Tukio lake la mwisho alilofanya Arusha akiwa DC Hai kupora dukani, kupiga wafanyakazi wa duka, kumpiga Diwani ambaye ni mwanaCCM mwenzake ndilo lililopigilia msumari wa mwisho katika jeneza lake. Hata kama ulihitajika ushindi dhidi ya Mbowe Hai, ilikuwa kosa kubwa sana kuwa na DC kama huyo ambaye alitumia harakati hizo kujinufaisha binafsi na kuletea watu mateso makubwa, ieleweke na kwa vyovyote vile kuwa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Arusha ilishafanya kazi yake na kukabidhi mamlaka. Sabaya hasingiziwi tuhuma yoyote, ndiyo matendo yake na kamwe hataweza kubadilika. Mama anafuata sheria hataki kuonea mtu, tuache mkondo uchukue nafasi yake.