Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Sabaya amesimamishwa kazi sababu ya tuhuma. Na wanaofurahia kusimamishwa kwake kazi ni wanachama wa CHADEMA. Watu wenye upeo wa kufikiri tunajiuliza maswali mengi na machache kati ya hayo ni haya :
1- tuhuma zinazomkabili Sabaya sio za leo wala jana, ni tuhuma za kuanzia mwaka jana kurudi nyuma. Sasa je, wakati Sabaya anatuhumiwa, huyu Madam SSH yeye hakuwa Makamu wa Rais? Alichukua hatua zipi dhidi ya Sabaya kwa nafasi aliyokuwa nayo?
2- Madam SSH akisema kipindi hicho hakuwa na sauti, Je, sasa hivi akiwa kama Rais yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya kila tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa viongozi au Serikali anayoiongoza sasa hivi?
Hata chama chake CCM kinatuhumiwa sana kwa udanganyifu na wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Je, Madam SSH yuko tayari kufanyia kazi hizo tuhuma kwa kuruhusu uchunguzi huru dhidi ya chama chake na ikiwa itathibitika kuwa kweli waliiba kura, Je, atakuwa tayari kujiuzulu na kupisha uchaguzi mwingine ufanyike?
3- Spika wa Bunge, Job Ndugai anatuhumiwa sana kuisigina katiba ya nchi, Je, Madam SSH yuko tayari kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine maana mamlaka hayo anayo.
4- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatuhumiwa kudhulumu haki za kuishi za baadhi ya watu, Je, Madam SSH yupo tayari kupisha uchunguzi huru dhidi ya Makonda?
5- Usalama wa Taifa wanatuhumiwa kuhusika na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu, Je, Madam SSH yupo tayari kuruhu FBI wafanye uchunguzi wao kama walivyotaka kufanya baada ya tukio na kuzuiliwa?
Ikiwa Madam anasikiliza tuhuma za mitandaoni, Je, sio sahihi kwa yeye kusikiliza na kuchukua maamuzi dhidi ya tuhuma hizo nilizoziainisha hapo juu??

Na hapo sijataja tuhuma za utekaji watu, kupotea kwa baadhi ya watu kama Azory n.k.
Au Watanzania mnapenda sana kushabikia vitu pasipo kufikiri kwa kina? Hamjui kwamba wanasiasa wote wamejaa unafiki?
Madam SSH yeye siyo MALAIKA, yeye ni Mwanadamu tena mwanasiasa. Hana tofauti na aina za wanasiasa tuwajuao.
Kwa hiyo wewe hujapenda sabaya kusimamishwa?
 
Kwani wakaskazini wao wanasemaje?
Hawasemi wanasema tu ni jambazi, ila katika kusearch kwa mtandao nadhani sababu kubwa alikuwa mkali sana kwa walionacho uko kaskazini, katika mambo mbalimbali..alisema kuna watu walinyang’anywa mashamba na wengine walikuwa hawalipi....so ile aggressiveness yake ilileta shida kidogo...
 
Hivi huyu kuku anajiamini nini au ni maneno ya mkosaji?
FB_IMG_1620935064377.jpg
 
Mheshimiwa Rais ungekuwa mtu wa kawaida ningekualika nyumbani kwangu uje tu kuweka Baraka. Huyu mama ni Mungu alimleta kutukomboa Watanzania. Taifa lilikuwa linageuzwa kisiwa cha mateso makubwa, kisiwa cha Mungu watu wachache, kisiwa cha Udikteta ambao mfano wake DUNIANI hakuna. Mama Mungu akupe maisha mrefu na afya, akupe nguvu ya kuendelea kuwaongoza watanzania.

Eti huyo kijana mwenye kibri atathubuti kumlinganisha Mh. Samia na Magufuli? Alikosea mno maana hizo ni tawala mbili tofauti kama mbingu na Ardhi. Tena akithubutu kabisa kufananisha Our Intelligent and understanding President na huyo mtu.

Rest in Peace Ole Sabaya.

Leta Mvinyo. Cheers
 
Inaonekana kama hauridhishwi vile na maamuzi ya Mheshimiwa Rais.
Sijarishishwa kabisa. Sabaya ameonewa. Wenye tuhuma kama za kwake za mitandaoni ni wengi kwa waliokuwa viongozi awamu ya 5. Sabaya atendewe haki. Tuhuma zinazoelekezwa kwake zipo nyingi kwa watu mbali mbali toka JPM aingie madarakani. Ameonewa ameonewa ameonewaaa.
 
Yaani huyu mama anajua kumalizia sikukuu yangu vizuri kweli, hela sina Ila napata raha tu.

Walikuja kumsafisha humu tukawaambia katika mambo aliyobugi ni kufanya ile interview ya clouds, pale amemchokonoa pweza aisee. Mama akikaa kimya anatafuta namna ya kumuondoa kimya Ila amemlazimisha mama amuondoe kwa kashfa akazijibu.

Meaning ameshtakiwa kiuongozi aisee hii sio kutenguliwa amefukuzwa kwa kashfa. Ameharibu CV.

Sasa waliokuwa wanamtetea wakamsaidie kujibu tuhuma. Kenge wakubwa
Mkuu hata ukiwa huna kumi mfukoni lakini FURAHA ipo ni poa tu. Yaani Mimi sijawahi kupata FURAHA kama niliyo nayo kwa sasa. Mwaka 2021 Mungu alituonekania haswa. Maanguko ya Munguwatu🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom