Rais Samia ana dalili za kuwa Rais bora kama Nyerere na Mkapa. Anaonekana kuwaacha mbali Magufuli na Kikwete

Kwenye suala la mafuta kupanda bei kakosea wapi? Na sisi tumrushie mawe
Leo spika anaasema Kuna tatizo mahali
Aliyeshinda kuleta mafuta keta kwa Bei ya juu kuliko iliyowekwa na TPDC.

Hadi hapo uone Kuna kitu hakipo sawa.

Lakini pia jiulize kwa nini Zanzibar mafuta ni nafuu kuliko huku?
 
Karibia kila nchi nchi isiyozalisha mafuta, kuna kilioi cha inflation lakini kelele anapelekewa Sa100

Kweli inflation inaathiri Dunia nzima lakini viongozi wa nchi mbali mbali wanatumia mbinu za kuhakikisha wananchi wao hawaumii kwa bidhaa kupanda bei huku mapato yao yako chini!! Sasa hawa viongozi wetu kutuambia tu kuwa huu mfumuko wa bei ni sababu ya vita ya Putin haisaidii kupunguza machungu ya wananchi wanayoyapata bila serikali kuchukua hatua kupunguza hizo bei za bidhaa!!! Rwanda na Kenya majirani zetu serikali zao zimechukua hatua kwa kutoa subsidies lakini sisi waziri wetu wa fedha hana ubunifu kwani ni mtupu anaishia kufunga skafu ya bendera ya Taifa tu na kuzunguzunguka huku akikashifu kuwa wasioweza vumilia wahamie Burundi!!!
Samia hana budi kuzinduka na kupanga safu ambayo itamnusuru na huu mfumuko wa bei; kuna nchi serikali iliondolewa madarakani kwa sababu ya bei ya mikate kupanda, hivyo isifike mahala uzalendo ukawashinda wananchi!
 
Kwenye suala la mafuta kupanda bei kakosea wapi? Na sisi tumrushie mawe
Kwenye suala la mafuta amekosea kule kuonesha kuwa she is in a hopeless situation na hana jinsi ya kujikwamua!! As ahead of State hatakiwi kuonesha kuwa ameishiwa options kunusuru wananchi kuhusu suala la kupanda bei ya mafuta!! Unfortunately amezungukwa na wasaidizi akiwemo waziri wake wa fedha ambao hawana weledi wa commodity trading ambapo wangeweza kutumia options katika bulk procurement ya mafuta wakati bei inategemewa kupanda hivyo kuweza kuthibiti bei ya mafuta!!!! Mbinu hizo ndio hutumiwa na makampuni makubwa yanayotumia mafuta mengi kama AIRLINES !!! Mwigullu ni mtupiu hana weledi huo!!!!
 
Saizi Sukuma gang na Chadomo kete yao ni Bei ya vitu kupanda eti wanategemea itawavusha hadi 2025 😀😀😀😀..

Ukiwaomba Sukuma gang waweke rekodi za mwaka mmja wa mtu wao vs SSH wanakwepa baada ya Samia kuwa outperform pakubwa ..

Utasikia miradi ya Magufuli,huwa nawauliza kwa nini miaka 6 hakumaliza mradi hata mmja at the same time wanataka Samia amalize ndani ya mwaka wake mmja na kuanza mipya 😆😆😆..

Uzuri wa Samia hapendi masifa ya kijinga wala kulazimisha kupendwa kwa maigizo na propaganda.za kitoto za shujaa wa Chato..

Sikiliza wabunge huko Bungeni wanavyofurahia mahela lundo kwenye Halmashauri zao hadi raha na wanakiri haijawahi kutokea Rais kutekeleza bajeti na ilani kama Samia.Huu ni ukweli mchungu watetezi wa legacy hawapendi kuusikia..

Ila kumfananisha na Nyerere,hapo hapana mkuu umezingua.
 
URAIS SI KUKAKAMAA USONI NARUDIA
Ndio umerudi JF kihivi? Sasa tofauti yako na kundi la watu kama Magonjwa, Jingalao na wengine wa aina hiyo itakuwa ipi?
Nimesoma kichwa cha habari tu, nikatosheka na kuamua kuandika haya.
 
