Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Hii ndiyo sababu mtu kama Dr. Augustine Mahiga alivyotoka Tanzania alizungushwa sana kufanya kazi maalum kwenye balozi za Tanzania na UN kabla ya kupewa ubalozi mwaka 2003 na Mkapa.

Nilikuwa najiuliza sana kwa nini Dr. Mahiga hawajampa ubalozi miaka yote ile?

Nikaja kugundua angepewa ubalozi mapema angekuwa na profile kubwa sana kazi nyingine nyeti asingeweza kufanya.
 
Sensa ya 2023 watanzania ni milioni 61.....2012 ilikuwa milioni 48....juu ya soko huria na adabu mbovu inayohusisha kulegalega kwa uzalendo kwa taifa na kwa raia wenyewe....mabadiliko hayasha gazi.....
Kwa rate hii, sensa inayokuja mnamo 2032 tutagonga angalau milioni 75.

Baada ya hapo next stop 2042 angalau milioni 95.

Na hayo ni makadirio ya chini kabisa.
 
Upo sahihi
 
Nchi yoyote inao uwezo wa kumkataa balozi au mwanadiplomasia. Au akiwepo ubalozini inaweza kumfanya persona non grata au ikampa masaa kadhaa awe ameondoka.

Huyo jamaa atasema ni woga wakati sio
na hii inatokana na pale wamegundua mienendo fulani ya kutiliwa mashaka
 
Pongezi nyingi kwake kwa kuaminiwa.
Jambo la msingi asimwangushe Rais, atimize matarajio ya Rais na Taifa kwa ujumla.
Uzalendo, umahiri, umakini na weledi wa Hali ya juu ni muhimu sana kufanikisha.
 
Huyu Mzee ni Jasusi wa TISS, alopelekwa na Mzee wa Msoga kule Rwanda .


Utendaji wake mbovu ,ndio ulipelekea kudhorota Kwa uhusiano wa Rwanda na Tanzania, kiasi Cha Marais wawili kutupiana Vijembe.



Itoshe tu kusema, DPW wameamua na Rwanda Imeamua !!.
 

Mkuu unamsema Massoro au Siwa?
 

anayechukuwa bandari zetu kibabe ni rwanda hakuna cha mwarabu wala babake mwarabu, real Emirate UAE hawezi kupoteza muda wake na kijbandari cha dar ukichukulia kwamba wananchi hawataki, mali zimeenda kibabe hiyo inaunganishwa na mzigo unaoporwa kongo kibabe kupitishiwa kwetu ambapo hatumiliki tena bandari hivyo kila senti itakayolipwa kwa kusafirishia mzigo wa kongo inaenda kibabe pia kwa mbabe.

ukitakata kujua ni utapeli na uharamia ingia website ya DPWorld hakuna neno tanzania popote pale kwa nini kama wanakuja kufanya uwekezaji mkubwa kiasi hicho? mbona kwingine kote wametaja nchi walizowekeza au wanazotarajia kuwekeza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…