Rais Samia amteua Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)

Kusimamishwa sio shida inawezekana uchunguzi umefanyika ikabainika hakuhusika ,hongera sana Raymond Mungu akubariki
 
CAG hatafuti sifa za kijinga kama unavyodai,bali anafanya kazi professionally kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya ukaguzi(International Standards of Auditing) hivyo kazi yake ni ku-Audit,Kutoa Taarifa na kutoa Reccomendation.Kwenye Report husika CAG karipoti kuwa Deni la MSD limefikia 382 Bln na akashauri lilipwe ili kulinda Mtaji wa MSD,hapo CAG kishafanya kazi yake,Utekelezaji(Implimentantion) inabaki kuwa Taasisi Husika Chini ya Serikali.Hsta hivyo,Kuidai serikali siyo Justification ya MSD kuvunja taratibu xa manunuzi ya Umma(Public Ptocutement) kama kulipa suppliers bila contracts, kununua madawa bila ku-involve PMU wala TenderBoard ya MSD,kununua dawa overseas za 17Bln kwa Mikataba ambayo haikufanyiwa vetting na AG?,n.k,ambavyo vimechangia kula kichwa cha Mjeshi Maj.General Mhidze

 
Nimekuelewa baadhi ya categories, nililenga lile kasambaza dawa 34% hii iko proportion na approved budget, je zilipelekwa fedha hizo za kununua dawa. Note: Kama una madeni kwa washitiri huwa nao ni wajanja ukimpa tenda nyingine anachukua anafanya partial delivery hadi ulipe lile . Hivyo mbinu jinsi ya kupata dawa zitumike. Maana ukitenda wanajitokeza hao hao wanakudai. Hivyo kuwe na ustaarabu wa serikali kulipa deni la msd na kutekeleza bajeti ya dawa Kama ilivyopitishwa bungeni na msd ilipe washitiri iliowakopa
 
Hizi nafasi ilipaswa ziwe za ushindani na kuwe kuna open platorm hadi tupate shortlisted candidates kwa uwazi ila kwa katiba hii kila siku itakua okota okota tu na panga pangua..
 
Ipo kila sababu hizi nafasi za juu wawe wanaomba badala ya teuzi zenye malengo ya maslahi binafsi
 


Chaguo zuri my schoolmate Ilboru Sec School. Tatizo kubwa pale ni siasa
 
Hongera Le super chief Hangaya. Teuzi hizi mbili za MSD ni nzuri sema funding iwe kwa wakati na wanachokihitaji.

Alipelekwa Mgaya pale jamaa katoka marekani lakini hakuweza kuperform wakati wa kikwete.

Siasa naona kidogo wakati huu zinaweza kupungua juu ya menejimenti. Kupewa amri za wanasiasa.
 
MSD wizi haujaanza leo na wala hautoisha leo. Wizi wa MSD ni mnyororo mrefu sana unaoanzia huko MSD kuja kwenye Halmashauri mpaka kwa Waganga wakuu wa Hospitali na Maafisa Ugavi wao... Manunuzi mengi yanayofanyika MSD yana wizi ndani yake.

Kitambo kile kabla ya hela kuingizwa kwenye mfumo wa manunuzi kidijitali ilikuwa Hospitali inaenda kufanya manunuzi MSD wa dawa mfano za Milioni 100, lakini dawa zinazoletwa ni za Milioni 50 halafu hiyo Milioni 50 watu wanagawana,,, Zinaletwa mashine ambazo ni za bei za chini na zingine unaziona kabisa hizi hazitokaa hata miezi 6 halafu Waganga Wakuu na viongozi wenzake, Afisa Ugavi, Makatibu na huko Halmashauri wanapandisha bei hata mara 10 ya uhalisia na nyiye watumiaji mnalazimishwa msaini madokezo.
 
Siku hizi barua za uteuzi zinasainiwa hotelini. Haya mama endelea kuupiga mwingi.
Zama zimebadilika sana , hizi ni enzi za E government, , mtu anaweza kufanya mkutano na wakirugenzi kadhaa akiwa mbali kabisa na ofisi alimradi tu kuna internet.
 
Akitaka kufanikiwa wale wakurugenzi wote wa idara aombe kibali wapangiwe Kazi nyingne... Otherwise Bado atanyoshwa tu Kama mwenzake na watu wanaojiita wazoefu wa kaz
 
Wazee was kufukua makaburi fukueni la HUYU mtu tuone yake au hayapo ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…