DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023.
Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.
Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.
Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.
Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.
Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).
Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.
Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.
Pia, soma:
Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!