Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Ile haikuwa awamu ya Wakristo. Ilikuwa awamu ya Wasukuma ambao hawakuwa Waislamu ila walikuwa Wakristo. Acha watu waseme ukweli wao wa moyoni. Na zote ni serikali za CCM. Na hata wakati wa Magufuli tulipigia kelele kuhusu teuzi za akina Maduhu, Masanja, Maganga... Usijifanye haukuwepo.
Hapa ndugu unakosea sana...mbona hao waislam wakati wa Magufuli akifanya teuzi walikuwa hawasemi kuwa mwaka wa wakristo huu! Usitake niamini "the lights are on,but nobody is home!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea.

Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba.

Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua


======

Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.

Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Mambo ya vilemba si haba
 
Hajui kiingereza fasaha

Huwezi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais halafu lugha haipandi, Hatoshi tu

Ataenda kuwa RAS simiyu kunamtosha
si kweli lugha anaijua sana kasoma HGL Ilboru secondary kule Ilboru hawapelekwi vilaza acha uongo.walikuwa na Ayubu Lyoba enzi hizooo.kipindi hicho walikuwa wanasoma watu cream hivyo usipotoshe watu humu umlaumu kwa jingine na si lugha ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom