Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Kuondolewa ubalozi ina impact gani kwenye uchumi wetu?
 
Nyie ni wale wajinga wa jukwaa? Huu ushuzi kawaeleze wazee vijiweni juenda wakanunua huu ushauri wako
Tatizo lenu mukiambiwa ukweli munavimba nusura ya kupasuka ila usisahau kinachokupa hiyo jeuri ni amani iliyopo hapa nchin unayotamani itoweke kwa maslahi ya usiowajua japo unajihis shujaa
 
Acha upotoshaji wa kijinga, Slaa hakuvuliwa upadre bali aliamua kuachana na upadre. CDM hakufukuzwa bali aliondoka baada ya CCM kumpokea fisadi Lowassa. Ubalozi wa Tanzania nao ni kitu cha kujivunia, ungekuwa ubalozi wa US hapo wangalau.

Hapa ndio imedhihirika hivi vyeo ni kwa ajili ya kuwafunga watu midomo. Kumvua Slaa ubalozi baada ya kupigania raslimali za nchi ni sifa wala sio aibu. Labda kwenu chawa ndio mnaona ni pigo.
Kwanza Upadri huwa hauvuliwi unaweza kuavhwa usitoe huduma ila unabakia na Upadri wako maisha yote
 
Kumbe ata ukitenguliwa unakuw bado VIP katk hadhi ya x- balazo had rais akuvue kbsa
Niliwahi kusikia mahali kuwa cheo na hadhi ya ubalozi huwa havifutiki....yaani ukishapewa hiyo hadhi ya balozi basi ni moja kwa moja wanasema once a soldier always a soldier
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023.
Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017

Julai 22, Dkt. Slaa aliizungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari akisema ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Aliweka wazi kuwa hapingi uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam bali anapinga mkataba wa uwekezaji kwa kueleza kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Aidha, siku alisema kuwa “Najua maneno hayo ni makali… nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini najau ninachosimamia“

View attachment 2735983

=====
WILLIBROD PETER SLAA NI NANI?
View attachment 2735984
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).

Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

Pia, soma: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!
Na Magufuli atavuliwa urais hivi karibuni, kisa ni waraka wa TEC. Wakatoliki mjiandae kwa visasi
 
Yaan chukinwaliyonayo watu dhidi ya mama naona atavunja recodi ya magu
Rais samia anapendwa sana na mamilioni ya watanzania ndio maana Anaendelea kuungwa mkono kila kona ya nchi yetu. Kama humpendi ni wewe na familia yako tu ambayo unaweza kuta hata mkeo anampenda na kumuunga mkono mh Rais wetu , kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wote.
 
Niliwahi kusikia mahali kuwa cheo na hadhi ya ubalozi huwa havifutiki....yaani ukishapewa hiyo hadhi ya balozi basi ni moja kwa moja wanasema once a soldier always a soldier
Leo umejua sasa kuwa haikuwa kweli ... hongera
 
Machafuko yapi unayoyazungumzia wewe ambayo hayapo?? Kijana graduate kuwa dereva wa bodaboda sawa na yule form four failure, wewe hauoni kama hayo tayari ni machafuko??
Hujui unachozungumzia hivi hamujifunzi kwa nchi za wenzenu? Au umezaliwa jana jion hujui historia
 
Rais samia anapendwa sana na mamilioni ya watanzania ndio maana Anaendelea kuungwa mkono kila kona ya nchi yetu. Kama humpendi ni wewe na familia yako tu ambayo unaweza kuta hata mkeo anampenda na kumuunga mkono mh Rais wetu , kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wote.
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Vyovyote Vile, Ila Huwezi Kuelewa Umuhmu Wa Amani Mpaka Itakapo Ondoka, Huo Ujasiri Ulionao Hapo Wa Kuchukua Simu Yako Na Kuqoute Coment Yangu Ni Kwasababu Ya Hii Amani Unayotamani Itoweke Kwa Maslah Ya Watu Ambao Hawawezi Kukukmbuka Wewe Wakifanikisha Azma Yao
Nadhani huijui amani, bali unaondelea uoga. Jinsi mnavyopora uchaguzi na watu wako kimya hapo unaweza kujivunia amani? Ama hujui amani maana yake ni nini?
 
Back
Top Bottom