Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

You cared already!
Yaani wewe mtoto ungekuwa karibu na mimi ningekuwa nishakuchapa viboko.inaonekana huna adabu kwa wakubwa zako.unajibu jibu tu.

Embu kalale huko.kesho ukatume maombi serikali yenye matunda ya jpm imetoa kazi.

Jpm alishasema kuhusu hizi ajira.kwahiyo sio jambo geni msije anza kunikera hapa. Tutakerana ooh!!
 
Kuna watu wa hivyo sana katika taifa hili, hivi unapotokwa povu unamfananisha Sokoine na Saba utakua na akili sawa sawa?
Kabla hujaongea aibu hii hebu jibu maswali haya;

1.Hivi Nyerere au Sokoine alikua anaweza kuvamia maduka ya watu usiku na mabaunsa na kuleta vurugu?

2.Uliwahi kusikia Nyerere au Sokoine walinyoa Panki au Viduku?

3.Uliwahi kusikia Nyerere au Sokoine anavamia hoteli za watu usiku na mabaunsa wakilazimisha kupewa wanawake waliolala humo?

4.Ilikua tabia ya Nyerere au Sokoine wakijifanya kua ni usalama wa taifa?

Sabaya na Sokoine wafananishwe kwenye Kabila na sio matendo. Acheni madhambi ya kujitakia
 
Viongozi wengi waliopenda maigizo kipindi Cha magu wame keep low profile kuusoma mwendo wa mama naona huyu dogo alijisahau sn
 
Endelea kupiga pambio mama utakuja kujua hujui pindi ukion tumaini limepotezwa na chunusi. Ni kawaida ya mbwa akijifungua kumtafuna mwanae wa kwanza.

Kwa hiyo wewe unalinganisha makosa ya Kitwanga (Ulevi na ubabaishahi wa majibu bungeni) na Lugola (kucheza midundiko, suala la Lugumi na usimamishaji wa kibali cha kiongozi asasi) ni sawa na ya Ole Lengai? Wait for the nod and wink by deceptive agents to outsmart your passionate unto phenomenon drill.

Mbona unaweweseshwa na vitu vidogo sana? Yaani Sabaya anakuchetua vibaya mnooo
Wewe tulia huyo kapisha upelelezi na kazi inaendelea
Pole lakini kwa kuweweseka
 
Aaaah aah wanazi wa CHADEMA watafurahi sana!

Lakini kazi aliyofanya kwa wananchi wa kawaida ni ya kutukuka!pamoja na uwezekano wa kuteleza hapa na pale!

Bravo Sabaya!,

Mengine yanatazamika, yanatafsirika, yanajadilika, na yanasubirika. Muda utatoa maana Pana ya yanayotukia sasa.
Kazi gani mavi matupu
 
Yaani wewe mtoto ungekuwa karibu na mimi ningekuwa nishakuchapa viboko.inaonekana huna adabu kwa wakubwa zako.unajibu jibu tu.

Embu kalale huko.kesho ukatume maombi serikali yenye matunda ya jpm imetoa kazi.

Jpm alishasema kuhusu hizi ajira.kwahiyo sio jambo geni msije anza kunikera hapa. Tutakerana ooh!!
Ebu njoo pm nikusugue hicho kisimi wewe Bibi naona kinawasha achana na hao watoto
 
PART 1

Mama ametupa zawadi nzuri ya Eid. Huu ni ushahidi kuwa Sabaya ameumiza watu wengi ndio maana maamuzi ya kumfurusha yamepokelewa kwa furaha kubwa na nchi nzima.

Jambo la muhimu zaidi mama hajaishia kumfurusha tu bali ameagiza ufanyike uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ili afikishwe mahakamani. Kwahiyo sasa hivi Sabaya ni mtuhumiwa. Muda wowote tutamuona nyuma ya karandinga.

Sabaya ana tuhuma mbalimbali (lukuki) kama taarifa ya Ikulu ilivyoeleza. Anatuhumiwa kupora, kunyanyasa na kutumia madaraka yake vibaya. Tuhuma hizi zimekuwepo tangu enzi za mwendazake lakini amekua akilindwa.

