Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).
Rais Samia, pia amemteua Joyce Gideon Mapunjo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) akichukua nafasi ya Mhandisi Musa lyombe ambaye amemaliza muda wake.
Taarifa ya uteuzi wa huo imetolewa leo Jumatatu Desemba 2, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.