PART 4
February 09, 2021 Sabaya na genge lake walienda Arusha kumvamia Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la mapazia la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu. Wakamwambia "tuna taarifa unafanya biashara ya kubadili pesa za kigeni kinyume cha sheria" Asaad akakataa.
Anadai Sabaya alimtaka atoe 100M ili asipewe kesi ya uhujumu uchumi. Lakini akamwambia wewe ni DC wa Hai unapata wapi mamlaka ya kuja kunihoji Arusha? Sabaya kusikia hivyo akaagiza milango ifungwe, wakampiga na kumtaka aoneshe pesa zilipo. Wananchi kusikia kilio wakampigia simu Diwani wa Sombetini Bakari Msangi. Alipofika na kuhoji akaunganishwa kwenye kipigo.
Kwa kifupi Sabaya alimiliki kikundi cha kigaidi. Na alikua anaenda nacho popote, iwe ofisini au night club. Hata juzi Dar alikua nacho, akizunguka nacho sehemu mbalimbali.
Mimi ni "survivor" wa kikundi hicho. November mwaka jana nilisema kitendo cha Sabaya kutumia plate number za UN kufanya uhalifu ni doa kubwa kidiplomasia. Akanipigia simu, sikupokea. Akaniandikia 'sms' ya vitisho. Akaniambia akinikamata nitajuta kuongelea vitu nisivyovijua. Sikumjibu lakini nikascreenshot na kumtumia rafiki yangu mmoja ambaye ni kiongozi serikalini just for reference likitokea lolote.
December 26 nikiwa na Don J Mbowe mahali flani Moshi, tukifurahia sikukuu za mwisho wa mwaka, tukaondoka saa 7 usiku. Kesho yake Meneja wa eneo hilo akanipigia simu akasema tulipoondoka tulimuachia balaa kubwa. Sabaya alifika na kikundi chake na kutuulizia. Alipoambiwa tumeondoka, hakuamini.
Akachomoa bastola na kufyatua hewani. Akaleta taharuki, watu wakatawanyika. Hakujali kuharibu biashara, alichojali ni kutimiza matakwa yake. Mabaunsa wakapekua counter hadi vyooni. Hatukuwepo.
Sijui wangetukuta ingekuaje. Pengine tungepigwa na kuwekewa dawa za kulevya mfukoni. Halafu kesho yake dunia ingetangaziwa kuwa tumekutwa na dawa za kulevya. Tungeshtakiwa na kunyimwa dhamana. Huenda hadi leo tungekua tunasota gerezani.
Lakini Mungu wa rehema akakumbuka watanzania tunaowarudishia(ga) tabasamu akaamua kutuokoa. Tuliondoka tukidhani tunaenda kupumzika, kumbe ilikua njia ya Mungu kutuepusha na mkono wa yule mwovu.