Pre GE2025 Rais Samia ampa Sheikh wa Arusha Land Rover Discovery limsaidie kwenye shughuli za kidini. Hii si Rushwa kabisa?

Pre GE2025 Rais Samia ampa Sheikh wa Arusha Land Rover Discovery limsaidie kwenye shughuli za kidini. Hii si Rushwa kabisa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwamba Sheikh hakuwa na gari la kutembelea?
 
Kwenye mahubiri kila ijumaa tujiandae
1.kusikia tudumishe amani yetu kuna wachache wanataka kutuvuruga..
2. Nani kama mama
3. Mitano tenaView attachment 3135085
nyerere day, kuna sheikh alipiga dua pale alisema chama kiendelee kubaki madarakani na vyama vingine vizidi kukisaidia chama hiki.
 
nyerere day, kuna sheikh alipiga dua pale alisema chama kiendelee kubaki madarakani na vyama vingine vizidi kukisaidia chama hiki.
Yeye nawe atakuwa alishapewa kisirisiri au yupo kwenye zamu.. kwahiyo alikuwa anapalilia jambo lake.. hawaropokagi bure hao watu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
*#&%$@ g#&%$$$hezi yaani kama sio kwamba kuna kupigwa ban leo ningetukana humu mpaka nyote mngejuta
Gari moja, gari moja, gari moja
 
Wakuu,

Nawaacha mtoe mapovu, mambo ndio kama haya, Sheikh amepewa land rover bana likamsadie kwenye kutoa huduma zake.... Hii si rushwa kabisa? Tusubiri 'zawadi' hizi ziendelee kutolewa kwa viongozi wengine wa dini.

Tunataka uchaguzi ufanyike kila mtu akiwa na fursa sawa ya kushindana, kwa namna hii mwenzangu na mimi atakuwa na nafasi ya kushindana na mtu kama huyu? TUNAFANYAJE KUMALIZA HAYA? Kwa kuendelea kuwa chawa na kulalamika?

Narusha swali kwenu Wakuu.


Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amekabidhi gari mpya chapa ya Land Rover Discovery yenye Thamani ya Milioni 100 kwa Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma ili kuweza kumsaidia kwenye shughuli zake za kidini Mkoani hapa.

Kupata vimbwanga vingine wakati wa Uchaguzi ingia hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Paul Makonda amekabidhi gari hilo muda mchache baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa kwenye msikiti Mkuu wa Bondeni Jjjini Arusha leo Oktoba 25, 2024, akiwataja Viongozi wa dini kama msingi mkuu wa amani na utulivu unaoshuhudiwa kote nchini Tanzania.


Kwa Upande wake Sheikh Shaaban Bin Juma baada ya kukabidhiwa gari hilo, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Upendo wake kwa Watanzania, akimuombea Kheri Rais Samia pamoja na wasaidizi wake katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.:BearLaugh::BearLaugh:
Tutaona mengi hata ambayo hatukuona tangia uhuru ,
 
Back
Top Bottom