Rais Samia amkabidhi nyumba Rais Mstaafu Kikwete
Nakumbuka nyumba ya mzee mwinyi ilitumia kiasi shilingi vzaidi ya bil 7, amekabidhiwa akiwa na miaka 95! Ccm ni ileile
Tuliaaa! Mama anawakomesha mataga
 
Enh bado mziki unaendelea kumbe... kwahiyo kila Raisi aloyeko madarakani anakabidhi nyumba kwa maraisi waliopita pamoja na wizi wote walioufanya au hii kuwafumba midomo
Tulia mama awakomeshe mataga
 
Marehemu baba yangu alikuwa mwalimu zaidi ya miaka 40, akastaafu mkulima wa kibanda cha makuti, baada ya kuwafundisha hawa hawa au watoto wao!
Kumbe kuna kazi hapa hapa Tanzania unafanya miaka 10, Utembelee dunia nzima, hatimaye uzawadiwe nyumba, 80% ya mshahara, watumishi, walinzi, kufuta jasho! Sioni wivu, ila najilaumu tu kwa nini sikupiga, garagaza, ua, ongopa, nipate kazi hiyo?
Wanajiaminisha nini kutangaza mambo haya? Pengine wana malengo mazuri ya kutaka sisi wote tujaribu kupata kazi kama hiyo, 'by any means necessary'!
 
Ni haki watu warogane kwani ni mtanzania gani asiyependa mashavu kama hayo, unalipwa penshen na marupurupu kibao kama rais mtaafu na nyumba kiwango yenye hadhi ya rais unapewa?
 
Tulieni dawa iwaingie, mama anatupeleka pazuri 😝😝😝 nchi ilipoteza dira!
Msimtafutie sababu Mama hizi sheria kazitunga mwenyewe JPM wakati wake na alishamkabidhi Mwinyi na Mkapa ya Kikwete alikuwa amkabidhi wiki 2 kabla hajafariki hapa anatimiza haki za kisheria. Suala la sheria mbaya au nzuri hilo ni jambo lingine lakini zote zilipishwa bungeni tena kwa makofi na sisi tukawapa tena 99% mwaka jana. hakuna kulalamika kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom