Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo anatakiwa afungweakisubiri kazi nyingine.
mhhhWe unaishi hapa Tanzania? Yule dereva aliyefariki Mbeya ulipata taarifa zake? Mwanza kituo cha polisi kirumba unafahamu habari zake? Watu wanauliwa na mkuu wa mkoa anajua sio wahalifu.
😂 😂 😂 😂Kwani Katiba inasemaje kuhusiana na Nafasi ya Supika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania?
Sababu za kukoma kuendelea na Nafasi hiyo?
kuna mufungwa mdomoHuyo anatakiwa afungwe
Bado Muro wa Meru"Piga mchungaji mkuu mwovu na vikondoo vidogo vidogo viovu vitatawanyika na kukamatwa kimoja kimoja na kuchinjwa kabisa"
Mchungaji mwovu: Mwendazake Magufuli
Vikondoo vyake viovu: Kina Ole Sabaya, Makonda, Chalamila, Jerry Muro nk nk vinaanza kutawanywa na vinachinjwa kimoja kimoja...
Hakuna UOVU unaodumu...
Haki hudumu daima...
Haileweki hasa huyu kijana Ole Sabaya alikuwa na sababu gani kupambana na Freeman Mbowe - M/kiti wa CHADEMA - Taifa.
Ngoja uchunguzi uanze,wako mashahidi wengi ambao wamemrekodi kwwnye cctv akivamia Nyumba za watu ma kuomna Rushwa kwa nguvu.kuna mufungwa mdomo
kufungwa kamba
kufungwa jela
na kufungwa vifungo vya shati.
kufungwa jela haiwezekani.
jamani mkuu wa wilaya Hai atoke eneo lake la kazi akafanye hayo kwenye eneo la mwingine Arusha!!!!?? hebu tupeni tuhuma za kweli kama kazi tayari ameshafutwa hakuna haja ya kumchomea kiasi hicho,Sabaya matatani kwa kumshambulia Diwani wa Sombetini Arusha
![]()
Philip Kana 23rd February 20210 Comments
MKUU wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, ambaye amekuwa anatuhumiwa na kuhusishwa na matendo kadhaa ya kijambazi, sasa ametuhumiwa kumshambulia Diwani wa kata ya Sombetini, jiji Arusha, Bakari Msangi, Februari 9 mwaka huu. Katika tukio hilo, Sabaya aliambatana na walinzi wake binafsi sita wakiwa na bunduki moja na bastola mbili.
Kwa mujibu wa Msangi na watu walioshuhudia tukio hilo, diwani huyo alishambuliwa baada ya kupigiwa simu na mfanyabiashara mmoja mkoani humo, Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la mapazia la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu, jijini Arusha.
Mfanyabiashara huyo alimpigia Msangi simu akimuomba msaada baada ya vijana wake wa dukani kumtaarifu kuwa Sabaya na vijana wake wamewafungia dukani na wanawapiga.
Sabaya alikuwa anahitaji shilingi milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara huyo, Asaad, akimtuhumu kufanya biashara ya kuuza fedha za kigeni kwa magendo.
Sabaya alitaka apewe fedha hizo, vinginevyo angemfungulia Asaad kesi ya uhujumu uchumi.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Salum Hamduni, Februari 16 mwaka huu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akasema wanaendelea na uchunguzi ingawa hakuwa tayari kulizungumzia kwa kina.
Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama mkoa Arusha, ambacho mwenyekiti wake ni mkuu wa mkoa, Iddi Kimanta, kilichokaa Februari 12 mwaka huu, kilimwalika diwani Msangi na kupokea maelezo yake, kisha kikamwagiza RPC Hamduni kuhakikisha anaendelea na taratibu za kipolisi wakati wao wakiendelea na taratibu za kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi wa DC Sabaya. Tangu siku hiyo, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Siku ya tukio, Sabaya alifika dukani kwa mfanyabiashara huyo majira ya saa 11 jioni akawataka wafanyakazi wake wamweleze alipo Asaad. Walimpigia simu akawa hapokei.
“Waliniambia mpigie simu mjomba wako mwambie tunataka pazia. Mimi nikampigia mjomba simu ikawa inaita tu. Wakatunyang’anya wafanyakazi wote simu tukawekwa chini ya ulinzi,” alisema mmojawao, Norman Jasin, na kuongeza:
“Nilikuwa mimi na mfanyakazi wangu mmoja, ikawa mtu yeyote akiingia dukani anawekwa chini ya ulinzi wanataka kujua ni nani. Machinga waliokuwa wanaona duka linafungwa wanakimbilia kuchukua mali wawapelekee wateja akiingia wanawekwa chini ya ulinzi na kipigo juu.”
“Walivuta mlango wakaanza kutupiga kwa kupokezana. Sabaya akawa analazimisha tusema mjomba Asaad alipo, sisi tukawa hatujui, tukipiga simu yake inaita tu. Sabaya akapanda juu akageuza kamera ili wasionekane, lakini ilikuwa imesharekodi.”
“Diwani Msangi alipofika dukani hapo akawa anaongea na Sabaya lakini tukashangaa na yeye anapigwa hata kuliko sisi.”
(Diwani Msangi, wa kwanza kushoto, katika picha na makada wenzake wa CCM Arusha).![]()
Kwenye tukio hilo vijana wa duka hilo zaidi ya watatu na wateja wao walipigwa. Kuna waliojisaidia haja kubwa na waliojikojolea .
Baada ya kuwapiga sana, majira ya saa tatu usiku, aliwachukua vijana wawili akawapeleka kwenye kituo kikuu cha polisi na kuagiza wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi huku akiondoka na diwani Msangi ambaye walikuwa wamemfunga pingu.
Msafara wa Sabaya ulikuwa wa magari mawili. Gari moja liliwabeba vijana wawili wa dukani na jingine ambalo alikuwemo Sabaya mwenyewe aliingizwa diwani Msangi.
Sabaya ametumia gharama kubwa kuhakikisha habari hii haiandikwi kwenye chombo chochote cha habari. Siku moja baada ya tukio hilo waandishi walianza kuifuatilia.
Sabaya alipopata taarifa majira ya saa 2 usiku waandishi hao wakiwa wameweka kambi polisi, aliwasiliana na mmoja wao, kisha akawatumia kiasi cha shilingi laki nne kwenye simu ya mwandishi mmoja.
Hata hivyo, alipata taarifa kuwa bado kuna waandishi wengine wanne wanafuatilia habari hiyo aliwasiliana na mmoja wao akawaita ofisini kwake Hai, akawapa fedha, laki moja moja.
Baada ya hapo, alikuwa akijipongeza kuwa suala hilo limekwisha, akiwaeleza watu wake wa karibu kuwa suala hilo lingekuwa gumu kulimaliza endapo vyombo vya habari vingeandika, ila kwa hatua iliyopo anajua namna ya kulimaliza.
Hata hivyo, amekuwa akiendelea na jitihada za kumshawishi diwani Msangi wayamalize, na yuko tayari kumpatia hata fedha milioni 20, lakini imeshindikana.
Sabaya amekuwa akizunguka mara kwa mara jijini Arusha huku akilazimisha wafanyabiashara wampe fedha, vinginevyo atawafungulia kesi za uhujumu uchumi.
Amekuwa akizunguka na magari yake binafsi matatu ambayo hubandika namba za usajili tofauti tofauti ikiwemo za umoja wa mataifa (UN) na ya Miradi inayofadhiliwa na watu kutoka nje ya nchi, (DFP) ambapo huwa na mabaunsa kati ya watatu na sita na hupenda kufikia hoteli za kitalii za Tulia, Mount Meru, Orlando Garden na Lush garden.
Sabaya amekuwa akitumia muda mwingi jijini Arusha wakati yeye ni Mkuu wa wilaya ya Hai, jambo ambalo limekuwa likiibua maswali mengi kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara ambao ndio wahanga wa matukio yake ya kitapeli.
(ole sabaya)![]()
Mwaka 2019 Sabaya alikusanya zaidi ya milioni 300 kutoka kwa wafanyabiashara jijini hapa akiwaahidi kuwatafutia fursa ya kuwa miongoni mwa wafanyabiashara watakaoshiriki kikao cha Rais John Magufuli na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo zilipofika Ikulu Sabaya aliitwa na alishikiliwa kwa siku tatu ili atoe maelezo ambapo yeye mwenyewe anasema kilichomsaidia wakati ule alikuwa akinunua madiwani na viongozi wa Chadema Hai .
Sabaya ambaye huongea kwa kujidai na kujiamini mbele za watu anasema alimweleza Rais, Magufuli fedha ni kweli alichukua na ndiyo anazitumia kutekeleza mpango huo a na kamhakikishia Rais Magufuli atazitumia kumng’oa Freeman Mbowe kwenye ubunge jimbo la Hai hivyo akasamehewa.
Sabaya amekuwa akitumia mamlaka yake ya ukuu wa wilaya kuwatisha wafanyabiashara kwenye mikoa ya kilimanjaro na hasa Arusha huku ambapo kwa wenye vituo vya mafuta hutumia mabavu kulazimisha magari yake matatu anayozunguka nayo yajazwe mafuta.
Hata hivyo tayari baadhi ya wafanyabiashara hao wameamua kutoa taarifa kwa mkuu wake wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mugwira ndipo akapunguza kuwatisha.
Sabaya amekuwa na kawaida ya kuongozana na mabaunsa wake na amekuwa akionekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe ila amekuwa na tabia ya kutokulipa bili mara baada ya kuanya matumizi.
“Sabaya akiingia hapa kila mtu hataki kumhudumia. Huwa anakunywa na kula lakini halipi. Unashangaa wanaanza kuondoka mabaunsa wake halafu yeye anakuwa wa mwisho kuondoka akiwa anaongea na simu hata ukimfuata mpaka kwenye gari anaendelea kuongea na simu huku gari inaondoka,” alisema mhudumu wa bar moja iliyopo maeneo ya Sakina.
Hadi tunaenda mitamboni, Sabaya hakupatikana kujibu hoja na tuhuma zinazomkabili. SAUTI KUBWA inaendelea kumsaka.
Hatimaye Mbowe kashinda
Majibu ya Mungu huja kwa wakati sahihi, nashauri na Makonda achunguzwe utajiri wakeNdio atamuelewa Mbowe ni nani? Hahahaha Mbowe ni Mtoto wa mjini
Ewaaaa.... fanya maarifa basi...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Babu tulia basi, hebu ukuje nyumbani tuyamalize.
Kwa Serikali ya dikteta bwana yule... hakuna lisilowezekana kwa team Mataga...jamani mkuu wa wilaya Hai atoke eneo lake la kazi akafanye hayo kwenye eneo la mwingine Arusha!!!!?? hebu tupeni tuhuma za kweli kama kazi tayari ameshafutwa hakuna haja ya kumchomea kiasi hicho,
Una uhakika gani hajamwita kumsikiliza?Ukiwa kiongozi mwenye maono muite na muulize tatizo ni nini? Baada ya hapo tafuta mbinu ya kusikiliza upande unaolalamika baada ya hapo fanya maamuzi, tofauti na hivyo huu ni mwendelezo wa Rais anae sikiliza maoni ya watu pasipo kujiridhisha.
Safi kabisa mama SASHRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021
Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo
RC Kilimanjaro Anna Mghwira alaani wahuni walioshambulia msafara wa Tundu Lissu
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ameshutumu vikali kitendo kilichofanywa na vijana wahuni wanaodaiwa kukodiwa na kuushambulia kwa mawe msafara wa mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu. Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mkuu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini Askofu Shoo...www.jamiiforums.com
Kilimanjaro: Waliohusishwa na utekaji wa watu na kujitambulisha kama Usalama wa Taifa watiwa mbaroni
Watu watatu waliokuwa wakimfuatilia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia wakiwa na gari aina ya Toyota Prado namba DFP 788 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Moshi jana saa 10 alasiri eneo la KDC baada ya Polisi kufukuzana na gari hilo na kufanikiwa...www.jamiiforums.com
Mbowe: Ole Sabaya akiwa na gari lenye namba UN na silaha za moto aliongoza genge la wahalifu kwa lengo la kunidhuru na kuniua
DC wa Hai Ole Sabaya akiwa na gari yenye namba @UN na silaha nzito za moto ameongoza genge la wahalifu kuvamia Hotel ya Kitalii ya Aishi, Machame kwa lengo la kunidhuru na kuniua. Wameteka, kutesa na kuumiza walinzi wawili wa hotel. Wamepora silaha yao na kuwatekeleza Arusha Rd. Pia soma...www.jamiiforums.com
Ole Sabaya ukipona hii panguapangua, chinja kondoo
Huu ni ushauri wa bure kabisa nakupa mdogo wangu Mkuu wa Wilaya ya Hai Bwana Lengai Ole Sabaya. Ukibahatika kuendelea kuwa Mkuu wa hiyo Wilaya ya Hai katika hii pangua pangua inayokuja tafuta kondoo mweupe mchinje waite Masheikh hapo Bomang'ombe wakufanyie dua! Na usirudie tena kutumia mamlaka...www.jamiiforums.com
Uchaguzi 2020 - Lema: Msafara wa mgombea Urais, Tundu Lissu washambuliwa vibaya katika Ofisi ya CHADEMA Wilayani Hai, Kilimanjaro
Aliyekuwa Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter amesema msafara wa Tundu Lissu umevamiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilayani Hai Amesema "Msafara wa mgombea Urais Mh Tundu Lissu umevamiwa na kushambuliwa vibaya katika ofisi ya CHADEMA HAI,magari yame...www.jamiiforums.com
Habari ndo hiyo
Nawatakia Eid Njema.
====
Alizaliwa mwaka 1980 katika mkoa wa Arusha
Hayati John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 alimteua Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai
CHAMA: CCM
#NA SASA KAZI IMEANZA#
TAARIFA ZA ELIMU YAKE
SVISC. MASSACHUSET UNIVERSITY USA
BSC.ED ST JOHN UNIVERSITY DODOMA
UNED: SINIOUR SIX –BUGEMA HIGH SCHOOL-UGANDA.
FORM IV: IKIZU SEC SCHOOL
STD VII: SAMBASHA PRIMARY SCHOOL.
OTHERS: IST: PRESIDENT ST. JOHN’S UNIVERSITY DODOMA 2007.
CHAPEL PREFECT BUGEMA HIGH SCHOOL UGANDA.
CEO: TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT CENTRE
SEMINARS BSYMPOSIUM: S. KOREA YOUTH CONFERENCE ,SOUL
YOUTH SUMMIT COMMISSIONED BY HON. PINDA TYDC:2010
CAPRIPOINT YOUTH EMPOWERMENT 2014