Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Kwa hotuba ya leo ya Samia kama Ndugai asipojiuzulu basi hana akili timamu na anatumikia tumbo lake tu. Samia amesema wazi kuwa kilichomsukuma Ndugai kupinga mikopo ni Uchaguzi Mkuu wa 2025. Aidha amesema wale wote wanasioweza kwenda pamoja na yeye katika kuwaletea wananchi maendeleo atawaondoa katika serikali ya ili wapate muda wa kutosha kujiandaa na uchaguzi wa 2025!
Ushawai pigana na mtu ukamtwanga kwerikweri halaf akazimia..akazinduka ukaenda mwomba msamaha.hahahah
 
Mama Samia baada ya kuapishwa na alipoenda kulihutubia bunge aliwaambia wakosoe vikali. Na hili lilipongezwa na wengi kuwa huenda ukawa mwanzo mpya wa bunge kuikosoa serikali na hivyo kuacha alama.

Ila yanayotokea sasa ni kuwa mama hakubaliani na huo ukosoaji, au ilibidi wakosoe kitu gani maana kwenye hili la tozo na mikopo umekua mkali sana.

Mama rejea tena hotuba yako ya kwanza bungeni, uliwaambia mwenyewe.
 
Ndio akome alijifanya Mungu mtu nchi Kama ya kwake ananyanyasa wapinzani, wabunge wenzie na watu mbali mbali akadhani anaweza tukana Hadi level ya Raisi akawa salama...Sasa mwisho wake umefika.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
sina mahaba na ndugai wala ccm.

ila usimlaumu kwa kukurupuka kwake kuomba msamaha.

pressure kutoka ndani ya ccm ilikuwa kubwa sana na jamaa akawa hana namna. alibanwa kwenye crempu.

na ukute hata kundi lililokuwa nyuma yake lilimuacha apambane kivyake.

shida ni kwamba amemuomba msamaha mwanamke, mbaya zaidi ni mwanamke mwenye asili ya pwani. wanawake wa pwani na vichambo ni pete na kidole.

kichambo alichopewa leo sidhani kama alikitarajia. angalau leo yale maccm yenye tamaa ya kiti cha urais, yamejua rangi halisi ya mama.
Nilisema juzi,, kupambana kwa maneno na mtoto wa pwani,, ni kazi kwelikweli,,

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugai kama Spika, ka mtu binafsi, ka mbunge na kama kiongpzi ndani ya CCM, uovu wake, kama walivyo wenzake, ni mwingi, na umewaathiri sana Watanzania negatively.

Hata hivyo, hakuna mwanadamu mwenye kiapo na uovu. Kama Ndugai ameamua kujutia uovu wake na kutaka kuweka alama itakayokumbukwa katika nchi hii, asaidie kupatikana kwa misingi na mifumo bora ya kiutawala. Na hilo, hakikisho lake lipo kwenye katiba.

Kwa kuanzia, Bunge likatae unafiki wa Serikali, unaowekwa kwenye mswada wa mabadiliko ya katiba. Mswada huo ni upuuzi na kiinimacho. Bunge liukatae, na kuitaka Serikali kupeleka mswada wenye dhamira njema.

Uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwatumia wateule wa Rais kupendekeza majina ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa Rais, ni ujinga, upuuzi na kukosa hekima na uadilifu kwa waliouandaa huo mswada. Bunge liukatae, kwa sababu ni mswada wa kijinga kabisa.
Uovu wake ni upi weka tuone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama angeonyesha tu 'umama' kwa kukaa kimya kwakuwa lilishaombewa msamaha tayari.......hakukuwa na haja ya kurusha vijembe tena inakuwa km kushindana. Atake asitake ndugai ni muhimu sana kule bungeni na anaweza kumharibia.

Lkn labda mama alimaanisha huyu 'mama tanzania' (mbatia) maana nasikia nae alibwatuka kwa ukali
 
Uwiiiiiiiiiiiiiii!

Sukuma gang chaliiiiiii

Chato legacy chini!!!!!?!

Nyanengh'we!!
200 (3).gif
 
Back
Top Bottom