Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Bw. James Wilbert Kaji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kaji alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu