Rais Samia amkabidhi nyumba Rais Mstaafu Kikwete
Nenda kasome katiba siyo kuleta uchochezi . Mkapa naye alipewa, mbona hilo husemi?
 
Dadeki, huku Wana Dar es salaam wengi wakiishi store na kitchen bado wenye majumba na magari wanazidi kupewa mengine
 
Hizi nyumba watakabidhiwa marais wote wastafu na zilinza kujengwa kipindi cha jpm hii kikwete alisema waimalize kwanza yeye bado amepanga na hadaiwi kodi hatimae leo wamekabidhi


Nyie maskini mtajijua awamu hii ipo kwa wakubwa na matajiri wa taifa
Nyumba zilianza kujengwa wakati wa JPM alafu papo hapo unasema awamu hii ipo kwaajili ya wakubwa! Hivi zinakutosha kweli?

Ninyi wahuni mlioachwa na marehemu Mungu wenu mnajipa tabu sana.

MMpaka mama amalize awamu yake mtakuwa mmeshapata vyeti vya mirembe
 
Wanagawiana utajiri wa nchi hii kama Njugu.

Kikwete mwenye Lijumba lote lile Msoga ana shida gani ya nyumba?

Wanajitungia misheria ya kulipana mibenefits ya kufuru halafu tukiwauliza wanajitetea kwa sheria hizohizo!

Hiyo nyumba wala hajajengewa Kikwete bali ni urithi wa Riziwani, Miraji, Salama, Mama Salma na watoto wa Kikwete.

Mambo mengine ya nchi hii yanatia kinyaa ajabu.
Watumishi wanaambiwa wasubiri, serikali haina pesa.
 
Kila kamba ile kwa urefu wa mbuzi yake.
 
Kama ni nyumba tayari yupo kwenye nyumba yake ya milele aliyojengewa na serikali tarehe 26/03/2021
Tena ile nyumba ya 26 March ni nzuri ajabu. Kitu kilikuwa kina slide kama mtelezo. Ila naye lazima ajengewe nyumba. Alianzisha na itahusu marais wote watakaokuja kwa kuanza na yeye. Mjanja sana.
 
Tena ile nyumba ya 26 March ni nzuri ajabu. Kitu kilikuwa kina slide kama mtelezo. Ila naye lazima ajengewe nyumba. Alianzisha na itahusu marais wote watakaokuja kwa kuanza na yeye. Mjanja sana.
Ajengewe ya pili wakati hayupo?
 
Amefungulia twitter, bank account za watetezi wa haki za binadamu zilizofungwa na Magufuli, amendoa VRF ya HESLB, n.k. Fanya research kabla ya kuropoka!
Mweleze huyo mkuu wangu. Kwanza mwambie kuwa kazi kubwa kuliko zote ni kurejesha furaha na uhuru wa mtanzania ulioporwa miaka 5 na ushee. Hata asipofanya kazi nyingine hiyo tu inatosha kwa mwaka 2021.
 
Back
Top Bottom