Hii vita ya putin mmeamua kuisingizia tu na kuifanya chaka la kujifichia bila sababu..mkibanwa kwenye hilo mnarukia kisingizio cha covid 19 utadhani imeanza mwaka huu..
sisi wakulima mmetunyanyasa sana msimu huu unaosha...mbolea ya kupandia ilipanda toka 54,000 hadi 120,000, Urea ilitoka 50,000 hadi 100,000, CAN ilitoka 40,000 hadi 90,000...hizo bei ni kwa maeneo yetu sisi kwa wengine huko sijui hali ilikuaje...njoo vifaa vya ujenzi,mafuta yote tu, Nyama, sabuni ni kila kitu in short...lakini sasa hivi mnaweka nguvu nyingi kutaka kuaminisha watu kuwa vitu vimepanda bei mwezi huu tu. acheni hizo basi
Aliibuka yule waziri wa biashara nadhani akajifanyisha kukemea na kuikumbusha FCC iingilie kati mwezi wa 10 mwaka jana ile nadhani,wafanyabiashara walimdharau tu,juzi kasema waziri mkuu, nadhani wafanyabiashara walivosikia kauli yake ile watakuwa walicheka tu