Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
RAIS SAMIA KUMPANGIA MABEYO MAJUKUMU MAPYA
Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kumpangia majukumu mengine aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo ambaye amestaafu kulitumikia Jeshi.
Amesema hayo baada ya kumuapisha Jacob John Mkunda kuwa CDF mpya, Ikulu Dar es Salaam, leo Juni 30, 2022.
“Umefanya kazi kwa uadilifu mkubwa, nakushukuru na kukupongeza kwa kuwa si kazi rahisi, unaacha ukiwa bado kijana una nguvu, tutaendelea kukupa majukumu utusaidie. Jioni ya leo Katibu Mkuu Kiongozi utamsikia, ameshakupangia kazi ya kufanya, uendelee kulitumikia taifa lako,” - Rais Samia.
=============
RAIS SAMIA: KWENYE JESHI HAKUNA ANAYEINGIA NA YAKE
Rais wa Samia Suluhu Hassan amesema katika Jeshi hakuna mtu kuingia na yake kama ilivyo katika Serikali, ambapo ametoa wito kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jacob John Mkunda kuendeleza alipoishi mtangulizi wake, Venance Mabeyo.
Amesema hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2022 wakati akiwaapisha maofisa kadhaa wa Jeshi akiwemo CDF Mkunda.
“Kwa wote mlioapa nawapongeza na ninawatakia kazi njema, maelekezo zaidi tutazungumza ‘inbox’, mfanye kazi kama aliyetoka alivyofanya,” – Rais Samia.