Rais Samia amteua Wilbert Haji kuwa Mkurugenzi wa NIDA

Rais Samia amteua Wilbert Haji kuwa Mkurugenzi wa NIDA

Sijajua shida ya NiDA ni.siasa au.bajeti au.weledi. Niliamini.sana Dickson Maimu angeliweza kumalizia kazi.aliyoianza.

Nida inahitaji au.inabidi iwe na.team.ya.watu.wa.ICT waliobobea sana.

Hongera Kachero mbobezi JK. Nenda kabadilishe nida iwe na.matumizi kama ilivyokusudiwa kama marekani social security card na wakupe bajetiya.kutosha sio vitambulisho mara vinafutika.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Bw. James Wilbert Kaji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kaji alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Sharifa B. Nyanga

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

"Rais Samia amteua Wilbert Haji kuwa Mkurugenzi wa NIDA" moderator badilisheni heading inaitwa Kaji sio Haji. Jamaa alikuwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kbl ya kushika nyazifa za kisiasa Tanga na Kilimanjaro, Alipambana vema sana akiwa DCEA. sijui ni kwa nini walimuondoa na kumweka kando kbs enzi za Magu!!​

 
Tuliambiwa NIDA na RITA zinaunganishwa. Bado hawajamaliza mchakato?
 
Back
Top Bottom