PreGE2025 Rais Samia ampa TSh 20 milioni Askofu wa jimbo jipya la Bagamoyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa TSh20 milioni kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Stephano Musomba, kwa ajili ya kusaidia gharama za mafuta ya gari katika mizunguko yake ya kichungaji.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo Jumapili, Mei 4, 2025 na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliyemwakilisha Rais Samia katika ibada ya kumsimika rasmi askofu huyo, iliyofanyika mkoani Pwani.

"Ninaomba nimalizie hotuba hii kwa kukabidhi fedha kidogo, TSh20 milioni ambazo Rais amenituma nimkabidhi Baba Askofu Msomba kwa ajili ya mafuta ya gari ya kuanzia ziara zake za kichungaji, katika jimbo hili jipya," amesema Dk Mpango.
View attachment 3324484
Kwa kuwa zimetoka sirikali ni vizuri kusema serikali imetoa shillingi millioni 20 kumsaidia Askofu.....
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa TSh20 milioni kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Stephano Musomba, kwa ajili ya kusaidia gharama za mafuta ya gari katika mizunguko yake ya kichungaji.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo Jumapili, Mei 4, 2025 na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliyemwakilisha Rais Samia katika ibada ya kumsimika rasmi askofu huyo, iliyofanyika mkoani Pwani.

"Ninaomba nimalizie hotuba hii kwa kukabidhi fedha kidogo, TSh20 milioni ambazo Rais amenituma nimkabidhi Baba Askofu Msomba kwa ajili ya mafuta ya gari ya kuanzia ziara zake za kichungaji, katika jimbo hili jipya," amesema Dk Mpango.
View attachment 3324484
Maaskofu rudisheni hiyo pesa.
 
Milioni ishirini kwa ajili ya mafuta..
Anaendesha scania au bus huyo askafu?
Kwakuwa kwa hiyari na kwa moyo ameona hivyo achana na maswali mengine kilichobaki ni mhusika kuona inatumikaje ili kutoa huduma kwa jamii ikiwa ni pamoja na sauti ya haki,uhuru,uwazi na amani kwa mambo ya kijamii na kitaifa.
 
Mi nilikua nahoji tu na kujiuliza kwa maana hio pesa ya mafuta tu unanunua gari..
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa TSh20 milioni kwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Stephano Musomba, kwa ajili ya kusaidia gharama za mafuta ya gari katika mizunguko yake ya kichungaji.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo Jumapili, Mei 4, 2025 na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliyemwakilisha Rais Samia katika ibada ya kumsimika rasmi askofu huyo, iliyofanyika mkoani Pwani.

"Ninaomba nimalizie hotuba hii kwa kukabidhi fedha kidogo, TSh20 milioni ambazo Rais amenituma nimkabidhi Baba Askofu Msomba kwa ajili ya mafuta ya gari ya kuanzia ziara zake za kichungaji, katika jimbo hili jipya," amesema Dk Mpango.
View attachment 3324484
Kutoa kodi zetu kuchangia makanisa na misikiti ni kuchanganya dini na siasa,na kwa hali tete iliyopo baada ya shambulio la Dr. Kitima hii ni rushwa ili kuliziba mdomo Kanisa Katoliki, hii haikubaliki kabisa.
 
Imeshakubalika wamepokea.
 
Back
Top Bottom