Ndugai kama Spika, ka mtu binafsi, ka mbunge na kama kiongpzi ndani ya CCM, uovu wake, kama walivyo wenzake, ni mwingi, na umewaathiri sana Watanzania negatively.
Hata hivyo, hakuna mwanadamu mwenye kiapo na uovu. Kama Ndugai ameamua kujutia uovu wake na kutaka kuweka alama itakayokumbukwa katika nchi hii, asaidie kupatikana kwa misingi na mifumo bora ya kiutawala. Na hilo, hakikisho lake lipo kwenye katiba.
Kwa kuanzia, Bunge likatae unafiki wa Serikali, unaowekwa kwenye mswada wa mabadiliko ya katiba. Mswada huo ni upuuzi na kiinimacho. Bunge liukatae, na kuitaka Serikali kupeleka mswada wenye dhamira njema.
Uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwatumia wateule wa Rais kupendekeza majina ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa Rais, ni ujinga, upuuzi na kukosa hekima na uadilifu kwa waliouandaa huo mswada. Bunge liukatae, kwa sababu ni mswada wa kijinga kabisa.