napenda sana unavyohangaika humu awamu hii, hadi ikaishe naamini akili itakuwa imekukaa sawa.

Kipindi cha Magu ulikuwa miongoni mwa chawa wakuu, mkiwaita wakosoaji kuwa ni wapiga dili na mirija yao imekatwa. Sasa kwa hali hii nadhani kamba yako imekatwa na ikafungwa juu ya mti kiasi kwamba hata majani yaliyo miguuni mwako huyafikii.

Kila uzi ninaoingia nakukuta unalialia, sasa umeona haitoshi umeanza kufungua nyuzi zako mwenyewe!

giphy.gif

KARMA is a Bitch!!!
 
Hoja hapa ni rahisi tu.

Je kukopa ndio njia inayosemekana ya kurejesha mahusiano na nchi za Ulaya??

Je hakuna njia nyingine ya kufanya hivyo??

Majibu yake tafadhali.

Jibu lake ni kwamba hakuna njia nyingine mkuu! Labda ccm itoke na kije chama kingine huenda kitakuja na njia mbadala
 
Aliyekudanganya kwamba Magufuli alikuwa hakopi bila shaka alikuloga pia .
 
Mh. Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha...
Ni uwongo mkubwa kudai kwamba wakati wa Magufuli, aliwahi kukataa mikopo su misaada. Huo ni uwongo mkubwa. Ukweli ni kwamba, watoaji wa misaada na mikopo wa nchi za Ulaya, America na vyombo vya kifadha vya kimataifa, kama WB, ndip waliokataa kutupatia, kwa sababu chini ya utawala wa Magufuli, Tanzania ilikuwa ya utawala wa kidikteta.

Sharti kubwa la mikopo na misaada toka mataifa yaliyoendelea, ni Serikali izingatie demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Wakati wa uongozi wa dikteta marehemu Magufuli, hivyo vyote vilitoweka kwa 100%.
 
Sio kwa kasi hii ya sasa.
Utawala wa Magufuli ulikopa kuliko utawala wowote, tena kutoka mabenki ya kibiashara, kwa riba kubwa sana. Hatushangilii ukopaji, lakini kama ni kwa kulinganisha katika ukopaji, basi utawala wa Magufuli ulikuwa ni nguruwe, na utawala wa Samia ni simbilisi.
 
Onaga aibu basi kuwasifia hao washenz wanaopata maendeleo kwa kuiba resources za nchi yako kupitia mikataba mibovu.

Weng mnaomlaumu magu ninyi ni bendera fuata upepo, hiv unaweza orodhesha hayo aliyowajaza watu ambayo hayana ukweli...
Magufuli hakuifanya nchi ijitegemee. Kikubwa alichofanya ni kuendesha siasa za hila, uwongo na ulaghai. Akawadanganya watanzania wajinga kuwa tunajenga miradi kwa pesa yetu wakati anakopa kila mahali alipoweza kupata, tena kwa riba kubwa.
 
Wazungu hawakuacha kuja kutalii kipindi cha Magufuli, Wakati huo bishara ilikuwa nzuri tu kwani sisi tulikua moja wapo ya nchi chache ambazo hatukua na lock down...
Ukiwa mjinga, unaweza kuamini uwongo wa Marehemu Magufuli. Ni uwongo mkubwa kudai exports ziliongezeka wakati wa Magufuli. Exports za mazao ya kilimo zilianguka kwa 50%, ukuaji wa utalii ulianguka toka 15% mpaka 3.6%.

Ukuuaji wa uwekezaji ulianguka toka 28% mpaka 4%. Magufuli alikuwa mtawala mzuri kwa wajinga wa kufumu, wasio na akili wala uelewa.
 
Mh. Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha...

Mkuu Stroke mimi nakupongeza kwa kujishughulisha na maslahi ya kitaifa hata kama hoja yako katika bandiko hili imepinda na haina msingi wa uhalisia wa mambo. Sikujua kuwa una mawazo makubwa zaidi.

Angalau ni bandiko la maana kuliko yake ya enzi zile ya kuizodoa CHADEMA tu bila kusema cha maana.
 
Rais hajakopeshwa fedha isipokuwa alipewa msaada (grant) ambao ulizuiliwa kutokana na sera mbaya za jiwe na kuzorota kwa uhusiano wa Kimataifa.
 
Tatizo halipo kwenye kukopa ila pesa hzo haziendi sehemu husika zinaishia kwa watu wachache tu halafu mzigo anabeba mwananchi ni juzi tu hapa morogoro wamekamatwa watu na mabilion ya pesa kule kwa ally hapi watu wamepiga pesa za miradi
Mi naona hzo pesa hazina msaada wowote kwa wananchi wananufaika wao na familia zao.
 
Ni uwongo mkubwa kudai kwamba wakati wa Magufuli, aliwahi kukataa mikopo su misaada. Huo ni uwongo mkubwa. Ukweli ni kwamba, watoaji wa misaada na mikopo wa nchi za Ulaya, America na vyombo vya kifadha vya kimataifa, kama WB, ndip waliokataa kutupatia, kwa sababu chini ya utawala wa Magufuli, Tanzania ilikuwa ya utawala wa kidikteta.

Sharti kubwa la mikopo na misaada toka mataifa yaliyoendelea, ni Serikali izingatie demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Wakati wa uongozi wa dikteta marehemu Magufuli, hivyo vyote vilitoweka kwa 100%.
Demokrasia ndo hii mtoto akipata mimba arudi shule na afuate masharti ya Corona tusubirie na hela za kuruhusu ushoga sasa.
 
Back
Top Bottom