Rais Samia ana dalili za kuwa Rais bora kama Nyerere na Mkapa. Anaonekana kuwaacha mbali Magufuli na Kikwete

Basi hilo suala ni la Dunia nzima, kwa sababu hata Mmarekani, Germany inflation ni kubwa pia. Hamuongozwi na malaika.
 

Rais Samia ana dalili za kuwa Rais wa ajabu kuliko marais wote waliotangulia.​

 
Hili tatizo la mfumuko wa bei limerekodiwa kwa kiwango ambacho akijawahi kushuhudiwa Duniani. Nchi nyingi ni waathirika kwenye hili. Mmarekani, German, wanalia na huu mfumuko wa bei. Tafuteni taarifa.

Raisi akikosea tutaongea na akipatia tutamsifia na akibebeshwa mizigo isiyoyake tutaibeba tu.
 
Well said ! aongoze tu saiz hakuna kutekana tena pambavu mpaka wale waliohama chama wanarudi kwwnye vyama.vyao simba.wa.Yuda Has gone.
 
Umelipwa shilingi ngapi uhe uongee ijinga uku,au unalinda maslahi yako.maana sio kawaida mtu apege domo la propaganda zisizo na uhalisia bure bure.Maana kama mwaka mmoja tu wa rais huyu umeshamwona ni mzuri kuliko waliotangulia basi wewe huna faida yoyote kwenye hii nchi zaidi yakujali maslahi binafsi.
 
Hii vita ya putin mmeamua kuisingizia tu na kuifanya chaka la kujifichia bila sababu..mkibanwa kwenye hilo mnarukia kisingizio cha covid 19 utadhani imeanza mwaka huu..
sisi wakulima mmetunyanyasa sana msimu huu unaosha...mbolea ya kupandia ilipanda toka 54,000 hadi 120,000, Urea ilitoka 50,000 hadi 100,000, CAN ilitoka 40,000 hadi 90,000...hizo bei ni kwa maeneo yetu sisi kwa wengine huko sijui hali ilikuaje...njoo vifaa vya ujenzi,mafuta yote tu, Nyama, sabuni ni kila kitu in short...lakini sasa hivi mnaweka nguvu nyingi kutaka kuaminisha watu kuwa vitu vimepanda bei mwezi huu tu. acheni hizo basi
Aliibuka yule waziri wa biashara nadhani akajifanyisha kukemea na kuikumbusha FCC iingilie kati mwezi wa 10 mwaka jana ile nadhani,wafanyabiashara walimdharau tu,juzi kasema waziri mkuu, nadhani wafanyabiashara walivosikia kauli yake ile watakuwa walicheka tu
 
Acheni unafiki. Kwanza it is a crime before man and a sin before God.
Wakati wa mtu yule mlisemaga, mtu yule ndio rais Bora kabisa aliyewahi kutokea.
Wakati wa Nyerere vivyo hivyo leo Tena?
 
Leta Takwimu blaa blaa za nini? Mnajaribu kumfichia aibu Dhalimu 😀😀
"... Kumfichia aibu Dhalimu", yupi huyo ninayemfichia aibu?
Kujadili jambo na watu msiojitambua kama nyinyi inakuwa ni shida sana!

Sasa kwa kuwa wewe ni 'chawa' kwa huyo unayempigia upatu hapa, unadhani kila mtu ni lazima ajitoe akili kama unavyofanya wewe?
 
'Ota mswelani'.

Nimekusoma kwa mara ya kwanza humu JF. Nitaendelea kukusoma.

'mlaunu'?
 
Hakuna wa kufanana na Nyerere
Mwalimu aliipenda Tz na Watu Wake kwanza
Hakuendekeza upendeleo ulafi

Udini Ukabila aliukataaa
Sasa hivi tupo kwenye zama za ' mimi dini yangu ni mimi ni wa kanda ya mimi ni Kabila la.....
So tumheshimu Mwalimu Nyerere si wa kufananishwa na yeyote

Tz imepanda boat inakoelekea hakujulikani boat imeanza kujaa maji.....
Tuombe sana Neema Ya Mungu
 
Basi hilo suala ni la Dunia nzima, kwa sababu hata Mmarekani, Germany inflation ni kubwa pia. Hamuongozwi na malaika.
Hujajibu hoja bali unatetea upopoma, huko marekani Biden anahangaika kuwanusuru watu wake mpaka anadiriki kutumia EMERGENCY RESERVE ya mafuta ya nchi yao ili kupunguza maumivu ya kupanda bei!! Sasa sisi hapa Watu wanapokea mshahara na posho tu bila kufikiria kuwakwamua wananchi wao na machungu ya mfumuko huu!! Wamebakia kuimba tu vita ya Ukraine na Urusi ndio sababu, so what?
 
You can sai again and again 🔥🔥🙌
 
Wacha kulinganisha Marekana na vitu vya kijinga hata aibu uoni? Unaijua reserve ya Mmarekani??? Unataka Samia afanye kama Biden?? Poor comparison.

Kisa Biden kafanya unataka na Samia apite humo humo???
 
Wacha kulinganisha Marekana na vitu vya kijinga hata aibu uoni? Unaijua reserve ya Mmarekani??? Unataka Samia afanye kama Biden?? Poor comparison.

Kisa Biden kafanya unataka na Samia apite humo humo???

Wewe kifuu unasahau kuwa wewe ndio omeleta comparison ya Marekani na Ujereumani kuwa nao wana inflation!! Mimi ndio nikakuonesha kuwa huko Biden anagalau anajihangaisha kuthibiti mfumuko huku nyie mkiimba Vita ya PUTIN!!! Hamjisumbui kuthibiti watu wenu wanavyoibia nchi kwa dili za kijinga kupitia contract za kiwizi wizi mnabakia kulalama na kuimba taarab tu!! Chunguzeni hizo tenda za ununuzi wa mafuta muone jinsi hao mliowaweka kuongoza wanavyoihujumu nchi!!
 
Tunaposema ni tatizo la Dunia inflation, hiyo Marekani na German wapo Mars??? Humu ni for great thinkers only. Unatuchosha
 
Waziri mmoja aliropoka fedha Sasa imerudi mtaani,naombeni mniambie mtaa gani unahela nami nihamie huko maana mitaa yetu ya igomelo hela haipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…