Yeye mwenyewe amewahi kujitapa kuwa hakuna anayeweza kumpa order isipokua mwendazake pekee. Alimdharau hadi RC wake. Ndio maana mama Mghwira alipomwambia aache kutumia mabavu alimcheka kwa dharau. Mwaka 2019 PM alifanya ziara K'njaro wafanyabiashara wakamueleza jinsi Sabaya anavyowanyanyasa, lakini hakuchukua hatua yoyote. Akasema atayafikisha kwa mamlaka yake ya uteuzi.

Lakini hakuna chochote Sabaya alichofanywa. Badala yake alizidi kuwa kiburi kuliko mwanzo. Wale wafanyabiashara "waliomchongea" kwa PM walipata joto ya jiwe. Na PM hakuwa na chochote cha kumfanya. Hatimaye leo mama amevunja kisiki kilichowashinda maksai.

Sabaya anatuhumiwa kutumia mabavu kupora fedha kwa wafanyabiashara mbalimbali. Mmoja wao ni Cuthbert Swai mmiliki wa Asante Tours na Hoteli ya kitalii ya Weruweru.

Cuthbert anadai mwaka 2018 Sabaya alitaka ampe 10M otherwise atampa kesi ya uhujumu uchumi. Kwa kuhofia jela akampa. Baadae akataka tena 10M, akamwambia hana. Baada ya vitisho vya mara kwa mara, wafanyabiashara wenzake wakamwambia mpe tu, usicheze na mjinga atakutoboa jicho. Akampa kishingo upande.

Baada ya miezi michache Sabaya akamwambia kuna "special mission" amepewa hivyo inatakiwa pesa nyingi kuitekeleza. Kwahiyo wafanyabiashara wanatakiwa wachangie. Akamtaka Cathbert atoe 15M. Cuthbert akamwambia biashara ya utalii imeyumba hivyo hawezi kupata fedha hizo.

Na hapo akatangaza uhasama na Cathbert. Akaenda kwenye mashamba yake huko Rundugai akasema alidhulumu wanakijiji. Akatengeneza wazee feki waliojifanya wamedhulumiwa, halafu akatangaza kuyataifisha.

INAENDELEA, SOMA PART 2
 
PART 2

Hakuishia hapo akavamia hoteli ya kitalii ya Weruweru inayomilikiwa na Cathbert. Siku hiyo Nandy alikua na show Arusha, akalala Weruweru. Usiku saa 9 Sabaya akavamia akiwa na kikosi cha watu 6 wenye silaha. Akalazimisha aoneshwe chumba cha Nandy, mhudumu aliyekua mapokezi akakataa. Sabaya akampiga sana. Walinzi walipotoka nao wakapigwa na mabaunsa wa Sabaya.

Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV camera but who cares? Pamoja na video hiyo kusambaa lakini hakupewa hata onyo. Utamwambia nini mtoto pendwa wa mwendazake? Aliwahi kujitapa kuwa yeye ndiye DC pekee anayeweza kumpigia simu mwendazake usiku wa manane na akapokea.

Akaendelea kuvuruga biashara mbalimbali za Cathbert na kuagiza TRA wafreeze baadhi ya akaunti zake. Hali ikawa ngumu hadi mali za kampuni ya Asante Tours zikapigwa mnada. Akavuruga shamba la wanyama (zoo) la Cuthbert maeneo ya Maili sita. Akaharibu mizinga 200 ya nyuki kwenye shamba la Cathbert kwa madai hana kibali cha maliasili cha kufuga nyuki.

Baada ya hapo Cuthbert anadai Sabaya alitishia kumuua. Ikamlazimu kukimbilia ziwa Jipe mpakani mwa Kenya akaishi huko. Zaidi ya watu 300 waliokua wameajiriwa kwenye biashara zake mbalimbali wakapoteza ajira kwa sababu ya Sabaya. Just imagine.