Ila kumfananisha na Nyerere,hapo hapana mkuu umezingua
Imenibidi nivute hadi juu kuangalia mwandishi wa maneno niliyosoma toka mwanzo hadi mwisho. Ikanibidi ninyanyue huo mstari mmoja huo hapo mwisho, ambao ndio pekee ninaokubaliana nao katika andiko lako lote uliloweka hapo.

'The Sunk Cost Fallacy'?
 
Hivi wewe unajitambua kweli?watu wanajadili uozo wa serikali,serikali kushindwa kuongoza vizuri mfano bidhaa zinapanda bei ovyo,nchi inaenda ovyoovyo mawaziri wasio na sifa wamepewa wizara kuongoza wizara mbalimbali alafu unawaita watu sijui sukuma gang au chadema uozo wa serikali usiongelewe na watanzania?kama huna cha kuchangia ili nchi iende sehemu nzuri nyamaza.samia kauotperfom kitu gani miradi yote mikubwa ni ya magufuli,Hali ya uchumi bado ni mbaya tumerudi kwenye uchumi mdogo au Ka autperform kwenye kusafiri Sana kwa sababu Hali ya uchumi bado ni ovyo,miradi yotee ni ya magufuli.
 
Mapovu plus..

Unajua maana ya uozo? Vitu kupanda bei ndio kushindwa kuongoza? Mawaziri wasio na sifa na wenye sifa ni wepi? Kipimo Chao ni kipi?

Miradi yote mikubwa ni ya Magufuli,alikuwa wapi kuimaliza miaka yote 6 ya kuwa madarakani?

Hiyo miradi imesimama? Ulitaka imalizike kwa mwaka 1 wakati kuna Rais kashindwa kuimaliza kwa miaka 6?.

Uchumi mkubwa ulikuwa na faida gani ikiwa Serikali ilishindwa kukusanya mapato,ilishindwa kukuza Uchumi na ilishindwa kupeleka pesa kwenye miradi yote unayoita ya Magufuli,ilishindwa kulipa madeni ya wazabuni na wakandarasi na ilikuwa inaishi kwa mikopo huku ikidanganya wananchi kwa kuwatisha na propaganda..

Matokeo ya kuongozwa na wajinga ndio haya mkaanza kupora pesa kwa wafanyabiashara,,kubambikia kesi na kubargain kwa pesa,kubambikia Kodi,kupora pesa kwa machinga kwa kisingizio cha vitambulisho vya mjasiliamali,at last maisha yakawa hovyo,kaua kilimo hakuna hata bajeti ilipelekwa kusaidia kilimo.etc

Narudia tena weka metrics hapa za mwaka mmja wa Samia vs Mwaka 1 wa Magufuli maana ni wazi hadi 2025 Samia ataifunika hiyo legacy..

Kichaka ambacho nyie Sukuma gang na Chadomo mumebakia nacho ni kusema vitu vimepanda Bei,hoja ambayo ni ya kitoto kwa sababu it is a global phenomenon and the gvt is working on the best ways to mitigate its effects on people's welfare,and so utapata majibu PM anapo wind up bajeti yake..

Mwisho ni kwamba umejaa usaha kichwani ,chuki zinakusumbua ndio maana huwezi leta Takwimu hapa 👇





 
Imenibidi nivute hadi juu kuangalia mwandishi wa maneno niliyosoma toka mwanzo hadi mwisho. Ikanibidi ninyanyue huo mstari mmoja huo hapo mwisho, ambao ndio pekee ninaokubaliana nao katika andiko lako lote uliloweka hapo.

'The Sunk Cost Fallacy'?
Leta Takwimu blaa blaa za nini? Mnajaribu kumfichia aibu Dhalimu 😀😀
 
Sisi watanzania sijui tupewe nini tu? miezi 13 iliyopita hata ku comments post ya mtu ilikuwa lazima uangalie kushoto au kulia ndio ucomment.
Ni kweli. Yaani jamaa alikuwa ametufinya kweli kweli. Kuna unafuu sasa hivi Madame karejesha furaha kwa kweli
 
Asante kwa kufuta chaguzi zote za Urais japo haujatuambia mamlaka uliyonayo nchini.
 
Wewe na Uhasama wako utaacha lini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…