Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Huu mchezo wa viongoziwa serkali kutishia kuulizwa, unaenda kulifanya bunge kuwa mfu. Toeni bunge linakula hela zetu tu, maana ni bunge la Ndioooooo
 
Kwel kabisa
 
Kwa kuwa mama kakorofishwa Ndugai aachie ngazi, angekuwa mwanaume labda angeendelea kukaza kuongoza Bunge, ila si kwa vijembe hivyo, na sasa wataendelea hadi mwenyewe ajichukie!
Mwanamke wa pwani sio wa kuanzisha ugomvi nae😅
 
Kwani kukopa ni dhambi kikubwa Hi yo mikopo itumike vizuri sio unakopa trion 1.3 unakula trion 1 then 0.3 ndo inatumika kwenye Miradi ya maendeleo rubbish..then job hakukosea kuhoji kwasabbu yeye ni muhimili kamili na ndo kazi ya huo muhimili labda kwa sababu ya utamaduni mbovu tulionao Rais Ana influence kupatikana kwa spika ndo maana tumezoea kuona spika anamsupport rais but haitakiwi iwe ivo ndo maana katiba mpya inatakiwa ili rais asione ameonewa kuhojiwa na spika kuhusu mambo mbalimbali
 
Kwakweli baada ya kuomba msamaha sikutegemea mtu mwingine aje na hii hii agenda...Huu si uungwana...Kama mtu kakosea na ameliona kosa lake ni busara kumwelewa na kusonga mbele
 
Kwakweli baada ya kuomba msamaha sikutegemea mtu mwingine aje na hii hii agenda...Huu si uungwana...Kama mtu kakosea na ameliona kosa lake ni busara kumwelewa na kusonga mbele

Kwani alifanya Kosa gani hadi akaenda kuomba MSAMAHA ?

Kusema kwamba mikopo haina tija ni hoja ya Msingi , tumekopa na tozo juu , means Mama ni failure na amekosa njia Mbadala ya kuongeza pato , hiyo ndiyo hoja ya bwana mdogo ndugai na ni hoja yenye mantiki.

Kitendo cha kuomba radhi ni utii wa kukosa uanaume

The boy is soft na ameprove he is cowardly
 

Leo nadhani ata kahawa hapo nyumbani kwake haipiti. Hiki kitamtafuna siku zote ameonekana ni dhaifu zaidi
 
Kuhoji si tatizo lakini si kwenye majukwaa ya siasa, wangefanya hayo bungeni what could have been a problem? Waziri wa fedha angebanwa na hata kama kulikuwa na shida angetakiwa yeye kuwajibika. Sasa kinachoendelea Mungu mwenyewe atusaidie, haijulikani who is who!
 
Rais ni mwenyekiti wa chama atawatuma wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani nae,,,spika ni mtu mdogo sana kwa nchi yetu

Na bunge linaweza kupiga kura kutokua na imani na serikali unyama unyamani
 
Kwa kuwa mama kakorofishwa Ndugai aachie ngazi, angekuwa mwanaume labda angeendelea kukaza kuongoza Bunge, ila si kwa vijembe hivyo, na sasa wataendelea hadi mwenyewe ajichukie!
Wale wajumbe walisimama na kumwimbia mama siju huko pia ni kumzomea spika na je, wabunge wasimama wapi
 
Kosa kubwa alilofanya mgogo ni kuomba msamaha, maneno ukishayatamka hayawezi kurudi mdomani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…