Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Sasa labda na hio return on investment its about time to rethink our strategy...., Huyu Mama Kuendelea kushikia Bango hii issue inamfanya kuonekana petty..... Ingawa sio mbaya kujibu hoja (ila hoja hujibiwa kwa hoja na sio vioja)
Amemjibu kwa hoja labda kama wewe hukuelewa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mwanzoni kabisa niliwasikia watu wakisema bunge ni dhaifu.


Spika kaongea kidogo tu watu wamemvaa tena.


Kwahiyo mnataka nini??


Halafu suala la Rais wa nchi kuendelea na hili suala la mikopo ni ufinyu wa akili.

Mtu ameshaomba radhi.

Yeye bado kashikilia bango.

Poor thinking capacity.
 
Serikali yake ituambie pesa za makusanyo ya tozo zinakwenda wapi mbona siku hizi hakuna update zozote?

Kwenye hii issue yake na Ndugai kwangu Ndugai ndie mshindi, yeye anafurahia ushindi anaodhani ameupata kwasababu tu kuna kundi kubwa la wanafiki nyuma yake wanaojali matumbo yao wako upande wake kwasababu ya mamlaka aliyonayo kama mkuu wa nchi, lakini hajashinda kwa nguvu ya hoja.
 
Sio lazima spika wa bunge awe kibaraka wa rais.
Nchi inaweza kusonga mbele vizuri kama bunge likiacha urafiki na serikali.
 
Alichosema Ndugai karibuni. Hakina tofauti na alichosema baada ya kifo cha Magufuli kwamba awamu iliyopita ilikuwa ya ajabu sana!!

Saa nyingine anaongea kama mtu aliyestuka kutoka usingizini. Awamu ya 5 walikopa bilioni 29 lakini hakuwai kusema chochote kuhusu nchi kupigwa mdana. Leo anakuja ku argue trilioni 1.3!!

Sisema kama mtu akupinga kitu fulani awamu iliyopita basi haruhusiwi kupinga awamu hii..no! Lakini anatakiwa atolee maelezo kwa nini anamtazamo tofauti sasa hivi ukilinganisha na awamu iliyopita. Sio cheap kama alivyosema yeye. Afadhali ata na Polepole anajenga hoja!!
 
Moja Kuhoji sio Kutikisa nchi au kutaka kuitikisa...

Pili jambo kama hilo haliwezi kufanywa kwenye nchi ambayo ni Banana Republic lakini nchi inayojitambua mtu yoyote ruksa kuhoji au kusema anachodhani hakipo sawa na Bunge / Mbunge let alone Speaker anayo mandate ya kutoa mawazo yake yeye kama part ya muhimili unayoshauri / kuisimamia serikali (ingawa Bunge limeshakuwa kama rubber stamp huenda ndio maana watu wanashangaa linapojaribu kubadilika)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…