Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Sijarishishwa kabisa. Sabaya ameonewa. Wenye tuhuma kama za kwake za mitandaoni ni wengi kwa waliokuwa viongozi awamu ya 5. Sabaya atendewe haki. Tuhuma zinazoelekezwa kwake zipo nyingi kwa watu mbali mbali toka JPM aingie madarakani. Ameonewa ameonewa ameonewaaa.
Bado Ndugai
 
Sijarishishwa kabisa. Sabaya ameonewa. Wenye tuhuma kama za kwake za mitandaoni ni wengi kwa waliokuwa viongozi awamu ya 5. Sabaya atendewe haki. Tuhuma zinazoelekezwa kwake zipo nyingi kwa watu mbali mbali toka JPM aingie madarakani. Ameonewa ameonewa ameonewaaa.
Subiri kuna safu inakuja ya wakuu wa mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na wengine. Hutawasikia wa aina ya Sabaya. Na leo tumbuliwa ya Sabaya ni wametumiwa Habari kwa Njia ya upepo. Huko walipo wakiamka kesho watakuwa wapole kama wamemwagiwa maji ila haisaidii maana mafaili yao hawawezi badilisha huko kitu.

Mwisho wa Mungu watu ndiyo huu.

Long Live our Excellency SSH.
 
Baada ya kumfyatua Sabaya,sasa ni zamu ya wakuu wa wilaya wenye mabega marefu,afuate Yule Kitwala Komanya wa Tabora Mjini, hana tofauti na Sabaya kagombana na kila mtu na haelewani na katibu Tawala mkoa.

Halafu yule DC wa Kilolo nae ni kero kwa watumishi na wananchi.

Halafu DC wa Gairo
 
watu hai sijui wanasemaje
 
Huyu anahitaji uchunguzi gani?
Alitakiwa awe nyuma ya nondo huyu.
 
Sabaya hayupo peke yake, hasa kama issue ni aina ya uongozi wa viongozi wengi DCs na RCs wa awamu ya 5. Kusiwepo na dano standadis katika kuwajibishana.
 
Tukio lake la mwisho alilofanya Arusha akiwa DC Hai kupora dukani, kupiga wafanyakazi wa duka, kumpiga Diwani ambaye ni mwanaCCM mwenzake ndilo lililopigilia msumari wa mwisho katika jeneza lake. Hata kama ulihitajika ushindi dhidi ya Mbowe Hai, ilikuwa kosa kubwa sana kuwa na DC kama huyo ambaye alitumia harakati hizo kujinufaisha binafsi na kuletea watu mateso makubwa, ieleweke na kwa vyovyote vile kuwa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Arusha ilishafanya kazi yake na kukabidhi mamlaka. Sabaya hasingiziwi tuhuma yoyote, ndiyo matendo yake na kamwe hataweza kubadilika. Mama anafuata sheria hataki kuonea mtu, tuache mkondo uchukue nafasi yake.
 
Mwataka niwatolee nani Idd hii,,
Watu wale wakajibu "twamtaka sabaya"
🤣🤣🤣🤣🤣 yaani leo hii thread napita na kusoma kila post. Silali nakwambia. Ni burudani tosha. Hata kuku wa Eid siyo mtamu kama habari ya leo. Ni tamu haswaaa. Leta Mvinyo😍😍😍
 
Back
Top Bottom