Rais Samia ana dalili za kuwa Rais bora kama Nyerere na Mkapa. Anaonekana kuwaacha mbali Magufuli na Kikwete

Siko kwa mwendazake mimi na siutaki uongoz wa mwendazake hata kidogo, lakini siwezi kumsifia mama kwa kupandisha tozo za simu ambazo zimeleta maumivu kwa watu wa chini, so kwa kwahiyo uchumi ukiaribika duniani nawewe unakaa kimya watu wako waendelee kuumia bila kuchukua hatua yoyote yakunusuru maumivu kwa wananchi wako, Ndege mpya zinakuja sijui ni kikao kipi cha bunge kulipitisha hayo manunuzi, ni kama magu tu
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] muwe mnafuatilia Bunge la bajeti, tusichoshane. Bajeti imepitishwa trillion 37, inatoka wapi kama sio kukusanya kutoka kwa wananchi.

Msikatwe Tozo halafu muhoji barabara hazitengenezwi. Hospital hakuna dawa, shule hazijengwi.

Bajeti trillion 37, makusanyo ya TRA 1.8 trillion kwa mwezi. Kwa Mwaka hata haifiki trillion 23. Hiyo trillion 37 inafikiwaje bila kuchangia maendeo kwa njia ya Tozo,????

Tuweni realistic
 
Aisee!!!!
 
Tatizo la watanzania wengi ni kupenda mno kulalamika mpaka wanapoteza uhalali wa hayo malalamiko.

Umefuatilia hansard za bunge ukaona kuwa bajeti ya kununua hizo ndege hawakuipitisha?.
 
Huna taarifa ndio maana unalinganisha Kenya na Tanzania, Mwaka wa kumi na zaidi Kenya wanatambulika kama Nchi ya uchumi wa Kati, Tanzania tumeingia uchumi wa kati juzi na jana tumetoka. Solution anazochukua Uhuru Kenyatta ni kwa sababu nchi yake inamudu.
Huyu Mama anajitahidi kuweka weka na vitozo tu match na wenzetu bado mnamuita majina ya hovyo hovyo. Yaani pamoja na Tozo bado hatujaweza match hata na Wakenya bado mnalilia waondoe na hizo Tozo???? Maendeleo yenu yatachangiwa na nani????
 
Unasahau kwa makusudi kuwa hawahawa Mapaka(MaCCM) ndiyo wanatufanya tuingie uchumi wa kati na kutoka!Wanaopaswa kubeba lawama zote katika hilo ni hawahawa Mapaka.
 
Unasahau kwa makusudi kuwa hawahawa Mapaka(MaCCM) ndiyo wanatufanya tuingie uchumi wa kati na kutoka!Wanaopaswa kubeba lawama zote katika hilo ni hawahawa Mapaka.
Ndio mara ya kwanza tunapata kiongozi Mkuu Mwanamke, bado watu hawaoni anachofanya. Mimi nadhani support ni muhimu hata kwa hiki kidogo, pia akizingua tutaongea lakini sio kumtupia furushi la lawama kitu ambacho kipo nje ya uwezo wa nchi.

Hakuna mtawala anayependa kuongozi watu wenye simanzi. Hata wangekuwa CDM au Simba wa Yuda lazima mafuta yangewatikisa tu.
 
Kwamba ubora wa Rais unapimwa kwa kusema "UKWELI"?

Siku Mama yenu akitoka ndiyo mtaujua ukweli wenyewe.

Kwa sasa komaeni tu na mapambio
 
MAGUFULi BABA LAO

Mifumo ya kukusanya kodi Na Mapato kupitia control namba na kudai risit ya malipo yenye kodi ya TRA ni nani aliyeijenga na kuhakikisha inafanya kazi ktk nchi hii?

Hebu tuache ushabiki wa kimaamuma wa kumsakama mwendazake.

Mama yetu bado yuko kwenye teuzi tuache kumpamba.
 
Bunge gani unalolizungumzia wewe kifuu? Wabunge wako busy kujadili jinsi ya kupata special plate numbers za Magari yao hawana muda wa kufifkiria taabu za wananchi? Wewe unaishi Tanzania ya wapi? Nadhani uchawa unakusumbua. Kutumia wataalam wanaojua mambo ya commodity trading internationally hakuhitaji ridhaa ya bunge wewe chawa! Ufisadi ndio unaowasumbua kutaka kupiga cha juu.
 
Ngoja mchoro uishe kwanza ndipo ujue uzuri wake; mchoraji anaweka kalamu kwenye karatasi tu umeanza kusifia kabla hata hujaona ni picha gani inayochorwa? Tuliomsifia Magufuli wengi wetu ni wale waliomchukia sana tangu alipoteuliwa kuwa mgombea hasa kwa maneno yake ya majigambo, ila mchoro wake uliopoanza kuonekana kiutendaji hadi mwaka 2018 ndipo tukaona kuwa picha anayochora ni nzuri.

Your browser is not able to display this video.
 
Ila Urais mgumu sana,Obama aliondoka na Mvi, Mkapa aliondoka na upala, JK alichakaa chakaa , Magu alifia kabisa kazini.Biden kila leo wasemaji wake wanasahihisha kauli akikaa sawa anasema napenda ice cream.
Hii nafasi ni ngumu Tumuombee Mama aimalize salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…