Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupangiwa kazi nyingine

Mimi ni mkristo ila Bora Waislam wawe wengi Wana utu kuliko wagalatia,roho mbaya sana hawana adabu wala heshima japo ya dini.
Me pia mkristo,lakini Bora wakiongoza Waislamu huwa Wanakuwa na utu Sana kuliko wakristo, we angalia kwetu mbeya,makanisa mengi,lakini kunaongoza kwa uchawi na mahuaji ya hovyo,mikoa yote yenye wakristo wengi ni hatari
 
Hivi Mashangazi wa twitter Hawana au taarifa za Shangazi mwenzao kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Suluhu
 
Jaffari mbona yeye ametenguliwa wakati Rais alisema yeye afukuzi anakurekebisha tuu? Jaffari yeye mbona katenguliwa jamani? Amekosea wapi kuliko wengine?
 
We kubali udini upo na ukanda upo,awamu ya tano tuliyaona hayo,hii awamu ya sita dalili pia zinaonyesha the same
awamu ya tano ulikuwa unaweza kwenda kkwenye mkutano sehemu fulani ukahutubia kilugha. ajabu sana. mfano, mtu unaenda Mwanza, ambako kumejaa makabila yote (kuna wachaga, wanyakyusa, wahehe, wapare, wamakonde etc) pamoja na kwamba majority wanaweza kuwa wasukuma lakini makabila mengine yapo, kiswahili kinajulikana kwa wote, haupo kijijini upo mjini, wewe ukaanza kuongea kisukuma.
 
Mwaka wa Waislamu huu, Ndugu yangu Jaffar Haniu kakosea wapi? Sitaki kuamini kakubali kirahisi hivyo kuacha yale mapochopocho mix kuku sambusa wa ikulu.

Mwezake Msigwa tangu afutwe kazi ikulu siku hizi kapauka kweli, Ikulu ikulu tu.
Msemaj ni mtu wa karib sana wa rais...sasa jinsia mbili tofaut inakua ngum...
 
Jina tu halisemi dini ya mtu..Jafari ni jina lenye asili ya uarabuni sio lazima awe Muislam...huku Pwani kuna watu wengi tu wanamajina yenye asili ya kiarabu na kupewa tafsiri ya majina ya waislam lakini wenye majina hayo ni wakristo..kumbuka aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani..huyu alikuwa hadi anapiga kinanda kanisani
kwetu kuna majina ya watu wanaitwa kina omari, rajabu lakini ni wakristo na wanakula kitimoto kwenda mbele.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amemteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu akimrithi Jaffar Haniu. Mwezi uliopita Zuhura aliaga BBC na hakusema anapoelekea.

Haniu aliyerithi kijiti kutoka kwa Gerson Msigwa Juni mwaka jana atapangiwa kazi nyingine akihudumu kwenye ofisi hiyo kwa miezi saba.

Wanawake oyeee, mpaka maji yaitwe mma.. Tunasubiri matokeo kutoka Dodoma japo tunayajua


======

Zuhura Yunus ni mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni BBC, Dira ya Dunia akihudumu kwenye shirika hilo kwa miaka 14. Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazao ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi wa Tanzania mwaka 2010.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania. Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti ya HIV/Aids. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen newspaper.

Mwaka jana Zuhura aliandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor, mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Zuhura katika utumishi wake amewahoji viongozi wa Afrika kama vile Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kama sehemu ya taarifa kuhusu biashara haramu ya wanyama pori pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Mahojiano aliyoyafanya na mgombea urais wa upinzani, Edward Lowassa mwaka 2015 yalizua gumzo katika vyombo vya habari nchini.

Zuhura ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, Uganda na ana shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Hii kweli ndo maana halisi ya AJIRA HAKUNA maana imekuwa ni ukoo wa Panya unaacha kazi hapa unateuliwa kule, vijana wanaotoka Vyuo Vikuu wataisoma namba sana tu.
 
Nchi yetu imeharibika sana. Hakuiharibu Samia. Samia anaendeleza tu sera za CCM. Aliyeanzisha ni yule alikuwa anateua Wasukuma wenzie na kupeleka miradi ya kimkakati ya kitaifa kijijini kwake. Huo ndio ukweli. Wala haihitaji Waislam na Wakristo kugombana.
kujenga airport ya chattle ambako kwa mwezi mzima ndege inasafiria abiria 250 tu. the whole good month.
 
awamu ya tano ulikuwa unaweza kwenda kkwenye mkutano sehemu fulani ukahutubia kilugha. ajabu sana. mfano, mtu unaenda Mwanza, ambako kumejaa makabila yote (kuna wachaga, wanyakyusa, wahehe, wapare, wamakonde etc) pamoja na kwamba majority wanaweza kuwa wasukuma lakini makabila mengine yapo, kiswahili kinajulikana kwa wote, haupo kijijini upo mjini, wewe ukaanza kuongea kisukuma.
Yule mtu alikuwa wa ajabu sana
 
Back
Top Bottom