Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Kwa Hakika mh Rais amefanya jambo lililokonga na kukosha mioyo ya watanzania,Ameziteka nyoyo za watanzania ndani ya muda mfupi sana,amefanya jambo la kipekee ,la kijasiri na kishujaa sanaa. Niliandika humu kuwa Dr Slaa Hastahili Kuendelea kuwa kupewa heshima ya ubalozi.hakustahili kabisa kuwa nawadhifa huo mpaka muda huo. Safi sana Mh Rais,hongera sana mama yangu kwa hatua hii ya kishujaa na kijasiri inayoendelea kuungwa mkono na wengi.
 
Kwa Hakika mh Rais amefanya jambo lililokonga na kukosha mioyo ya watanzania,Ameziteka nyoyo za watanzania ndani ya muda mfupi sana,amefanya jambo la kipekee ,la kijasiri na kishujaa sanaa. Niliandika humu kuwa Dr Slaa Hastahili Kuendelea kuwa kupewa heshima ya ubalozi.hakustahili kabisa kuwa nawadhifa huo mpaka muda huo. Safi sana Mh Rais,hongera sana mama yangu kwa hatua hii ya kishujaa na kijasiri inayoendelea kuungwa mkono na wengi.
Pambana mkuu, one day Yes. Unaweza ukateuliwa
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023.
Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017

View attachment 2735983

=====
WILLIBROD PETER SLAA NI NANI?
View attachment 2735984
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).

Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
View attachment 2735986
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

Pia, soma: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!
Mazao ya dhambi ya usaliti yameiva, ikibidi kama alivyofurahia wakati alipandikiza usaliti, afurahie yakati hizi za mavuno pia!
 
Unafki hautaisha miongoni mwetu kwa sababu ukisimamia ukweli, au ukiongea kinyume na aonavyo alie juu ya yote unavuliwa kunzia nguo mpaka utu!
Hatujasahau ya ndugai bado! Ni jinsi gani inatupasa kutafakari upya aina ya viongozi wanapaswa kutuongoza
 
Avuliwe tu, kipindi Cha Magu alikuwa kimya analamba asali baada ya kuwekwa kando ndio analeta choko choko. ...Safi Samia hakuna kucheka na wanafiki
Sasa hebu elezea maisha yako na ukoo wenu yatabadilika vipi kwa yeye kuvuliwa Ubalozi, yaani
 
Kwingineko, wanajeshi wanastaafishwa, hapa watu wanavuliwa ubalozi.

Africanism
 
Mbunge anawakilisha wananchi ndani ya jimbo.

Balozi anawakilisha nchi/rais nje ya nchi so ana play role as a president
Unajua Passport za Kidiplomasia wanapewa watu gani? Nazani kwa akili zako fupi unazania wanapewa Mabalozi pekee, rudi kasome,
 
Back
Top Bottom