Lakini hakuishia kwa Cuthbert, akaendelea kufanya ukatili kwa watu wengine. September 2020 alivamia hoteli ya Protea Aishi iliyopo Machame, inayomilikiwa na Freeman Mbowe. Hotelini hapo kulikua na wageni kutoka nje ya nchi wanaopanda mlima Kilimanjaro.

Sabaya akawakamata na kudai wamekuja kusaidia Chadema kwenye uchaguzi. Wakatolewa hotelini usiku wa manane na night dress kupelekwa kituo cha Polisi Bomang'ombe. Wakahojiwa na kuachiwa, lakini wamesababishiwa usumbufu, na wameweka doa kwenye sekta yetu ya utalii. Kumbuka tunatumia fedha nyingi kutangaza utalii, halafu mtu mmoja anawadhalilisha kwa mihemko tu.

Siku ya uchaguzi (October 25) alivamia tena Aishi hotel akiwa na magari yenye namba za UN. Wakawapiga walinzi na kukamata baadhi ya mawakala wa Chadema waliokua hapo. Wakawatia matambara mdomoni na kuwapiga sana kabla ya kwenda kuwatelekeza maeneo ya Sanya stesheni usiku huo.

INAENDELEA, SOMA PART 3
 
PART 3

Mmoja wa vijana hao Simon Mwacha alivunjwa mkono karibu na joint. Hadi sasa amefanyiwa upasuaji mara 3 lakini hajapona. Wiki iliyopita viongozi wa BAVICHA walimtembelea na kumkuta amewekewa POP jingine. Huu ni mwezi wa 7 tangu avunjwe na Sabaya na bado hajapona.

Kutumia number za UN kufanya uhalifu ni doa katika diplomasia ya nchi, lakini hakujali hilo. Yeye ni mtoto pendwa wa mwendazake, mtamfanya nini? Kama PM alishindwa kumfanya lolote, aliamini wengine hawamuwezi.

Aliwekeza nguvu na akili zake zote kwa mwendazake. Alimtumainia, alimuabudu na kumsujudu. Lema aliwahi kumwambia huyo unayemtegemea si Mungu. Ipo siku hatakuwepo na utakosa mtetezi. Sabaya akacheka kwa dharau. Leo yametimia yale aliyosema Lema miaka mitatu iliyopita.

Sabaya anatuhumiwa kumteka na kumpiga mtia nia wa udiwani huko Machame. Anatuhumiwa kunyanyasa wananchi mbalimbali kwa sababu za kisiasa. Anatuhumiwa kumpiga ngumi na kumpasua uso mfanyabiashara (Shoo) wa Bomang'ombe baada ya kumkuta akiuza vileo kwenye duka la bidhaa za rejareja.

Sabaya alitengeneza kikundi cha "mabaunsa" ambacho kilikua kinatembea nae popote. Hawakua walinzi rasmi wa serikali. Ni "wahuni" tu aliowaokota mtaani na kuwapa silaha, kama alivyofanya(ga) Bashite.

Kikundi hiki kilikua hakina tofauti na "Mungiki" maana kilitii kila order ya boss wao, hata ambazo ni unlawful. Kiliteka, kilijeruhi na kiliharibu mali kwa order ya Sabaya. Kikundi hiki kiliwahi kuteka moja ya magari ya Freeman Mbowe (likiwa imepaki Arusha) na kutia chumvi kwenye engine. Pamoja na Mbowe kuripoti polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Kitendo cha Sabaya kuokota vijana mtaani wasio na mafunzo yoyote ya kijeshi na kuwapa silaha wamlinde ni kosa kisheria. Lakini nani wa kuhoji kama mwendazake alibariki hilo?

Kikundi hiki kimewahi kumpiga mfanyabiashara mmoja (Molel) pub moja maeneo ya Kijenge. Vijana wa Sabaya walimzingira na kumtuhumu kumshika "makalio" mpenzi wa mmoja wao. Wakampiga na kumlazimishwa kutoa kiasi cha pesa ili wamwachie. Kitendo hicho kiliharibu biashara ya eneo hilo, hadi sasa pamepoa licha ya kwamba ni eneo zuri la starehe.

