Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Ingawa ni baadhi yao ila kwa kiasi inazidi kudhihirisha mwanamke kuwa na madaraka ya juu ni tatizo katika jamii haswa kwa katiba kama yetu, sio mbali sana ya ndugai tulivyo shuhudia!
Akina Pendaeli tuliwambia jamami Katiba Hii utaipenda tu kama madarakani lakini wakishika wengine ndio utaona uchungu wako. Haya sasa.
 
Zaidi na Zaidi wamefanya Watanzania waanze kuelewa kwamba kuwa swala la bandari ni jambo nyeti sana na ni wazi serikali kuna inacho tetea na kulazimisha!
Hadi mimi mtanzania nisiyekuwa nafuatilia hili suala,nitaanza sasa kufuatilia


Wamenifumbua macho.
 
Msomi wa darasani Dr. Wilbroad Slaa (PhD) ina hadhi kuliko hata ule ubalozi wa kwenda kuzurura kwenye nchi za watu.
 
Huyu mama abdul atakwama tu kanda ya ziwa, CCM kazi mnayo 2025, mtaibaaa wee ila safari hiiiiiii safari kurahii haziibiki....

Kanda ya Ziwa, chimbuko la mabadiliko.
 
Hii imeknyesha serikali ya Dr Samia ni ya hivyo..wangemuachia ubalozi wake ingekuwa na manufaa Kwa upande wako kuliko walivyomuvua
Huwezi jua kuvuliwa hadhi ya ubalozi imemaanisha nini ?

hata kutupilia mbali suala la Katiba mpya pia ni Siasa

Rais alishauriwa sana kuhusu namna ya ku deal na Wapinzani akamuona JPM kama vile hakuwa na ubinadamu sijui hakuwa na utu ! sasa kaelewa bila shaka na nginja nginja mpaka baharini ya Dr Salmeen Amour na Hayati Mzee Mkapa inafanyiwa majaribio na kuna Mjinga mjinga atajichanganya atafanyiwa majaribio
 
Wewe mzee hebu jitafakari kama akili yako ipo sawa. Ulianza kuvuliwa upadri , Ukaingia kwenye siasa Chadema wakakuvua uanachama baada ya kusaliti chama chako na kuingia CCM. Leo hii tena umevuliwa Ubalozi cheo ulichopewa na CCM baada ya kuhama kutoka Chadema.

Kama mtu mzima lazima ujiulize wewe una matatizo gani? Kwanini kila ulipo jamii inakukataa.?

Nakushauri achana na mambo yote kaungame kanisani kwako ubaki muumini wa kawaida na utubu kwa Mungu akusamehe makosa yako.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Anatetea Taifa ....sio vyeo kibinadamu.....wanaojua historia nchi hii huyo ndio mpinzani no 1 1995 mbunge Karatu wa CDM.....aliwasumbuaaa.....uliza ujue
 
Msomi wa darasani Dr. Wilbroad Slaa (PhD) ina hadhi kuliko hata ule ubalozi wa kwenda kuzurura kwenye nchi za watu.
CCM wameonyesha kufeli, kila mtanzania kachukulia hili kama chuki binafsi.
 
We Slaaa kwa Umuri wake haihitaji hizo mbbwe, nyie ndio wale mnashinda kubeti badala ya kupigania nchi, endelea kubet na kuwaza kwamba sasa Slaa atakoma.

Kwani wakati hajawa Balozi si alikuwa ana safiri? Kuna alicho kuwa anapungukiwa akisafiri?
Siwez kukulaumu kwa kuniita mimi nashinda kubet sababu we are anonymous hapa jf.

Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa system ilimtumia dr slaa na baada ya kumalizana nae yeye mwenyewe akafanya mistake ikapata chance ikamdump
 
Kukataliwa na Mpumbavu, sio dhambi.



Kukataliwa na CDM, ilikua ni Haki ya Dr Silaa, kuandaliwa kugombea URAIS Kwa miaka mitano, na dakika za mwisho unapotezewa na kupewa mamuluki, kama mwanaume unayejielewa, lazima uchukue HATUA.



Kukataliwa Upadre, silizungumzii kwakua Sijui taratibu zao.



Bibi yako kazidi kuwaonyesha Watanzania kua Ana Kichwa Cha kuvukia Barabara na kusifia vifua vya wanaume, kuoa Wanawake wawili na maujinga ujinga kama hayo.

Kwa ufupi, URAIS umekua mkubwaaaaa, kapwaya pwaa pwaaa pwaaa
 
Msomi wa darasani Dr. Wilbroad Slaa (PhD) ina hadhi kuliko hata ule ubalozi wa kwenda kuzurura kwenye nchi za watu.
PhD ya Theology aliisaliti kwa kuparamia Wanawake na Ubalozi pia kaunajisi kwa kujaribu kukalia ncha ya Mkuki
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023.
Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017

Julai 22, Dkt. Slaa aliizungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari akisema ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Aliweka wazi kuwa hapingi uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam bali anapinga mkataba wa uwekezaji kwa kueleza kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Aidha, siku alisema kuwa “Najua maneno hayo ni makali… nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini najau ninachosimamia“

View attachment 2735983

=====
WILLIBROD PETER SLAA NI NANI?
View attachment 2735984
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).

Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

Pia, soma: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!
Hili limama hili[emoji57][emoji57][emoji57]
 
Siwez kukulaumu kwa kuniita mimi nashinda kubet sababu we are anonymous hapa jf.

Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa system ilimtumia dr slaa na baada ya kumalizana nae yeye mwenyewe akafanya mistake ikapata chance ikamdump
Ni Kama Ndugai tu😆😆😆
 
Back
Top Bottom