Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Balozi hana umuhimu sana kwenye ujasusi pale embassy, hana umuhimu kuliko attachƩ wa intelligence services. Vilevile Balozi hana umuhimu kuliko military attachƩ kwenye mambo ya kijeshi pale ubalozini.

Balozi ni kioo, kila anapokwenda na anachofanya anajulikana kwenye hiyo nchi. Huwezi mkuta anapambana kukusanya data za siri au anasimamia kufanya recruitments za mole, double agent wala nini, wanakwepa kumpa majukumu hatarishi na ya kutia doa diplomasia ya nchi endapo atakamatwa au kujulikana. Hata Diwani au huyu Said uwape ubalozi kwa nchi zinazojielewa hawatishiki kwa lolote.

Mara kibao nchi zinafukuza wanadiplomasia wanausalama na zinawaacha mabalozi wao. Anaweza teuliwa daktari wa mifugo na ujasusi ukapigwa kuliko maelezo.
Hii ndiyo sababu mtu kama Dr. Augustine Mahiga alivyotoka Tanzania alizungushwa sana kufanya kazi maalum kwenye balozi za Tanzania na UN kabla ya kupewa ubalozi mwaka 2003 na Mkapa.

Nilikuwa najiuliza sana kwa nini Dr. Mahiga hawajampa ubalozi miaka yote ile?

Nikaja kugundua angepewa ubalozi mapema angekuwa na profile kubwa sana kazi nyingine nyeti asingeweza kufanya.
 
Sensa ya 2023 watanzania ni milioni 61.....2012 ilikuwa milioni 48....juu ya soko huria na adabu mbovu inayohusisha kulegalega kwa uzalendo kwa taifa na kwa raia wenyewe....mabadiliko hayasha gazi.....
Kwa rate hii, sensa inayokuja mnamo 2032 tutagonga angalau milioni 75.

Baada ya hapo next stop 2042 angalau milioni 95.

Na hayo ni makadirio ya chini kabisa.
 
Zile ndio nchi zenye mifumo. Mkurugenzi anateuliwa na Rais na anapitishwa na Bunge, Senator yeyote anaweza weka pingamizi na evidence juu ya uhalali, uaminifu, elimu, uwezo, uzalendo wa huyo mtu na akakataliwa. Hivyo Rais anaumiza kichwa kuteua sio kuchagua machawa. Mpaka sasa Joint Chiefs of Staff wa Marekani hawajatimia sababu kuna pingamizi.
Rais akitaka kufukuza Jenerali jeshini mpaka hilo jopo likubali na kesi juu ya mfukuzwa.

Hakuna mambo ya kubadilishwa kitengo. Ukikosea ni kesi kama ni jinai kisheria hamna mambo ya kusamehewa sijui kujitafakari.
Upo sahihi
 
Nchi yoyote inao uwezo wa kumkataa balozi au mwanadiplomasia. Au akiwepo ubalozini inaweza kumfanya persona non grata au ikampa masaa kadhaa awe ameondoka.

Huyo jamaa atasema ni woga wakati sio
na hii inatokana na pale wamegundua mienendo fulani ya kutiliwa mashaka
 
Pongezi nyingi kwake kwa kuaminiwa.
Jambo la msingi asimwangushe Rais, atimize matarajio ya Rais na Taifa kwa ujumla.
Uzalendo, umahiri, umakini na weledi wa Hali ya juu ni muhimu sana kufanikisha.
 
Huyu Mzee ni Jasusi wa TISS, alopelekwa na Mzee wa Msoga kule Rwanda .


Utendaji wake mbovu ,ndio ulipelekea kudhorota Kwa uhusiano wa Rwanda na Tanzania, kiasi Cha Marais wawili kutupiana Vijembe.



Itoshe tu kusema, DPW wameamua na Rwanda Imeamua !!.
 
Huyu Mzee ni Jasusi wa TISS, alopelekwa na Mzee wa Msoga kule Rwanda .


Utendaji wake mbovu ,ndio ulipelekea kudhorota Kwa uhusiano wa Rwanda na Tanzania, kiasi Cha Marais wawili kutupiana Vijembe.



Itoshe tu kusema, DPW wameamua na Rwanda Imeamua !!.

Mkuu unamsema Massoro au Siwa?
 
Huyu Mzee ni Jasusi wa TISS, alopelekwa na Mzee wa Msoga kule Rwanda .


Utendaji wake mbovu ,ndio ulipelekea kudhorota Kwa uhusiano wa Rwanda na Tanzania, kiasi Cha Marais wawili kutupiana Vijembe.



Itoshe tu kusema, DPW wameamua na Rwanda Imeamua !!.

anayechukuwa bandari zetu kibabe ni rwanda hakuna cha mwarabu wala babake mwarabu, real Emirate UAE hawezi kupoteza muda wake na kijbandari cha dar ukichukulia kwamba wananchi hawataki, mali zimeenda kibabe hiyo inaunganishwa na mzigo unaoporwa kongo kibabe kupitishiwa kwetu ambapo hatumiliki tena bandari hivyo kila senti itakayolipwa kwa kusafirishia mzigo wa kongo inaenda kibabe pia kwa mbabe.

ukitakata kujua ni utapeli na uharamia ingia website ya DPWorld hakuna neno tanzania popote pale kwa nini kama wanakuja kufanya uwekezaji mkubwa kiasi hicho? mbona kwingine kote wametaja nchi walizowekeza au wanazotarajia kuwekeza ?
 
Back
Top Bottom