Rais Samia amtimua Hanafi Hassan Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kisa wananchi kurudisha Kadi za CCM

Unaweza fikiri kuwa kadi za chama ni kitu cha maaaaaana!

Kumbe ni kama card ya simba na yanga tu
 
Kiongozi wa watu katika nafasi yoyote anatakiwa awe mnyenyekevu, msikivu, asie jeuri wala majivuno. Kiongozi anaye jimwambafai basi ujue hapo ni bomu
 
Hao wanaonewa tu anaacha akina makmba akina mwigulu wa kula hela kubwa kubwa anahaungaika na vidaa ,
 
She is a source of the failing state. Firing a trivial sardine and leaving behind the big fish sailing across the natural resources for a personal beneficiary is an absolute betrayal to Tanzanians. There are several specific ministers who are underperforming but no stringent action has so far been imposed against them to date.
 
Wakati mkuu wa wilaya wanahongwa RC, RSO na DSO walikuwa wapi kwanini wenyewe wabaki ofisini? Hao watumishi si ndio aliwateua yeye na kuwatoa waliokuwepo kutokana na chuki tu kwamba waliteuliwa na mtangulizi wake JPM? Alifanya mabadiliko kwa mbwembwe bila kujua zimwi likujualo halikuli likakwisha?
 
Mambo si mazuri ndani ya CCM, naona mama kawageukia watendaji wake wameanza kufukuzana - sisi tunasemajeeee--- shughuli bado mbichi bandari yetu haiuzwi kwa gharama yoyote ile.
 
Je, Kadi ni Muhimu kuliko ripoti ya CAG?

Tangu Rais Samia ameingia Madarakani,kumekuwa na taarifa nyingi sana kuhusu ufisadi mkubwa sana unaoendelea kufanywa katika taasisi na miradi mingi ya kitaifa.Ikiwa pia ni katika halmashauri za majiji,Mikoa na Wilaya.

Hii ni kutokana na ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG. Kwa miaka miwili mfululizo kama sikosei.

Sasa basi,la kushangaza ni kwamba tangu ripoti hizo za mabilioni kwa matrilioni ya upotevu wa pesa za serikali kutolewa na CAG.

Hatujawahi kumuona au kumsikia Mh Rais Samia akichukua hatua za kuwawajibisha wahusika na hatimae kuweza kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria ili hatua stahiki za kinidhamu na kijinai ziweze kuchukuliwa

Kama sikosei mara ya mwisho tulimkariri Mh Rais akiishia kusema hao ni Wezi wa mali za umma ni "Stupid"
Badae hayo yalipita na maisha yameendelea,bila kusikia kauli ya Rais kuhusiana na ubadhirifu huo.
Mpaka sasa ilipoibuka ya huko Mtwara. Ambapo limetokea tukio hili.
Kwamba.

Wananchi wamerudisha kadi za CCM kisa ni kutoridhishwa na watendaji wa serikali katika mojawapo ya wilaya mkoani humo.

Sasa ndio tumemuona mama ametoka rasmi na kuanza kuwatumbua viongozi wa kiserikali. Kama DC,DED na wengine watakaofuatia.

Sitaki kuingia kutafuta mchawi kwa huko Mtwara.

Ila najiuliza tu kwamba!

Je!
Kwa yeye Mheshimiwa Rais JMT.
Hata ma-trilioni yanayoibiwa kila uchao na huku akipewa taarifa kuanzia ukarabati wa MV Magogoni huko Mombasa Kenya, kwa thamani inayozidi bei ya kununulia kivuko chenyewe.
Na mpaka sasa yuko kimya!

Ripoti za CAG.mpaka sasa yuko kimya!

Madawa ya kulevya yaliyokamatwa Mtwara na mpaka sasa kimya!

Na sasa kashfa ya mkataba wa DP-WORLD ametamka tena kwenye
Hadhara ya waumini kanisani kwamba "amekaa kimya na ataendelea kukaa kimya"

Mambo yaliyonyamaziwa ni mengi sana mpaka sasa!

Lakini kurudishwa kadi ameshindwa kukaa kimya sababu wamegusa maslahi yake.
Sababu kurudishwa kadi ni kifo kwa CCM ambayo ndiyo mzizi na nguzo kuu kwa U- Rais wake!

Kwamba hayo mengine hayamhusu sababu wanatekeleza maelekezo ya kula urefu wa kamba yake au?

Tumueleweje Mheshimiwa Rais wetu wa JMT?

Eeh Mola Inusuru Tanzania [emoji1241] [emoji813]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…