Rais Samia amkabidhi nyumba Rais Mstaafu Kikwete

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Shughuli hiyo muhimu ya kukabidhi nyumba ya kuishi maalumu kwa Mzee Kikwete imefanyika leo na Kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani

719B9900-3CA4-4F3E-94B4-4A150F0E5A30.jpeg

68D61EAC-6F35-437A-B934-9946CA8BA65C.jpeg

65D47C1B-23A8-4DA5-8A08-86665C626853.jpeg
 
Utaratibu wa mirath kwa levo ya Marhum Pombe unakuwaje yaan na wao huwa wanakaa kikao cha familia na kupeleka muhtasar wa kikao mahkaman ili kumpata msimamiz wa mirath au kuna namna myingine!!!???
 
Duh. No comment.

Kikwete ana mshahara 80% ya rais aliye madarakani.
 
Wanagawiana utajiri wa nchi hii kama Njugu.

Kikwete mwenye Lijumba lote lile Msoga ana shida gani ya nyumba?

Wanajitungia misheria ya kulipana mibenefits ya kufuru halafu tukiwauliza wanajitetea kwa sheria hizohizo!

Hiyo nyumba wala hajajengewa Kikwete bali ni urithi wa Riziwani, Miraji, Salama, Mama Salma na watoto wa Kikwete.

Mambo mengine ya nchi hii yanatia kinyaa ajabu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi nyumba ya kuishi Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete iliyojengwa katika Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam.

Nyumba hiyo imejengwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ikiwa ni utekelezaji wa kifungu namba 12 cha Sheria ya mafao ya hitimisho la kazi kwa viongozi wa siasa, sura ya 225 na marejeo ya mwaka 2020 ambayo pamoja na stahili zingine za matunzo ya viongozi wakuu wastaafu inaelekeza kuwa Rais anayestaafu anastahili kujengewa nyumba ya kuishi yenye hadhi ya Rais.

184135522_3815174611926818_2650470563457870835_n.jpg


Je, ni lini sheria zitarekebishwa ili kila mstaafu ajengewe nyumba yenye hadhi ya kazi yake aliyokuwa anafanya?
 
Back
Top Bottom