INAENDELEA, SOMA PART 4
 
PART 4

February 09, 2021 Sabaya na genge lake walienda Arusha kumvamia Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la mapazia la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu. Wakamwambia "tuna taarifa unafanya biashara ya kubadili pesa za kigeni kinyume cha sheria" Asaad akakataa.

Anadai Sabaya alimtaka atoe 100M ili asipewe kesi ya uhujumu uchumi. Lakini akamwambia wewe ni DC wa Hai unapata wapi mamlaka ya kuja kunihoji Arusha? Sabaya kusikia hivyo akaagiza milango ifungwe, wakampiga na kumtaka aoneshe pesa zilipo. Wananchi kusikia kilio wakampigia simu Diwani wa Sombetini Bakari Msangi. Alipofika na kuhoji akaunganishwa kwenye kipigo.

Kwa kifupi Sabaya alimiliki kikundi cha kigaidi. Na alikua anaenda nacho popote, iwe ofisini au night club. Hata juzi Dar alikua nacho, akizunguka nacho sehemu mbalimbali.

Mimi ni "survivor" wa kikundi hicho. November mwaka jana nilisema kitendo cha Sabaya kutumia plate number za UN kufanya uhalifu ni doa kubwa kidiplomasia. Akanipigia simu, sikupokea. Akaniandikia 'sms' ya vitisho. Akaniambia akinikamata nitajuta kuongelea vitu nisivyovijua. Sikumjibu lakini nikascreenshot na kumtumia rafiki yangu mmoja ambaye ni kiongozi serikalini just for reference likitokea lolote.

December 26 nikiwa na Don J Mbowe mahali flani Moshi, tukifurahia sikukuu za mwisho wa mwaka, tukaondoka saa 7 usiku. Kesho yake Meneja wa eneo hilo akanipigia simu akasema tulipoondoka tulimuachia balaa kubwa. Sabaya alifika na kikundi chake na kutuulizia. Alipoambiwa tumeondoka, hakuamini.

Akachomoa bastola na kufyatua hewani. Akaleta taharuki, watu wakatawanyika. Hakujali kuharibu biashara, alichojali ni kutimiza matakwa yake. Mabaunsa wakapekua counter hadi vyooni. Hatukuwepo.

Sijui wangetukuta ingekuaje. Pengine tungepigwa na kuwekewa dawa za kulevya mfukoni. Halafu kesho yake dunia ingetangaziwa kuwa tumekutwa na dawa za kulevya. Tungeshtakiwa na kunyimwa dhamana. Huenda hadi leo tungekua tunasota gerezani.

Lakini Mungu wa rehema akakumbuka watanzania tunaowarudishia(ga) tabasamu akaamua kutuokoa. Tuliondoka tukidhani tunaenda kupumzika, kumbe ilikua njia ya Mungu kutuepusha na mkono wa yule mwovu.
 
Baba yake sabaya akiwa DC serengeti alichoma nyumba za watu na kuwahamisha kwa nguvu.sabaya mtoto alishiriki kuchoma moto shule ya sekondari Ikizu mambo ufuata mkondo
 
Huyu jamaa kiufupi na bila kuficha ni moja kati ya mashetani wakubwa kuwahi kutokea nchi hii
Katesa watu sana, kaandaa magenge yake ya uporaji na unyanganyi na kufanya ubabe usio na maana Arusha na Moshi.
Walinzi wa mbowe walibambikiwa kesi za ugaidi na uhujumu uchumi, hadi leo wanaozea gerezani, kwa kifupi huyu mtu alitakiwa apelekwe mahakamani na ahukumiwe haraka sana
Habari ya kujificha kwenye uzalendo wa kutetea chama huku ukiumiza watu wasiokua na hatia nayo ni ushamba wa huyu dogo,
 
Bila shaka mama keshaliona tunaomba Mungu adhabu ziwe hukuhuku duniani.
Mbona tunamtwisha mizigo , iwe midogo au mikubwa, yote ni kwa Mheshimiwa Rais wakati kuna viongozi na watendaji wengi wanaotakiwa kufuatilia haya hasa kama ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom